Monday 21 January 2013

Re: [wanabidii] MARAIS WA ZAMANI WA ZANZIBAR WATAKA MUUNGANO WA MKATABA!

Matinyi,
Walioungana hawautaki muungano, wewe ambaye hujui hata chanzo cha muungano huo unautetea.why?!watu wanafunga ndoa wawili wakiachana ni wao wenyewe wameshindwana.wewe wawashiwa nini?7

On Monday, January 21, 2013, Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com> wrote:
> Issa,
> Ndiyo maana watu wengi wa Bara wanasema kwamba Wazanzibari ni walalamishi. Hebu angalie ulichokisema - unaashiria kwamba Zanzibar imefanywa jimbo wakati ina rais wake, makamu wawili, katiba yake, wimbo wake, bendera yake, nembo yake, mamlaka yake, mahakama yake, bunge lake, na sasa eti na eneo lake la mipaka, na inawakilishwa kwenye kila kitu ndani ya Muungano. Nadhani umeona hoja ya watu wengi wa Bara ambao wameshachoka na haya maneno. Mimi binafsi sijachoka na niko radhi hata tuvutane hata kwa miaka 1,000 lakini tusifuate uongo na unafiki. Hapa Marekani kati ya haya majimbo 50 hakuna hata moja lenye vitu vyote hivi kwa mtindo wa Zanzibar na hawalalamiki kitu. Muungano ni kuungana, siyo kubaki na kila kitu cha kwako.
> Matinyi.
>  
> ________________________________
> Date: Mon, 21 Jan 2013 11:11:16 -0800
> From: saidissa100@yahoo.com
> Subject: Re: [wanabidii] Re: MARAIS WA ZAMANI WA ZANZIBAR WATAKA MUUNGANO WA MKATABA!
> To: matinyi@hotmail.com; wanabidii@googlegroups.com
>
> Kaka Matinyi,
> Mengi yanasemwa pande zote mbili, lakini la muhimu ni hali ipo vipi hivi sasa baina ya washirika hawa wawili?
> Kweli ni Muungano wa nchi mbili au wa nchi moja na jimbo fulani?
> ...bin Issa.
> ________________________________
> From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
> To: saidissa100@yahoo.com
> Sent: Monday, January 21, 2013 11:05:39 AM
> Subject: RE: [wanabidii] Re: MARAIS WA ZAMANI WA ZANZIBAR WATAKA MUUNGANO WA MKATABA!
>
> Issa,
> Ina maana wewe humjui "Hapa pangu"? Humjui siyo? Karafuu iko wapi siku hizi? Wale waliotaka kuufutilia mbali utalii washatulia? 
> Halafu siamini kwamba eti wewe Issa hujui kuwa wimbo mkubwa visiwani hivi sasa ni kwamba Waarabu wataleta misaada kuanzia na Oman, halafu Arab League, OIC, na mataifa mengine, na hoja ni kwamba eti Zanzibar ni ndogo, Wazanzibari ni wachache, kwa hiyo misaada itasaidia zaidi. Huo wimbo mpaka Maalim Seif anauimba, bila hata haya, akija huku na kwingineko. 
> Lakini pia hili la "sisi" na "ninyi" halifai kabisa. Ni ubaguzi tu. Muungano una malalamiko yake na kama tungekuwa viongozi makini yangetatuliwa, lakini ubinafsi wa viongozi wa Tanzania, siyo Tanzania Bara, ndiyo tatizo. Ninaposema ubinafsi viongozi nazungumzia TANZANIA, yaani Bara na Visiwani.
> Matinyi.
>
>  
> ________________________________
> Date: Mon, 21 Jan 2013 10:52:22 -0800
> From: saidissa100@yahoo.com
> Subject: Re: [wanabidii] Re: MARAIS WA ZAMANI WA ZANZIBAR WATAKA MUUNGANO WA MKATABA!
> To: wanabidii@googlegroups.com; matinyi@hotmail.com
>
> Kaka Matinyi,
> Sasa kaka Matinyi kama kwanza ilikuwa Seif, halafu Karume na sasa Salmin na kesho Shein, hivyo bado hujafahamu tu Wazanzibari wanasema nini?
> Kama hukubali kuwa matatizo yaliyopo ni kwasababu ya Muungano basi kwanini hatuwezi kuyatatua?
>>Shida yetu kubwa ni kwamba tuna viongozi wezi, wabinafsi na sisi wananchi hatufanyi kazi.
> Hili ndilo jambo moja linalotufanya tuukimbie huu Muungano. Wenzetu mmezidi wizi na sio wizi tu lakini hata mkiwapata hao wezi hamfanyi kitu kwasababu ndio nyinyi wenyewe wezi - samahanini kwa lugha jamani, kwani sisemi kuwa nyote ni wezi - ni wakubwa wenu tu.
> Mzee Vijisenti kakubali kuwa anapesa nje, je, aliulizwa chochote? Yule Mhindi wa Radar yupo Switzerland, je, tumechukuwa hatua zozote za kumrejesha? Sitaki hapa kuzungumzia juu ya hizo pesa zilizofichwa huko huko Switzerland na ambazo serikali haitaki kuzidai kama Balozi wa Switzerland alivyoeleza. Mambo haya sisi Wazanzibari tunahisi yanasaidia kuturejesha nyuma, japokuwa nasi sio Mitume!
> <
>
> --
> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
> International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>  
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>  
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>  
>  
>

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment