Sunday 6 January 2013

RE: [wanabidii] Mbunge wa Lushoto azomewa Kanisani

Erick,
Shida iko hivi, kwanza, unapowasalimia watu kwa kutumia salamu ambazo wewe na baadhi ya wanajamii wameshazichukulia kwamba ni salamu za kidini, unapigilia msumari tofauti za kidini miongoni mwa WATANZANIA, kwamba baada ya salamu hiyo kila mtu anaanza kujiangalia kwa dini yake na kumwona mwenzake kwamba si mwenzake kwa kuwa ana dini yake yenye salamu yake. Hili ni tatizo kubwa.
 
Pili, inakuwaje kwa Watanzania ambao si waislamu wala si wakristo? Ni tatizo pia. Wapo wa dini zingine na wasiokuwa na dini pia. Tunawadharau?
 
Tatu, inakuwaje kwa wakristo ambao hawatumii salamu hiyo au hawaiamini au hawaipendi au hawaijui? Hii si salamu bali ni kauli mbiu tu na inaweza kuchambuliwa na wataalamu na kuonekana kwamba haistahili kutumiwa hivyo.
 
Nne, inakuwaje kwa waislamu ambao hawapendi kuitumia salamu hii au hawatumii Kiarabu? Kumbuka, Uislamu si Uarabu na Uarabu si Uislamu. Mtume aliwataka waumini kuwa waungwana na kuwajulia hali watu wote lakini hakulazimisha kwamba Kiarabu ndicho kitumike.
 
Tano, hatukuwa na salamu ya namna hii huko nyuma; sasa tunawashwa nini?
 
Sita, ni muhimu kuelewa kwamba mambo ya siasa na ya dini yana mipaka yake katika ukristo, kwamba Yesu alifundisha vema akisema yale yaliyo ya Kaisari mpeni Kaisari na ya Mungu mwachieni Mungu. Hili fungu lina maana yake kubwa zaidi na si kwamba Yesu alikuwa akisemea suala moja la kodi ama hela tu. Biblia inafundisha vema na ukisoma kwenye 1 Samweli 8 - sura yote, utaona jinsi Mungu alivyokuwa akimtuma Nabii wake Samweli aende akawaeleze wana wa Israeli tofauti ya kuwa chini ya Mungu na kuwa chini ya utawala wa kibinadamu - kwamba hizi ni tawala mbili tofauti. Watu wale wakaidi wakachagua kwenda na utawala wa kibinadamu wa kifalme na waachana na utawala kiungu. Msisitizo wa Mungu ulijengwa juu ya hoja kwamba SIASA na DINI ni vitu viwili tofauti na huwezi kuvichangana. Hakuna kuchanganya.
 
Saba, ingawa katika dini ya kiislamu kuna mafundisho kwamba Uislamu unajumuisha maisha yote na mazina ya mwanadamu, hii ikimaanishahata utawala wake wa kisiasa, lakini pia ni dhahiri kwamba SIASA bado inabaki na mahali pake na ndiyo maana Iran mathalani wana serikali mahali pake chini ya rais na dini iko mahali pake chini ya Ayatollah. Hali kadhalika, Saudia, ina mfalme wake na heshima ya dini iko mahali pake. Nchi zote za Kiislamu zinazofuata Uislamu katika katiba zao zinatenganisha mambo haya inapofika kwenye utendaji na kisichotenganishwa ni IMANI inayomwongoza muumini ambaye ni kiongozi pia. Fanya utafiti uone. Kwa hiyo huwezi kuwalazimisha watu wachanganye siasa na dini kirahisirahisi namna hiyo.
 
Niishie hapo, kama kuna lenye dosari, nitafurahi kurekebishwa na nitapokea ushauri lakini ukweli unabakia hivi - hizi salamu zinazotumiwa na wanasiasa uchwara siku hizi ni UPUMBAVU na hazitaisaidia TANZANIA wala WATANZANIA. Ni upumbavu mkubwa kuwabagua na kuwapambanisha watu kichinichini bila kujijua kwa salamu tu. Kwani Kiswahili kimekosa salamu? Kwa utamaduni wetu hauna salamu zake? Ni ULOFA wa mawazo tu kuziendekeza hizi salamu.
 
Tuwe waangalifu, siyo kudakia tu kila upupu.
 
Matinyi.
 

To: wanabidii@googlegroups.com
From: matinyi@hotmail.com
Subject: Re: [wanabidii] Mbunge wa Lushoto azomewa Kanisani
Date: Thu, 3 Jan 2013 16:16:51 -0500

Erick,
Nitakupa upande wangu. Hatari moja ya haya mambo ni kuwa na watu kama wewe.
Mnachanganya tu.
Matinyi.




T-Mobile. America's First Nationwide 4G Network

----- Reply message -----
From: "Erick Mathew" <mathewerick@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Subject: [wanabidii] Mbunge wa Lushoto azomewa Kanisani
Date: Thu, Jan 3, 2013 3:36 pm


Habari wanabidii!napenda kujibu kauri ya matinyi, anataka kupotosha umma au la atuambie kua yeye ni mpagani mpiga ramli na mtesa watu-
ndio kazi ya wasio mwamini mungu ambao ukijenga nyumba nzuri kuliko yake kesho yake unajikuta umelala kando ya mto au kugezwa msukule maana ndio shughuli yao!
Nataka aniambie anacho amini kati ya dini hizi kuu mbili,ili nimsaidie,ukristo or uislam!maana hakuna imani icyokua na alama yake ya utambulisho,hata vyama vya siasa vina utambulisho wao,na freemason pia wanao!Shekhefu alifanya kosa kubwa sana,angekua msikitini wangemtoa na bakora angelijua jiji!




________________________________
From: "matinyi@hotmail.com" <matinyi@hotmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, January 3, 2013 8:04 PM
Subject: Re: [wanabidii] Mbunge wa Lushoto azomewa Kanisani


Issa,
Haya, sawa, hiyo salamu ni ya kiislamu. Hapo ndipo ilipo hoja yangu, kwamba dini zikae mahala pake. Basi.

Shekifu huwa anaanza na hii na anamalizia na ya Bwana Yesu akiamini anawakosha watu wa dini zote. Huu ndio upuuzi kwenye siasa, tena mkubwa.

Tusibaguane, hata kwa mema.

Tanzania na siasa zake zisiwe na dini.

Matinyi.



T-Mobile. America's First Nationwide 4G Network

----- Reply message -----
From: "Said Issa" <saidissa100@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Subject: [wanabidii] Mbunge wa Lushoto azomewa Kanisani
Date: Thu, Jan 3, 2013 11:56 am


Kaka Matinyi,
You are misleading the guys na unafanya makosa. Wewe huijui dini ya kiislamu na huwezi kuandika kama alivyoandika hapa chini.
Ni kweli labda kwenye Kurani haimo salam - ngojea nitafute, lakini kwenye nguzo moja ya uislamu ambayo ni sala tunatakiwa tutoe salam mara mbili na tuseme 'assalaam alaykum' kwa upande wa kulia na 'asslaam alaykum wa rahamatullahi ' kwa upande wa kushoto - kama vile tunavyoamkiana na  ndio tuweze kumaliza sala.
Pia, uislamu sio Kurani peke yake. Mengi aliyoyafanya Mtume wetu Mohammad (SAW) ni part ya uislamu na mpaka mwisho inasemwa kuwa..."he who obeys Mohammad is indeed obeying Allah".
Mtume wetu akitoa salam popote pale anapowakuta watu - sio waislamu tu. Kufanya alilokuwa akifanya yeye kwetu ni sunnah (yaani jambo zuri) na linafaa.
Kwa bahati mbaya dini yetu imeshushwa kwa kiarabu, lakini hii haina maana tuchukie kila kitu cha waarabu.

Shekifu sio muislamu. Ninamjua vizuri sana - he is a very jolly guy. Yeye anafuata trend ya mambo yanavyokuenda tu na sio kwamba katoa salam kwasababu ni muislamu. Ni kweli katoa salam pahala sipo, lakini hii haina maana kwamba kutoa salam ni upuuzi na ujinga.
Hakuna haja kuumizana imani zetu unnecessarily!

.....bin Issa.




________________________________
From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
To: Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Thursday, January 3, 2013 8:32:22 AM
Subject: RE: [wanabidii] Mbunge wa Lushoto azomewa Kanisani



Kiukweli kabisa, salamu si dini. Dini ni utii wa mwanadamu kwa Mwenyezi Mungu. Kuitumia salamu visivyo ni tatizo.
 
Biblia haijamfundisha muumini yeyote salamu ya "Bwana Asifiwe" au "Tumsifu Yesu Kristo". Huu ni ubunifu tu wa watu na hauna ulazima wowote kufuata; sana sana ni ujuha tu. Mbona zamani hii salamu haikuwa na umaarufu huu? Wa nini leo kama si ulofa wa mawazo tu na hisia?
 
Kurani haijamfundisha muumini yeyote salamu ya "Asalam Aleikum" bali hii ni salamu ya Kiarabu, kama zilivyo "Ugonile" kwa Kinyakyusa au "Oyimore" kwa Kijaluo, au "Salut" kwa Kifaransa, au "Konichiwa" kwa Kijapani, au "Namaste" kwa Kihindi, n.k. Hakuna dini kwenye hii salamu na ndiyo maana hata Waarabu wakristo wanaitumia.
 
Hivyo, kuzitumia salamu hizi kwa kudhani kwamba ni kuziheshimu dini si sahihi. Hilo moja. Ni kujichanganya na kupotosha umma.
 
Pili, unapowasalimia Watanzania kwa dini zao, je, inakuwaje kwa wale wasiokuwa na dini hizo? Je, vipi kwa wasiomwamini Mungu? Je, vipi kwa Wakristo wasiotumia salamu hizo? Inakuwaje kwa muislamu asiyekitumia Kiarabu mathalani yile wa Bosnia au Uchina?
 
Lakini mbaya zaidi ni kujikuta kwamba tunajenga mbegu mbaya ya kujitambulisha kwa dini zetu badala ya utu wetu na Utanzania wetu. Hili ni jambo la hatari na linapaswa kupigwa vita na wote wanaoitakia mema Tanzania na wenye ufahamu wa wanachokisema na kukifanya; tusiendeende tu kama maboya majini, tutakuja kujuta. Hii ni mbegu ya kibaguzi na ni ulofa wa kiitikadi, kisiasa na ugonjwa wa kutojifahamu. Kwa nini unataka usalimiwe kwa unachodhani ni dini na wakati si lolote si dini?
 
Tanzania ni nchi ya Watanzania; siyo nchi ya Wakristo na Waislamu.
  
Matinyi.

 


________________________________
Date: Thu, 3 Jan 2013 08:26:11 -0800
From: bertmutta@yahoo.com
Subject: RE: [wanabidii] Mbunge wa Lushoto azomewa Kanisani
To: wanabidii@googlegroups.com


Kama wanasiasa na watu wengine hutumia salaam za aina tatu majukwaani kujali makundi matatuya kiimani  (asalaam alikum, Bwana Yesu asifiwe, Tumsifu Yesu Kristu)  basi asalaam aleikum sio sahihi tukiwa kanisani. ELIMU YA KUKARIRISHWA

Gosbert Mutasingwa
P.O Box 40
Biharamulo
KAGERA-Tanzania
0784 857 775/0758 491 247

--- On Thu, 1/3/13, Juma abdallah <juma.abdallah@huawei.com> wrote:


>From: Juma abdallah <juma.abdallah@huawei.com>
>Subject: RE: [wanabidii] Mbunge wa Lushoto azomewa Kanisani
>To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
>Date: Thursday, January 3, 2013, 5:49 AM
>
>
>
>Asalam alikum-Amani ya bwana iwe juu yenu
>Waalaikum salaam- Nanyi juu yenu iwe amani ya bwana.



>From:wanabidii@googlegroups.com [mailto:wanabidii@googlegroups.com] On Behalf Of Reuben Mwandumbya
>Sent: Thursday, January 03, 2013 3:05 PM
>To: wanabidii@googlegroups.com
>Subject: Re: [wanabidii] Mbunge wa Lushoto azomewa Kanisani

>Salim;
>Katika uhalisia Shekifu kakosea,alitakiwa kusoma mazingira asikwaze wengine.
>Salamu hii ni ya Kiarabu hata kama maana yake kwa kiswahili ni Jambo lakini haikutakiwa pale,then bado kachanganya dawa zinazoripuka.
>Pamoja na kwamba wapo Waarabu Wakristo ukweli unabaki kwamba sio asili yao,inawezekana walislimu kama wengine wanavyofanya

>Reuben
>
>________________________________
>
>From:Salim Rupia <zabarelo@gmail.com>
>To: wanabidii@googlegroups.com
>Sent: Wednesday, January 2, 2013 11:08 PM
>Subject: Re: [wanabidii] Mbunge wa Lushoto azomewa Kanisani
>
>
>
>Sikuwepo, labda ilikuwa Swaumu hiyo nyingine lakina alikuwa na Sheikh Ramia Bagamoyo na kichwa kilimuuma sana siku hiyo na pia hapa nam "quote" yeye mwenyewe kwenye hotuba zake; ukipenda kusikiliza utasikia.
>Lakini sikuwa na maana ya kuchanganya hoja na Swaum; tuseme nimekosea. Vipi kuhusu hiyo Salaam? Maana ndo hoja nilochangia kuna mtu alisema ya kijinga na upumbavu...
>2013/1/3 Reuben Mwandumbya <ipyana75@yahoo.com>
>Salim usitupotoshe tafadhali;
>Au labda upe ufafanuzi swaum unayoongelea hapa ni ipi?kama ni ya Kiislamu hutakuwa sahihi.
>Hata Wakristo tunafunga na tunakuwa na swaumu wakati wa mfungo wetu kipindi kuelekea PASAKA.
>So dont mix up issues.

>Reuben
>
>________________________________
>
>From:Salim Rupia <zabarelo@gmail.com>
>To: wanabidii@googlegroups.com
>Sent: Wednesday, January 2, 2013 10:44 PM
>
>Subject: Re: [wanabidii] Mbunge wa Lushoto azomewa Kanisani

>Jamani, "Asalaam Alaykum" ni sawa na "jambo?"; yaani greetings" tu  ila kwa lugha ya Kiarabu.
>Mnajua kuwa kuna Waarabu Wakristo na wanasalimia hivyo hivyo?
>Na ujinga na upumbavu unaosemwa hapa ni wa salaam hiyo na walioanzisha ama ni huyo Muumini binafsi?
>Mi namkumbuka Mkatoliki mmoja aliekuwa hadi anafunga Swaum ndiye aliehamasisha sana kusalimia kwa salaam hiyo majukwaani; alikuwa Mkuu wa kwanza wa Nchi hii. Tunasemaje hapo...
>Huyo M bunge alikosea sana kwa kuwa kama wengi waliochangia wanavyosema, inawezekana alikariri salaam; kuwa akiwa mbele ya watu wengi aanze na salaam hiyo bila kukumbuka mkusanyiko ule ulikuwa wa watu gani.
>Mi nakumbuka wakati wetu kwa wale tulopita National Service (JKT) ukipangwa ulinzi "Main Gate" kuna amri na maswali ambayo unakariri kuuliza kwa kila dereva wa gari litakalotaka kuingia kambini. Tulikuwa tunawatania kina "green kwanja" kuwa wao hata mchana watamwambia dereva "zima taa za mbele, washa taa za ndani" kwa kuwa hiyo ndo ilikuwa amri ya kwanza! Kisa; kukariri...
>2013/1/3 matinyi@hotmail.com <matinyi@hotmail.com>
>Hizi salamu ni za kijinga mno mno. Sijui huu upumbavu ulianzishwa na nani? Yaani tu taifa la ajabu sana.
>Matinyi.
>
>
>
>
>T-Mobile. America's First Nationwide 4G Network
>
>----- Reply message -----
>From: "godfred mbanyi" <mbanyibg@yahoo.com>
>To: <wanabidii@googlegroups.com>
>Subject: [wanabidii] Mbunge wa Lushoto azomewa Kanisani
>Date: Thu, Jan 3, 2013 5:14 am
>
>
>Huu unafiki wa kisiasa utawaponza wengi!!! Utakuta kiongozi ni mwislamu safi, swala zote na hija ameenda, lakini anasimama kwenye jukwaa la siasa na salaam za " Tumsifu Yesu Kristo"!!!!!!!!!! Kisa, kutafuta sapoti ya wapiga kura!!! Asifiwe, mtu usiyemwamini?
>
>
>
>--- On Thu, 1/3/13, magreth Mulokozi <m.mulokozi@gmail.com> wrote:
>
>
>From: magreth Mulokozi <m.mulokozi@gmail.com>
>Subject: Re: [wanabidii] Mbunge wa Lushoto azomewa Kanisani
>To: wanabidii@googlegroups.com
>Date: Thursday, January 3, 2013, 2:07 AM
>
>
>Duu anatafuta kura  za 2015 sasa , duu  pole sana Nd Shekifu
>
>
>
>2013/1/3 matinyi@hotmail.com <matinyi@hotmail.com>
>.....alikariri.....siyo alikalili.
>
>
>
>
>
>T-Mobile. America's First Nationwide 4G Network
>
>
>
>----- Reply message -----
>From: "adeladius makwega" <makwadeladius@googlemail.com>
>To: "mabadilikotanzania" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>, "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
>Subject: [wanabidii] Mbunge wa Lushoto azomewa Kanisani
>Date: Thu, Jan 3, 2013 4:46 am
>
>
>Shekifu aunza mwaka mpya Vibaya
>
>Mbunge wa  Lushoto Hendry Shekifu ameuunza  mwaka wa 2013 vibaya
>baada ya kuzomewa Kanisani  na  waamini katika    sherehe  za  mwaka
>mpya baada ya kupewa nafasi ya  kuwasalimu washirika wa Kanisa Kuu  la
>KKKT  Lushoto Tanga.
>
>Ibada hiyo ya kuukaribisha  mwaka  mpya ilianza kwa  waumini kupokea
>mahubiri  ya  mwaka mpya  yaliyohubiriwa na Mchungaji Walelaza  na
>baadae kufuatiwa na ibada  ya ubatizo ambapo watoto wawili kutoka
>familia  mbili walibatizwa.
>
>Mara baada ya  ubatizo huo  ibada  ilifuatiwa na utoaji wa  Sadaka
>huku  mbunge  huyo wa  Lushoto akionekana  kushiriki  kikamlifu
>katika  ibada hiyo .
>
>Akiwa  amevalia  suti  ya rangi  nyeusi  yenye mistari    midogo
>midogo  miyeupe Mbunge Shekifu ambaye  aliwahi kushika nyadhifa
>mbalimbali zikiwamo ukuu  wa mkoa alipewa nafasi ya kusimama  mbele ya
>waamini mithili ya  kasisi.
>
>Nafasi hiyo ilitolewa  wakati wa  Matangazo  huku  mchungaji
>akiwaomba  waumini hao  kumsikiliza Mbunge wao ili awasalimu. Basi
>Mbunge  Shekifu alisimama  huku akiweka    vizuri koti   kwa kujifunga
>vifungo vya koti hili ambalo  lilionekana  kuutosha  mwili wake
>mkubwa  uliojengeka  vizuri.
>
>Alikisogelea kipaza sauti  mara  alianza kuongea   kwa
>kujiamini."Aslaam Aleikumuuu…" Duu  utangulizi huo  uliharibu  hali ya
>hewa  ya kanisa hilo wauumini kuanza  kuzomea na kuguna   kutokana
>salaam  hiyo  iliyotolewa  mwanzoni  katika  sehemu  isiyo sahihi.
>
>Hali hiyo iliwafanya waumini hao  kuibua  munkali huo kutokana na
>kitendo cha  mbunge  huyo  pengine  kukalili namna  ya kusalimia watu
>katika  majukwaa ya kisiasa  bila ya kujua kuwa  sasa  madhari
>aliyokuwa nayo ilikuwa  ya  salaam moja  tu   kama sikosei ni Bwana
>Yesu asifiwe au  Tumsifu Yesu Kristu.
>
>Hekima  ilitumika   pengine  huku  yule aliyempa nafasi ya kuwasalimu
>wauumini wake akijilaumu kuitoa  nafasi hiyo iliyotia  shubiri
>kanisani hapo na kuibua  zomeazomea hiyo  ambalo  sio  jambo la
>kawaida  kwa waumini kufanya hivyo.
>
>Mchungaji Walelaze  ilibidi  kuinuka na kusema waziwazi  kuwa  Ndugu
>Shekifu umekosea  sana kwanza  ulitakiwa  kujitambua kuwa  wewe
>japokuwa ni  Kiongozi  pia wewe ni mkiristu   lolote utakalo fanya
>popote  pale    tambua     unamajukumu mawili kwanza  ukiristu wako
>na pili   kuwa  kiongozi.   Hapa ni kanisani  ulitakiwa kuwasalimia
>waashirika  kwa   salaam   yao  siyo salaam hiyo uliyoitoa hapa.
>


--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment