Saturday 19 January 2013

Re: [wanabidii] Natamani kuwa mwanasiasa

Wadau Hilde na wapendwa wengine nawashukuruni kwa ushauri wenu kwangu na kwa Watz wengi. Pamoja na ukweli kwamba vijana wengi katika mahala pengi hapa Tanzania hawapendi kufanya kazi ili kujipatia kipato japo wanapenda kustarehe lakini haeli iko tofauti kdg huko Tarime. Vijana wa huko wanapenda kazi hata za kilimo ila kuna uhaba mkubwa wa ardhi may be kwa sababu ya overpopulation maana huko kwetu tabia ya kuoa wake wengi inafanya familia kuwa kubwa kubwa sana. Ndio maana vijana wengi wa Tarime wapo huku Dar wakifanya kazi mbali mbali tena ngumu. Pia kuna ujambazi uliokithiri ambao unadiscourage local investment. Nakubali kwamba natakiwa kutumia elimu yangu kuanza kusaidia vijana na akina mama wa huko kwetu ili wainuke kiuchumi badala ya kusubiri nipate nafasi ya kisiasa ndio nisaidie. Nitaangalia jinsi ya kuanzisha miradi ya aina hiyo.
Lakini lazima tukubali kwamba malezi tuliyowapa vijana wetu yanawapeleka kwenye janga maana kila mtu hataki kufanya kazi lakini anataka kutanua. Matokeo yake wakienda vyuo wanaishia kufanya uchangudoa na vijana wanaishia kutafuta mijimama ya kuwalea ili mradi waendlee kutanua! Lazima turudi kwenye basics yuwafundishe watu wapende kazi na wapate kipato halali

On Jan 19, 2013 7:24 PM, "Hildegarda Kiwasila" <khildegarda@yahoo.co.uk> wrote:

Wachache sana wa watanzania tunawaza haya mazuri uliyoyasema hapa. Tunapenda kulaumu serikali tu lakini hatuoni vibanzi vyetu na raslimali za pale tulipo na hatujitumi.

Unasaidia maandamano ya Gas lakini hufanyi maandamano kijijini walipo watu wako kuwajumuisha kulima mazao yanayoza kulimwa hapo kila mtu awe na shamba la chakula na la mazao ya biashara; kuboresha chanzo cha maji ambapo kila mtu anatumbukia ktk kibwawa anachota humo na kuchangia na mifugo ifugwayo na mafisi. Mawe yapo, mafundi wa kijijini wajengao majumba mpaka makubwa ya kisasa wapo na wakichanga kila kaya 200/=  kaya 1000 watapata laki 2 ni mifuko tosha ya siment ya kufanya reinforcement ya kisima kwa mawe zaidi ya kimoja na hela za kununua metal cover ya kufunika kisima na kufuri la kufunga. akija mgeni ananunua eneo anatutumikisha kulima na vijembe hivyo vya mkono, tunamuuzia eneo wenyewe, anatutuma kukata miti ya msitu wetu, tunabeba mkaa hela twanyea pombe. watu wanaitamani nchi hii. Lima wewe kashamba huko kijijini kama utafuna usipoweka mlinzi. Hao waliokaa bure na cutomary land yao vast ndio hao watakaokuwa wanavuna embe zako, mihogo mahindi wewe hupati kitu. wao ndio waliokuuzia ardhi lakini inakuwa kero kuishi hapo mahala unakuja kujuta. Wanakula papai mbegu wanatupa jalalani na makokwa ya embe. wewe unaokota jalalani au ukila unapanda lakini unakuwa huna amani na mpera, mchungwa, mlimao na mwembe wako, licha ya hayo mahindi. Ifike wakati tukubali kubadilika mijini na vijijini. Tuendako-kubaya.

--- On Sat, 19/1/13, Jovias Mwesiga <ngonzy@gmail.com> wrote:

From: Jovias Mwesiga <ngonzy@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] Natamani kuwa mwanasiasa
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Saturday, 19 January, 2013, 14:48

Victor kama kweli unataka kuwatumikia wananchi ziko njia nyingi sana, lazima utakuwa umejiona unakipaji cha uongozi au watu wamekuona hivyo unahisi ni muda wa kuangaza nyota yako hiyo uliojaliwa. Mie ningeshauri anza katika level ndogo katika mazingira yaliokuzunguka fanya mambo badiliso mtitazamo ya watu wako. Wafunguo macho waone kuanyomambo mengi wanaweza fanya si kutegemea serikali kwa kila kitu. Mfano kiunadhambi gani kujenga nyumba nzuri za walimu kwa shule za kata kunakoweza shawishi walimu wanaopangwa kazi huko kwenu wabaki na kuwafundisha watoto wenu badala ya wanavyokimbia vituo vyao vya kazi sababu ya kukosa hata mahala pa kulala.

Waonyeshe wananchi wako raslimali zao na jinsi wanavyoweza kuzitumia kuendeleza familia zao. Peleka mabadiliko ya elimu, kuwa chanzo cha usuruishi wa migogoro mbali mbali huo uwakilishi utakuja wenyewe and that is how u can build ur legacy

2013/1/17 Victor Mwita <victormwita@gmail.com>

Ndugu wadau
Kwa muda mrefu nimetamani kuwa mwanasiasa nikiwa na lengo la kuwawakilisha wananchi wenzangu mjengoni na katika fursa mbalimbali ndani na nje ya nchi. Ni kweli kwamba huko nilikozaliwa kuna matatizo ya msingi ambayo kwa miaka mingi hayajawahi kutatuliwa. Tatizo kubwa ni siasa na vyama vyake katika nchi hii. Ili kutumiza azma yako inabidi ku-sacrifice sana muda, rasilimali (fedha) na utu wako kwa chama chako but hayo yote hayakuhakikishii kuendelea kubaki katika chama. Wakati wa kutafuta ticket ya chama ili uwe mgombea wa nafasi yoyote kuna mizengwe kibao!! Kubwa mno ni hii tabia ya watanzania kutaka uwape kitu kwanza ili ukawawakilishe!
Kwenye vyama nako kumejaa watu wa kila aina. Mwanzoni nilidhani vijana wanaoingia katika siasa wako serious kutaka kuleta maendeleo katika nchi hii, kumbe wanatafuta ajira na fedha. Ndio maana wananunulika na wanasiasa wazee na kuishia kujaribu kuharibu sifa za vyama vyao.
Mambo haya yananifanya nianze kupata wasi wasi na mustakabali wa siasa za nchi yetu. Najiuliza maswali kadhaa yasiyo na majibu. Kubwa zaidi ni hili na wananchi kuhitaji kitu kidogo kutoka kwa wagombea kabla ya kuwachagua. Je waliochaghuliwa watakuwa wanawawakilisha hao wapiga kura waliohongwa au wanaenda kutimiza matakwa yao? Labda ndio maana wawakilishi wetu wakishafika mjengoni wanafanya kila wawezalo kujiongezea posho na mishahara mikubwa ili kupata mitaji wa kwenda tena kununua kura next elections. Tumeona wawakilishi huko Kenya walijiandalia pension ya nguvu. Na ninaamini hata hapa kwetu hilo linakuja.
Vijana amkeni msimamie hatma ya nchi yetu. Kumbukeni the country is bigger than the individual. Msitumike kuvuruga vyama vyenu kwa faida yetu sisi ambao miaka yetu inaelekea mwisho lakini bado tuna uroho wa madaraka. Fikiria iweje wewe kijana mzee akupe vijisenti kidogo ili akutumie kuharibu carrier yako yote katika siasa?! Just say no and stay focused.
Bado najiuliza kama niingie katika siasa za huko kwetu na niingie kwa style gani
--
Victor Caleb Mwita
P.O. Box 9152
Dar Es Salaam

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
0 comments:

Post a Comment