Tuesday 29 January 2013

Re: [wanabidii] Kwa nini serikali tatu?

Nafikiri sababu ya msingi wanayosimamia CHADEMA ni pale Mbowe
aliponukuliwa akisema "tayari wakitoa uhuru wa Zanzibar kuwa na Rais,
bendera na wimbo wao wa taifa"
Ukiangalia kwa makini uwepo wa serikali tatu unaletwa zaidi na kitendo
cha wazanzibar kutaka kuwa na nchi yao inayojitegemea. Kama hilo
lisingekuwepo sidhani kama tungekuwa na mjadala unaohusu muungano.
Wote tungependa tuwe na serikali moja ya kitaifa na hivyo kila kitu
kuwa sawa kati ya bara na visiwani.

Mbowe na wafuasi wa CHADEMA wako sahihi kusema ziwepo serikali tatu (
Tanganyika au Tanzania bara, Zanzibar au Tanzania Visiwani na Serikali
ya Muungano). Kama Zanzibar wanapenda kutambuliwa kama wazanzibar
chini ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iweje Tanganyika isiendelee
kutambuliwa kama Tanganyika na watanganyika wake? Nafikiri jibu liko
wazi, ni ama kuwa na serikali moja au tatu hiki kiini macho cha kuwa
na serikali mbili ambapo tuna serikali ya muungano na serikali ya
Zanzibar kitaendelea mpaka lini? Je vitambulisho vya Tanzania vitakuwa
vya aina ngapi?

2013/1/29 Ntunaguzi Ntiyakunze <ntunaguzin96@gmail.com>:
> Wanabidii,
>
> Nanukuu kauli moja ya mwenyekiti wa CHADEMA katika kikao cha Kamati Kuu (CC)
> juzi ambapo agenda moja kubwa ilikuwa ni kupitisha mpango mkakati wa mwaka
> 2013 ili kushinda chaguzi zote kuanzia serikali za vitongoji, vijiji na
> mitaa mwaka 2014 na Uchaguzi Mkuu 2015.
>
>
> Katika suala zima la Muungano, Mbowe alisema uwepo wa serikali tatu
> hauepukiki kwa kuwa tayari Tanzania Visiwani wameshakuwa na serikali yao
> hivyo ni jukumu la Watanzania Bara kupata serikali ya Tanganyika na kisha
> kuwepo na serikali ndogo ya Muungano. Alisema serikali tatu inawezekana
> ikiwa viongozi wataacha unafiki wa kusema muungano utavunjika huku tayari
> wakitoa uhuru wa Zanzibar kuwa na Rais, bendera na wimbo wao ya taifa.
> Tunawaunga mkono wenzetu Wazanzibar katika kupigania uhuru kamili na kwa
> sasa sisi ndio tunaoonekana wa ajabu kushindwa kuuliza serikali ya
> Tanganyika," alisema.
> Swali;
> Je kuna sababu za msingi ambazo CHADEMA wanazo mpaka kufikia hatua ya
> kuzitaka serikali tatu tofauti na ilivyo hivi sasa?
>
> --
> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
> International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment