ndicho ambacho nilitaka kusema kwanza viongozi wetu, wawe makini na kauli zao lakini pia na sisi kama wadau tusiwe na jazba hata katika mambo ambayo hayajengi;
ni kweli pia kimantiki pale Shekifu hakutakiwa kutoa salamu hiyo lakini kwa kuzingatia msingi wake ni mkristo hakupaswa kudhalilishwa kwa hilo nadhani angepewa muda zaidi angeweza kufafanua ni kwanini alianza na salamu hiyo.
narudia tena hili ni funzo kwetu sote twendako sio salama nipo ofisini na wadau hapa wanasema ifike mahala tuwe na salamu moja ya kitaifa je inawezekana?
On Mon, Jan 7, 2013 at 4:14 PM, Lemburis Kivuyo <lembu.kivuyo@gmail.com> wrote:
This message is eligible for Automatic Cleanup! (lembu.kivuyo@gmail.com) Add cleanup rule | More info
Ndg yangu Mussa uko sahihi kwa upande wako lakini upande mwingine wa shilling hauko sahihi. We fikiria wewe ndio unajua hilo na wale washirika wa kanisani wengi innocent ignorant. Siku zote wao wanaamini Asalam Aykum ni salamu ya kiislamu na ili uwatoe hiyo itakuchukua miaka 20. Katika jamii wewe muelewa ndio unatakiwa kuchukua hatua na kusema sawasawa na wale watu wanavyoiamini.Shekifu alikosea na tunachotakiwa kujifunza hapa ni kuwa uelewa wa jamii hazilingani na sisi wanasiasa au wataal ambao tuna exposure kubwa kuliko waoTalk the way the community expect you to talk
Ngoja nikupe mfanoKuna sehemu nyingine wakristo wale wale ukiwasalimiaTumsifu Yesu Kristo unawakwaza kwa sababu wao sio wa hiyo salamuWengine Bwana Asifiwe unawakwaza kwa sababu wao sio wa hiyo salamuKwa wengine Bwana apewe sifa unawakwaza kwa sababu wao sio wa hiyo salamu
Hata kwa wasilamu nmaamini pia kuna tofauti hizi pia--
Real Change for Real Development,
Lemburis Kivuyo+255654650100/078 7665050/0755646470Website: www.kivuyo.com, Skype: lekivuyo, Facebook: http://facebook.com/lemburis.kivuyo, Titter: http://twitter.com/lembu1, Linkedin: http://tz.linkedin.com/in/lembukivuyo, Google+: gplus.to/lembukivuyo2013/1/7 mussa juma <mussasiwa@gmail.com>SHEKIFU hakukosea.
WADAU katika mjadala huu, Mbunge huyu, hakukosea kwani salamu hiyo haina tatizo, kwa tafsiri yangu ndogo Mtu kusema: Asalam Aykum humaanisha rehema na amani iwe juu yenu,ukiitikia wa alaykum salama, kipifu na wewe pia.
Sasa hapa hakuna udini
ni muhimu watu kupunguza jazba katika mambo madogo madogo kama haya kwani hayajengi na kikubwa zaidi Shekifu ni Mkristo sasa kumzomea kwa salamu tu nadhani hajatendewa haki;
Wadau mjadala huu ni funzo kuwa sasa Taifa liendapo sio salama sisi tuwe watoa elimu sahihi kwani chuki za kidini zimeanza kututafuna.
Mussa
ArushaOn Thu, Jan 3, 2013 at 1:07 PM, magreth Mulokozi <m.mulokozi@gmail.com> wrote:
Duu anatafuta kura za 2015 sasa , duu pole sana Nd Shekifu2013/1/3 matinyi@hotmail.com <matinyi@hotmail.com>
....alikariri.....siyo alikalili.
T-Mobile. America's First Nationwide 4G Network
----- Reply message -----
From: "adeladius makwega" <makwadeladius@googlemail.com>
To: "mabadilikotanzania" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>, "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Subject: [wanabidii] Mbunge wa Lushoto azomewa Kanisani
Date: Thu, Jan 3, 2013 4:46 am
Shekifu aunza mwaka mpya Vibaya
Mbunge wa Lushoto Hendry Shekifu ameuunza mwaka wa 2013 vibaya
baada ya kuzomewa Kanisani na waamini katika sherehe za mwaka
mpya baada ya kupewa nafasi ya kuwasalimu washirika wa Kanisa Kuu la
KKKT Lushoto Tanga.
Ibada hiyo ya kuukaribisha mwaka mpya ilianza kwa waumini kupokea
mahubiri ya mwaka mpya yaliyohubiriwa na Mchungaji Walelaza na
baadae kufuatiwa na ibada ya ubatizo ambapo watoto wawili kutoka
familia mbili walibatizwa.
Mara baada ya ubatizo huo ibada ilifuatiwa na utoaji wa Sadaka
huku mbunge huyo wa Lushoto akionekana kushiriki kikamlifu
katika ibada hiyo .
Akiwa amevalia suti ya rangi nyeusi yenye mistari midogo
midogo miyeupe Mbunge Shekifu ambaye aliwahi kushika nyadhifa
mbalimbali zikiwamo ukuu wa mkoa alipewa nafasi ya kusimama mbele ya
waamini mithili ya kasisi.
Nafasi hiyo ilitolewa wakati wa Matangazo huku mchungaji
akiwaomba waumini hao kumsikiliza Mbunge wao ili awasalimu. Basi
Mbunge Shekifu alisimama huku akiweka vizuri koti kwa kujifunga
vifungo vya koti hili ambalo lilionekana kuutosha mwili wake
mkubwa uliojengeka vizuri.
Alikisogelea kipaza sauti mara alianza kuongea kwa
kujiamini."Aslaam Aleikumuuu…" Duu utangulizi huo uliharibu hali ya
hewa ya kanisa hilo wauumini kuanza kuzomea na kuguna kutokana
salaam hiyo iliyotolewa mwanzoni katika sehemu isiyo sahihi.
Hali hiyo iliwafanya waumini hao kuibua munkali huo kutokana na
kitendo cha mbunge huyo pengine kukalili namna ya kusalimia watu
katika majukwaa ya kisiasa bila ya kujua kuwa sasa madhari
aliyokuwa nayo ilikuwa ya salaam moja tu kama sikosei ni Bwana
Yesu asifiwe au Tumsifu Yesu Kristu.
Hekima ilitumika pengine huku yule aliyempa nafasi ya kuwasalimu
wauumini wake akijilaumu kuitoa nafasi hiyo iliyotia shubiri
kanisani hapo na kuibua zomeazomea hiyo ambalo sio jambo la
kawaida kwa waumini kufanya hivyo.
Mchungaji Walelaze ilibidi kuinuka na kusema waziwazi kuwa Ndugu
Shekifu umekosea sana kwanza ulitakiwa kujitambua kuwa wewe
japokuwa ni Kiongozi pia wewe ni mkiristu lolote utakalo fanya
popote pale tambua unamajukumu mawili kwanza ukiristu wako
na pili kuwa kiongozi. Hapa ni kanisani ulitakiwa kuwasalimia
waashirika kwa salaam yao siyo salaam hiyo uliyoitoa hapa.
Basi mchungaji huyo alimaliza mtafaruku huo huku mbunge huyo wa
Lushoto akishuka katika mimbari ya kanisa hilo kwa fedhea na
kurejea katika kiti chake ambacho kilikuwa jirani na mlango wa
kutoka nje ya kanisa.
Mara baada ua ibada hiyo ya mwaka mpaya mbunge huyo alionekana
kuwa mtu wa mwisho kuondoka kanisani mara baada ya washirika wote
kuondoka lakini washirika hao walisema kuwa mbunge huyo
amekalili kusalimia kwa salaam hizo ndiyo maana alipitiwa.
"Mimi nilitaka Mbunge aombe msamaha kwa alilolifanya sio
kuondoka kimya kimya tu hawa wanasiasa hawana adabu kabisa wanakuja
na mbwembwe alafu wanapata aibu."alisema mama mmoja
aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Mama Sarah.
Mshirika mwingine alimuunga mkono mchungaji Waleleza kwa kumkumbusha
Mbunge huyo kuwa makini sana akiwa kanisani na kuheshimu salaam
za ibada za makanisa sio kuja na salaam za nyumba zingine
za ibada.
"Pengine inawezekana Mbunge huyu asipewe tena nafasi ya
kuwasalimu waumini kanisani kutokana na kosa hili," aliserma mzee
mmoja wa makamo ambaye alidai kuwa hilo ni kosa baya.
Mwishoni alionekana Mbunge Shekifu akiingia ndani ya gari yake
nyeupe yenye Bendera ya CCM ikipeperuka mkono wa kushoto. Ndani ya
gari hiyo kukiwa na akina mama watatu ambao walionekana wakifunga
milango na dereva wa gari hilo akiondoa gari katika eneo la
kanisa hilo.
Wasalaam Adeladius Makwega
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:
Post a Comment