Wednesday 16 January 2013

Re: [wanabidii] Juliana Shonza: Mimi bado ni Makamu Mwenyekiti BAVICHA *

Juliana Shonza anahitaji kushauriwa kuwa haya anayoyafanya kisiasa yanaweza hata kumharibia kwenye level ya familia......

Ngoja tuendelee kufuatilia!

On Jan 17, 2013 8:10 AM, "Ismael Kimirei" <kiakimirei@gmail.com> wrote:
unfortunately sipati printed copy. Natumia online version.


On Thursday, January 17, 2013 8:12:55 AM, nevilletz@gmail.com wrote:
Mwananchi la jana kasome uone iko ukurasa wa ngapi!
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania
------------------------------------------------------------------------
*From: * Ismael Kimirei <kiakimirei@gmail.com>
*Sender: * wanabidii@googlegroups.com
*Date: *Thu, 17 Jan 2013 08:01:28 +0300
*To: *<wanabidii@googlegroups.com>
*ReplyTo: * wanabidii@googlegroups.com
*Subject: *Re: [wanabidii] Juliana Shonza: Mimi bado ni Makamu
Mwenyekiti BAVICHA *

Meena,
Uliyoyasema juu ya Dr Slaa yanapendeza. Yanatia moyo. Ila cha
kushangaza - huyo huyo Shonza ndo mmempa ukurasa wa mbele kwenye
gazeti lenu kama alivyoomba wakati wa mkutano na wanahabari - kuwa
mkaitangaze vizuri ile habari. Kwangu mimi ile kitu ameandika
haikustahili hata kuwekwa ukurasa wa pili au wa tatu - ningeiweka
katikati huko au karibu na mwisho.
Kim
On 1/17/2013 7:36 AM, nevilletz@gmail.com wrote:
Mtu alikuwa mwanachama siku zote, leo kawekwa pembeni ndo anaamua
kusema kuhusu uozo, hapo the motive behind ni kutimuliwa kwake. Bado
ni binti mdogo, atulie atapata nafasi tena siku zijazo. Kwenda
hadharani na kuwasema viongozi wake wakuu wa Chama ni utovu wa nidhamu.

James Ole Millya alipotoka CCM kwenda Chadema hakuwahi kuwatukana
waliokuwa wakuu wake wa chama JK wala Mukama. Alieleza udhaifu wao na
udhaifu wa chama chake.

Dk Slaa ni mtu anayeaminika siyo ndani ya Chadema tu hata nje ya
chama hicho. Hana record yoyote ya ubadhirifu wa fedha tangu
alipokuwa TEC, Mbunge wala KM Chadema.

Akiwa Mwenyekiti wa LAAC alifanya kazi kubwa na hakuwahi kulala wala
kula kwa fedha za Halmashuri walikokwenda kukagua miradi, si mtoa
fedha kwa waandishi wa habari kama ilivyo kwa wanasiasa wengine,
haombi kuandikwa na vyombo vya habari bali vyombo hivyo humtafuta
kutokana na umuhimu wake.

Aliyoyafanya akiwa TEC kuanzisha Caritas Tanzania, miradi ya maji
kule Karatu na hata fedha alizoingiza pale CCBRT ni ushahid toka
kwamba siyo mbadhirifu wala mbinafsi. Mtu wa aina hii siyo rahisi
kuharibu credibility yake!

Kwa kauli za Shonza dhidi ya Dk Slaa, anajianika kwamba yeye ni mtu
wa aina gani!
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania
------------------------------------------------------------------------
*From: * Herment Mrema <hmrema11@hotmail.com>
*Sender: * wanabidii@googlegroups.com
*Date: *Wed, 16 Jan 2013 20:37:32 +0000
*To: *<wanabidii@googlegroups.com>
*ReplyTo: * wanabidii@googlegroups.com
*Subject: *RE: [wanabidii] Juliana Shonza: Mimi bado ni Makamu
Mwenyekiti BAVICHA *

Ndugu Wanabidii,

Haya makubwa, lakini tukubali au tusikubali kama haya hayapo siasa
hakuna. Changamoto ni sisi kuchambua ni zipi mbivu na zipi mbichi.

Cheers

Herment

------------------------------------------------------------------------
Date: Wed, 16 Jan 2013 14:05:54 -0600
Subject: Re: [wanabidii] Juliana Shonza: Mimi bado ni Makamu
Mwenyekiti BAVICHA *
From: ngonzy@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com

Sijui chama hakina taratibu za kushugulikia haya mambo? Yanakera
kweli kuyasoma

2013/1/16 Ireneus Kakuru Mushongi <ireneuskakurumushongi@gmail.com
<mailto:ireneuskakurumushongi@gmail.com>>

    Bongo politics...!
    Ngoma ya watoto haikeshi... Hivi hamna jinsi yoyote ya kumaliza
    matatizo haya?
    Mnadhani mnatengeza picha gani kwa mashabiki na wanachama wenu?
    Nadhani mwenye timamu hatakuja kuanika mambo haya (yenu)
    hadharani tena.
    Kuna kubwa gani la kugombania hapa na mnamwakilisha nani?
    Kwa hali hii tutarajie ngumi kwenye kikao chochote
    kitakachokutanisha makundi haya..
    Na huo ndio utakuwa mwisho wa Chdm. Na ushindi mwororo upande wa
    pili..
    Tafakari..ongozweni na busara, si jaziba matusi na maslahi binafsi..
    SIjamwona aliyetumia busara hadi hapo na zaidi tutarajie makubwa
    zaidi
    UONGOZI UMESHINDWA KUMALIZA HAYA YA WATOTO HAWA NDANI YA CHADEMA
    AU NI KWELI NAO NI SEHEMU YA TATIZO?
    Siko kwa ajili ya kukosoa au kumfinger point mtu..ila nahisi hii
    ni trela na kuna mengi nyuma ya pazia na isipotumika busara, ni
    hatari tupu. Safari ya 2015 itabaki ndoto
    Kama yale ya Mnara wa Babeli!
    Ireneus
    On Jan 16, 2013 11:45 AM, "Anthony Masare"
    <anthony_masare@yahoo.com <mailto:anthony_masare@yahoo.com>> wrote:

        Boxbe <https://www.boxbe.com/overview> This message is
        eligible for Automatic Cleanup! (anthony_masare@yahoo.com
        <mailto:anthony_masare@yahoo.com>) Add cleanup rule
        <https://www.boxbe.com/popup?url=https://www.boxbe.com/cleanup?token%3D0W1YPooSTHaFxyy3tB519K%252BHCpV%252FigMONxLK5PYYn7guXek2LMZ7ER63%252BE5x8Kh%252FCcf6XGgdoJ9IVKmoP2YF5%252BeeR2zLRWsazm0WJ6r7rQsiXVq%252FwMzZo4zdSfX6ZKtuCpRegHBqj%252BK04Bl%252B9kiunA%253D%253D%26key%3DrF%252Fk1CEdZEzePFMmTvh4OamPeDznFfConO%252B3YtzlHcw%253D&tc=13356526385_63802074>
        | More info
        <http://blog.boxbe.com/general/boxbe-automatic-cleanup?tc=13356526385_63802074>


        huyu dada shonza ni mnafiki mkubwa haya yote aliyosema hapa
        mbona hakusema akiwa ndani ya chama?amefukuzwa ameaanza
        kutapatapa tumpuuze mtu kama huyu hana nia njema na chama
        naamini sasa kweli huyu mtu ni kibaraka (mamuluki)

        --- On *Tue, 1/15/13, Juma Mzuri /<jumamzuri@gmail.com
        <mailto:jumamzuri@gmail.com>>/* wrote:


            From: Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com
            <mailto:jumamzuri@gmail.com>>
            Subject: [wanabidii] Juliana Shonza: Mimi bado ni Makamu
            Mwenyekiti BAVICHA
            To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com
            <mailto:wanabidii@googlegroups.com>>
            Date: Tuesday, January 15, 2013, 10:05 AM

            TAMKO LA KUTOA UFAFANUZI DHIDI YA TAARIFA BATILI
            ZILIZOZALISHWA NA
            MWENYEKITI WA BAVICHA
            BWANA: JOHN HECHE [WEGESA CHARLES SUGUTA] KUHUSU KUVULIWA
            UANACHAMA WA
            BAVICHA, NA KUSHABIKIWA NA MH. FREEMAN MBOWE, MWENYEKITI
            CHADEMA TAIFA


            Nawashukuru sana wanahabari, kwakuchukua muda wenu kuja
            kunisikiliza.
            Natambua mnakiu ya kusikiliza mambo mengiya kuwaeleza
            kutokana na
            taarifa zilizosambaa kuhusu hiki
            kichefuchefukinachosambazwa kwa
            makusudi na virusi vichache vilivyojivika ngozi yaukombozi.

            Nimepokea simu nyingi kutoka kwawatu mbalimbali kutoka
            ndani na nje ya
            Tanzania wakitaka kupata ufafanuzi baadaya kupata taarifa
            kupitia
            vyombo vya habari kuwa nimevuliwa uanachama naU-Makamu
            Mwenyekiti wa
            BAVICHA Taifa.Kama mlivyo ninyi, nami pianimeyasikia hayo
            kupitia
            vyombo vya habari, maana sijapata barua au
            mawasilianoyoyote toka kwa
            Mwenyekiti wa BAVICHA, Ndugu Wegesa Suguta (John
            Heche)aliyetoa tamko
            hilo.Kwanza kabisa naomba kuweka wazikwamba sijawahi pewa
            shutuma
            zozote au mashitaka yoyote yale yanayohusiana nahicho
            alichokiongea.

            Niliamua kupuuzia kwa sababunamjua Heche ni mlopokaji,
            kiongozi
            asiyejua wajibu wake, anayetumikiawasiomchagua, mtu asiye
            na malengo
            na mtegemezi wa siasa ili kuendesha maishayake na ya
            familia yake. Pia
            nilimpuuza kwa sababu najuasio Mwenyekiti aliyechaguliwa
            kidemokrasia,
            aliwekwa kwa matakwa ya wakubwazake ambao wanamtumia kwa
            malengo
            yaliyokusudiwa, ikumbukwe kuwa vijana watatu,Habibu
            Mchange, Mtela
            Mwampambwa na Grayson Nyakarungu walienguliwa
            kimizengweili Heche
            ashinde, hivyo kwetu sisi yeye ni sawa na Mwenyekiti wa
            kuteuliwa.Hivyo sikumjibu mtu asiyekuwa na sifa sawa na
            zangu katika
            harakati za kusakademokrasia ya kweli.

            Lakini kitendo cha Mwenyekitiwangu, Mh. Freeman Mbowe
            kujitokeza
            kupitia gazeti mojawapo na kudai madaiyangu ni ya kitoto,

            kwanza kimenifedhehesha, ni dharau kwa vijana
            walionionanina sifa na
            ukomavu na kunipa kura nyingi ili niwe Makamu Mwenyekiti
            waBAVICHA
            Taifa.

            Pili ni kama anahalalisha kikaobatili, kilichokiuka
            kanuni na katiba
            ya CHADEMA ili kuhalalisha matakwa yaoyenye lengo la kuminya
            demokrasia na uhuru wa kujieleza ndani ya chama.

            Tatu anahalalisha hoja za vijana,ambazo ndio uhalisia
            kuwa Heche
            hakuwa na sifa, na uwezo, hivyo alibebwa na Mh.Mbowe ili
            akae pale kwa
            malengo yake.Ndio maana nilisema ukionakifaranga
            kimepanda juu ya figa
            ujue mama yake yuko chini, hivyo mama yakekifaranga
            kajitokeza
            kuhalalisha kifaranga chake kupanda juu ya figa.

            MADAI YAALIYODAI MH. MBOWE KUWA NI YA KITOTONiseme wazi
            kwamba
            nimesikitishwamno na madai aliyoyatoa Mwenyekiti wangu wa
            CHADEMA Mh
            Freeman Mbowe kupitiagazeti la Mtanzamia la tarehe
            12/01/2013 kwamba
            madai yangu ni ya kitoto .

            Kwanza niweke wazi kabisa kwambanamuheshimu sana Kiongozi
            wangu huyu
            mkuu ambaye ndiye alipaswa kuwa mstari wa mbele katika
            kuhakikisha
            kwambahaligawi baraza la Vijana na chama kwa ujumla,
            ahakikishe kuna
            utawala borandani ya chama, na utendaji haki, lakini cha
            kushangaza
            ameibuka kumtetea Hechekwa hoja za mwegemeo wa upande
            mmojabila
            kuangalia maelezo ya upande wa pili.

            Niweke wazi kabisa kwamba kaulialiyoitoa dhidi yangu ni
            yakiushabiki
            maana kama ni madai yangu kuhusu namna
            ninavyohujumiwakupitia kwa
            Katibu Mkuu yeye anayo nakala ya malalamiko [ushahidi upo],
            lakinihakuna hatua ambayo ameichukua.

            Namshangaa Mwenyekiti kudai madaiyangu ni ya kitoto sasa
            sijui ni
            madaiyapi anayazungumzia ? madai ya kitoto ni yapi? na
            madai ya
            kikubwa ni yapi ? naje madai ya kitoto ni haya mimi
            kuhoji kwanini
            hatuweki akiba kwenye akauntikwa ajili ya uchaguzi 2015 kama
            tulivyokubaliana kwenye baraza kuu mara baadaya uchaguzi wa
            2010.Naombaniwajulishe wanachadema kuwa, nimejitahidi
            sana kushauri
            juu ya

            1; Uanzishwaji wa chuo chamafunzo ya uongozi kwa makada
            wa CHADEMA ,
            badala yake ni matumizi mabaya yafedha za ufadhili wa
            wadau tofauti na
            hasa mfadhili mkuu ndugu SABODO. Hiiingesaidia pia kulea
            ki-mfumo wa
            maadili ya uongozi kwa vijana wa umoja wawanafunzi wa
            CHADEMA wa vyuo
            vikuu yani " CHASO" ambapo mimi ni mwasisi wamkakati huu
            nchini.

            2; Chama kwa ujumla kutokuwa na jengo letu na hasa makao
            makuu yetu.
            Niaibu kwa chama kikubwa kama CHADEMA kuwa na ofisi
            tulizopanga na
            kulipa mamilioni ya fedha za ruzuku na misaada kwa manufaa ya
            Mwenyekiti Freeman Mbowena Mkurugenzi wa fedha wanaomjua
            mmiliki wa
            jengo la makao makuu. Kimsingi mimi natambua chama kina
            uwezo mkubwa
            wa kuwa na majengo yetu.

            3; Kupunguza mshahara wa katibumkuu Ndugu Dk. Slaa ambao
            ni zaidi ya
            milioni saba kwa mwezi na marupurupu kibao ili pesa hizo
            na mamilioni
            zielekezwe kujenga chama mikoani kama kweli tunataka2015
            tuingie
            Ikulu.

            4; Kuhakikisha pesa zilizochangishwa kwenye M4C
            zinatumika ipasavyo na
            si kama zitumikavyo kipindihiki ambapo ni kama tumelewa
            wingi wa watu
            kwenye mikutano ya hadhara.

            5; Kitendo cha Mwenyekiti wa chama kufumbia macho hatua
            ya ndugu Slaa
            (katibu mkuu) kujikopesha pesa ya ruzuku ya watanzania
            zaidi ya
            shilingi milioni mia na arobaini.

            6; Hatua ya mwenyekiti ndugu Heche kulipwa mshahara na
            marupurupu hali
            kanuni za chama haziruhusu huku Mbowe akifumbia macho
            wakati viongozi
            wa mikoa na wilaya hawapewi pesa na vifaa vya uenezi.

            7; Kitendo cha mchumba wa Dk.Slaa, Josephine Mushumbusi
            kuzunguka
            mikoani na kulazimisha kupokelewa kama mke wa mfalme na
            kuendesha
            vikao vya ndani na mikutano ya hadhara yenye kulenga
            kuwajenga
            wagombea ubunge anaowataka yeye na katibu mkuu kwa mwaka
            2015.

            Ndugu wanahabari, je hizi ndo hojaza kitoto anazodai Mh.
            Mbowe? Hivyo
            basi namtaka Mh. Mbowe sasa asikimbiliekujibu hoja
            kiushabiki.
            Ajitahidi kuwa na fikra na Busara ili kukisaidia chama
            kuvuka kwenye
            daraja la sasa la pepo kufukuzana. Atambue Baraka
            anazozitoa wanachama
            wafukuzwe hovyo na kunyanyaswa ni hatari kwa kuwa
            anaandaa kundi kubwa
            nje ambalo litageuka mwiba siku za usoni.

            UHALISIA ULIOPO:

            Ndugu waandishi wa habari,
            Naomba kuweka wazi kwamba mimi Juliana Shonza ni Makamu
            Mwenyekiti
            halali wa baraza la vijana (BAVICHA). Taarifa zozote zile
            mlizozisikia
            kuhusu kuvuliwa kwangu uanachama, naomba kwa nguvu moja
            kupitia
            taaluma yenu muwaambie watanzania kwamba wazipuuze. Ni
            taarifa
            zilizotolewa na kikundi cha kihuni kilicholenga kutimiza
            matakwa ya
            wakubwa wao. Kikundi hicho hakina mamlaka ya kikatiba
            yoyote yale ya
            kunivua uongozi huunilio nao.

            Kuthibitisha hilo kuwa ni kikundimufilisi, hadi
            ninapoandika waraka
            huu kwenu sijapewa barua yoyote ile inayonitaarifu kuwa
            nimevuliwa
            uongozi wangu. Hii ni wazi wanatambua kuwa wanachemka,
            wanatengeneza
            makundi kwa maslahi wanayoyaona yanawafaa.

            Sikuchaguliwa ili niwe chombo cha kuwatumikia watu, na
            badala yake
            nilichaguliwa ili niwatumikie vijana waCHADEMA na
            watanzania kwa
            ujumla, na pale nilipoona kuna ukiukwaji na kuhoji ndio
            chanzo cha
            mizengwe na matamko ya Ndugu Wegesa (John Heche).

            Nimekuwa nikiwasumbua viongozi wenzangu kuhusu
            kutengeneza kadi za
            BAVICHA na kusajili wanachama katika mfumo mzuri
            (database) ili tuwe
            na kumbukumbu ya wanachama wetu lakini yote
            yameshindikana kwasababu
            amekuwa akiendeshwa na mfumo dume kandamizi kwa mwanamke,
            mara nyingi
            nimemshauri kwa ajili ya maendeleo ya Baraza na nimekuwa
            nakwamishwa
            na Mwenyekiti na Katibu na hata leo sisi wote ni
            wanachama kwa
            kufikirika (imagination), kwa kuwa bado hatuna kadi za
            uanachama kwa
            vijana wa BAVICHA zaidi ya kutambulika na katiba ya chama.

            KUKIUKWA KWA KATIBA

            Ndugu wanahabari, ni wazi kuwakatiba pamoja na mwongozo
            wa baraza letu
            la vijana bavicha ulikiukwa katikakikao walichokiita
            kamati tendaji
            iliyokaa tarehe 05/01/2012 ambayo iliongozwa na Bwana
            Wegesa Suguta
            (John Heche) kama Mwenyekiti, hali inayonilazimu kusema
            wazi, bila
            kumung'unya maneno kwamba maamuzi yaliyotolewa na kikao hicho
            yalikwishapangwa na viongozi wa kitaifa hayakuwa halali.
            Nasisitiza
            kwamba ni ukweli ulio wazi kwamba agenda na maazimio ya
            kikao hicho
            yalikwisha amuliwa hata kabla ya kikao hicho kwasababu
            kubwa mbili:

            1; Taarifa za kufukuzwa kwetuzilikwisha anza kusikika
            kwenye mitandao
            ya kijamii kama vile jamii forum nafacebook mwezi mmoja
            kabla ya kikao
            cha kamati tendaji batili.

            2; Pili ushahidi wa kimazingirakwa maana ya ukiukwaji
            mkubwa wa
            kikatiba na mwongozo wa Baraza letu la Vijana uliofanyika
            siku ya
            kikao.

            Ndugu wanahabari,
            Ikumbukwe kuwa pamoja na uwepo wa taarifa za kikao mwezi
            mmoja kabla
            binafsi nililetewa taarifa hizo siku mbili kabla ya
            kikao, tena kwa
            njia ya ujumbe mfupi wa maandishi {sms} na baadae
            kupigiwa simu na
            Katibu wa Baraza Bwana Munishi ikinitaka kuhudhuria kikao
            hicho
            kutokana na kuwa nje ya Dar-es –salaam kwa mambo ya
            kifamilia zaidi
            niliwataarifu viongozi wenzangu kwa utaratibu maalumu wa
            mawasiliano
            ya kiuongozi kwa maana ya kuwatumia barua ya udhuru wa
            kutohudhuria
            kikao.

            Lakini cha kushangaza na kustaajabisha kwa viongozi
            wenzangu hawa
            ambao kwa namna moja ama nyingine napata ugumu wa kuelewa
            kama kweli
            wana sifa za kuitwa viongozi tena wa idara nyeti sana
            katika ustawi wa
            chama chetu, kwa makusudi kabisa ama kwa kutumwa kufanya
            hivyo ama kwa
            utashi wao mdogo wa kiupembuzi yakinifu waliamua kuvunja
            na kukiuka
            katiba ya chama na kujipa vyeo vya kiunyampara kwa kuamua
            kuchukua
            maamuzi ya kutuvua uanachama wa kufikirika wa baraza mimi
            na vijana
            wenzangu Ndugu Mwampamba na Mchange ambao nao hawakupewa
            nafasi ya
            kusikilizwa, ambao moja kwa moja tunapoteza sifa yakuwa
            wanachama wa
            CHADEMA.

            Ndugu wanahabari,
            Naomba sasanijikite katika katiba ya chama changu na
            mwongozo wa
            baraza la vijana sura ya sita kipengele cha 6.5 ambacho
            kinasema
            taratibu zifuatazo lazima zifuatwe katika kuchukua hatua
            za kinidhamu.
            6.5.2 kwa mujibu wa ibara 5.4.3 na .4.4 ya katiba, mwanachama
            yeyotehatachukuliwa hatua za kinidhamu ama kuonywa ama
            kuachishwa ama
            kufukuzwa uanachama bila kwanza

            {a} kujulishwa makosa yake kwamaandishi na kutakiwa kutoa
            majibu
            katika muda usiopungua wiki mbili.
            [b] kupewa nafasi yakujiteteakatika kikao kinachohusika.
            {c} Mwanachama atajulishwa kwamaandishi uamuzi wa kikao
            mnamo wiki
            mbili baada ya kusikilizwa.

            Ndugu waandishi wa habari,Nisemewazi kwamba hakuna kifungu
            kilichofatwa kati ya hivyo niliyoviainisha hapo
            juu,hakuna barua
            yeyote niliyojulishwa ya hayo waliyoyaita mashitaka yangu
            zaidi ya
            kuyasoma na kuyasikia kwenye vyombo vya habari baada ya
            wao na kikao
            chaoharamu kuchukua maamuzi yakunivua uanachama wa Bavicha .

            Sikupewa nafasi yakujitetea maanasikuwepo kwenye kikao,
            barua ya
            udhuru wakutohudhuria walikuwa nayo. Na vilevile mpaka
            leo hii
            sijajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao hicho batili
            badaa yake
            viongozi wenzangu hawa wameamua kuujulisha umma wa
            Watanzania na
            wanachadema kwa ujumla pasipo kunijulisha mimi kwanza.
            Ukiangalia pia
            kifungu cha 6.5.6 cha katiba kinasema KIONGOZI YEYOTE
            hatachukuliwa
            hatua za kinidhamu bila kwanza kupewa mashitaka kwa
            maandishi na
            mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu kwa maandishi.

            Sasa basi namtaka Bwana Wegesa Suguta awaeleze umma wa
            watanzania kama
            alivyokurupuka kuwaeleza kwamba Shonza amevuliwa
            uanachama wa Chadema
            ni wapi na lini yeye kama Mwenyekiti nilipewa barua ya hayo
            wanayoyaita mashitaka, na ni lini niliwapa majibu ya
            mashitaka hayo.

            UHALALI WAKIKAO CHA KAMATI TENDAJI

            Ndugu wanahabari,
            Ikumbukwe kwambakikao cha juu kuliko vyote kwenye ngazi
            ya chama
            husika ni Mkutano Mkuu ambao ndio ulioniweka madarakani
            kutokana
            nakuwa na imani na mimi na kikatiba ndiohaswa ulipaswa
            kuniandikia
            mashitaka, kunijadili, kunihoji na kutoa maazimio ambayo
            yangepelekwa
            kamati kuu ambao kimsingi ndiyo yenye mamlaka ya mwisho
            yakumvua mtu
            yeyote uanachama wake baada ya kujiridhisha na taarifa na
            uchunguzi
            kutoka kwenye kikao husika kilichomwandikia mwanachama
            mashitaka na
            kumuhoji.

            Ndugu wanahabari ifahamike wazikwamba kikatiba kuna ngazi
            mbili tu
            zinazoweza kumvua mtu uanachama wake ambazoni ngazi ya
            tawi na ngazi
            ya kamati kuu.

            Hivyo basi namtaka sasa Bwana Wegesa Suguta auambie umma
            wa watanzania
            kwamba ni lini kamati tendaji ya vijanailigeuka ama
            kukaimishwa
            madaraka ya ngazi ya tawi, ngazi ya mkutano mkuu
            amakamati kuu yakuwa
            na uwezo wakumvua kiongozi uanachama wake?

            Ndugu waandishi wa habari,
            Wajumbe wa kamati tendaji kikatiba ni makatibu wa kamati
            za uratibu za
            mikoa lakini badala yake Bwana Wegesa Suguta (John Heche)
            amekuwa
            akiwaita wenyeviti wamikoa na sababu kubwa ikiwa ni
            kwamba wengi wa
            wenyeviti hao hawastahili kuwepobavicha kutokana na
            kwamba umri wao
            kuwa zaidi ya miaka 35 hivyo kupoteza sifa za kuwa
            viongozi wa BAVICHA
            ambayo katiba inamtaka mwanabavicha yeyote kuwa namiaka
            18-35, hivyo
            basi kwa kuhofia kupoteza nafasi zao hulazimika
            kukubaliana na lolote
            lile ambalo bwana Wegesa Suguta analitaka hata kama
            wakijua kwamba ni
            kinyume kabisa na matakwaya katiba na mwongozo wa baraza.

            Hivyo kumpa Heche mwanya wakuamua lolote lileanalotaka
            ama kutumwa
            kulifanya. Kutokana na hilo natangaza wazikwamba kikao
            cha kamati
            tendaji kilichopita ni batili, chenye wajumbe batili,
            kimesimamiwa na
            viongozi batili kwa maana ya mwenyekiti na katibu wake maana
            wameshindwakuheshimu misingi ya kikatiba katika namna ya
            demokrasia ya
            chama chetu hivyo basi nachukua nafasi hii kuutangazia
            umma wa
            watanzania na wanachadema kwa ujumla wao kwamba maamuzi
            ya kamati
            tendaji yaliyotangazwa na kiongozi kilazana daraja la
            viongozi wa juu
            bwana Wegesa Suguta ni batili.

            Ndugu wana habari,
            Sifa ya Mwalimu ni kuweza kubadilisha hali ya umbumbumbu
            wa wanafunzi
            wake, Heche kama kiongozi, na Mwalimu kitaaluma (nina
            wasiwasi na
            ufaulu wake katika huo ualimu) alipaswa kuwa mfano bora
            kwa vijana wa
            Chadema kuwaelekeza na kuwafundisha namna ya kuheshimu
            misingi ya
            kikatiba ambayo kama chama na baraza tumejiwekea na
            tunapaswa kuifuata
            ni wazi kuwa Heche ameshindwa kuwa mfano bora kwa vijana,
            hajui kanuni
            za BAVICHA wala katiba ya CHADEMA, mkurupukaji,
            mropokaji, mwenye
            uwezo mdogo wa kufikiri, dikteta anayetumia mamlaka
            asiyokuwa nayo
            (akipewa mamlaka atatuchinja huyu) hivyo hafai kuwa hata
            Mwenyekiti wa
            serikali za mtaa, wala kuaminiwa popote kupewa nafasi ya
            kiuongozi. Ni
            wazi ubongo wake yeye nakatibu baraza bwana Munishi
            haujapewa tohara
            la kisiasa, ifike mahali wakubali kufundwa unyagoni na
            manyakanga wa
            kisiasa.

            KUHUSUKUVULIWA UANACHAMA WA BAVICHA;

            Ndugu wanahabari,
            Kuhusu kuvuliwauanachama wa Bavicha ambao moja kwa moja
            napoteza sifa
            ya kuwa mwanachadema namshangaa kiongozi huyu ambaye sifa
            yake kuu
            siku zote ni ukurupukaji kwa kusema kwamba nimevuliwa
            uanachama wa
            Bavicha huku akijua wazi Bavicha haijawahi kuwa na kadi
            za baraza.

            Katika mwongozo wa baraza lavijana kipengele cha 4.4
            KUJIANDIKISHA
            UANACHAMA 4.4.1 inasema ili kijanaaruhusiwe kujiunga
            bavicha ni lazima
            awe na sifa zifuatazo
            [a] Awe mwanachama wa CHADEMA
            [b] Awe na umri kati ya miaka 18 na 35
            [c] Awe anakubaliana na misingiya mwongozo wa BAVICHA

            4.4.2 Inasema kijana aliyekidhimatakwa hayo hapo juu,
            atanunua kadi ya
            uanachama wa BAVICHA

            Kutokana na kipengele hicho namtaka bwana Wegesa Suguta
            auambie umma
            wa watanzania na wanaCHADEMA kadi yake yeye ya baraza la
            vijana ni
            namba ngapi na aliichukulia wapi? Aueleze umma wa
            watanzania kadi
            yangu ya baraza la vijana ni namba ngapi na niliichukulia
            wapi?

            Ndugu waandishi wa habari,
            Nidhahiri baraza la vijana chadema hatuna kadi ambayo
            kimsingi ndiyo
            utambulisho wa mwana BAVICHA endapo akishakidhi sifa
            zilizoainishwa
            hapo juu. Na ni wazikwamba vijana wote wa CHADEMA tuna
            sifa za kuwa
            wana Bavicha lakini si wanachama wa BAVICHA kutokana na
            kwamba
            nimekuwa nikimwambia mara kwa mara umuhimu wa kuirasimisha na
            kuianzisha ili iwe taasisi kamili kwa kuwa na kadi za
            vijana kama
            mwongozo wa vijana unavyojieleza.

            UELEWA WANGU KUHUSUKUNDI ANALOLIITA NDUGU WEGESA SUGUTA
            (JOHN HECHE)
            NI "MASALIA"

            Ndugu waandishi wa habari,
            Hakuna kundi linaloitwa masalia ndani ya Chadema na
            BAVICHA. Gazeti la
            MWANAHALISI ndilo lililoandika kuwa vijana wote waliofutwa na
            kuondolewa kwenye uchaguzi wa BAVICHA mwaka 2011 ni
            MASALIA ya Zitto
            yanayopukutishwa Chadema. Kimsingi gazeti hili lilikuwa
            linafanya kazi
            yake ya kipropaganda ndani ya CHADEMA ili kukigawa Chama.
            Lilikuwa
            linatimiza wajibu wake wa kupika mpasuko ndani ya chama
            tena kwa
            kuhusisha na viongozi wakubwa ndani ya chadema.

            Ni aibu kubwa sana na ni hatari kuona kiongozi kama
            Wegesa Suguta
            anakuwa mstari wa mbele kushabikia neno masalia, huku
            akijua wazi
            kufanya hivyo ni kuligawa baraza la vijana. Kwa nguvu
            moja nalaani
            kitendo hiki cha kipuuzi kinachofanywa na Mwenyekiti huyu
            wa BAVICHA
            cha kuchekelea upuuzi uliopikwa na gazeti la MwanaHalisi.
            Naomba
            atumie rasilimali za chama kujenga umoja wa vijana imara,
            tushirikiane
            kuimarisha Bavicha yenye tija kwa chama na sio kusherekea
            mpasuko
            ndani ya baraza la vijana.


            UELEWA WANGU KUHUSU KITU KINACHOITWA PM7

            Ndugu waandishi wa habari,
            Naomba kunukuu maneno ya mtu maarufu sana mitandaoni na
            kwenye uga wa
            habari Mzee Mwanakijiji anasema
            "Uongozi imara sio kutegeana, kunyemeleana na kufukuzana.
            Uongozi
            imara ni kushirikiana".

            PM7 ni jina lenye maana ya "PATRIOTIC MOVEMENT" yaani
            harakatiza
            kizalendo kwa mujibu wa Ndugu Ben saanane ambaye alitumwa
            na kiongozi
            wa juuwa chama kuja kulitekeleza kwa vijana walioenguliwa
            kwenye
            uchaguzi wa BAVICHAmwaka 2011 na wanaoonekana kusigana na
            kiongozi
            huyo kimawazo. PM7 ni wazoliliobuniwa na kiongozi mmoja
            wa juu wa
            chama akishirikiana na Ben saanane wakinuia kutega mtego
            wa kuwanasa
            vijana wanaoonekana wapo tofauti kimawazo nakiongozi huyo
            wa chama.
            Kwa kuwa wazo hilo lilikuwahalina manufaa kwa chama,
            halikutekelezwa.

            Kiongozi huyo bila kumung'unya maneno ameamua kuwatumia
            vijana hao
            kuandaa kikao batili cha kamati tendaji ya John Heche ili
            awafukuze
            vijana hao. Hii ni hatari sana kuona kiongozi wa chama
            unageuka simba
            na kuanza kuwawinda watoto wake ili uwamalize kisiasa kwa
            sababu zako
            binafsi.

            MAAJABU KATIKAMEDANI ZA SIASA ZA BAVICHA MWAKA 2013

            Ndugu waandishi wa habari,

            1. Hii ni ajabu sana katika kikaocha kamati tendaji
            batili, Ambao
            hatukuhojiwa ni watu wawili, mimi Juliana Shonzana kijana
            mmoja
            anaitwa Exaud Mamuya. Lakini Mimi Juliana Shonza
            nimehukumiwa bila
            hata kusikilizwa wala kupewa mashitaka na chombo chochote
            katika
            chama. Wakati huo huo Exaud Mamuya hajahukumiwa kwa madai
            hakufika
            kwenye kikao. Hii ni dhahiri huu ni mkakati wa kipuuzi ambao
            unaendeshwa na watu wapuuzi tena kwa misingi ya kikabila
            na kikanda.

            2. Muasisi mwenza wa PM7 na kibaraka wa kiongozi wa juu
            wa chama
            aliyetumika kutoa shutuma chafu kwa Naibu Katibu Mkuu. Kijana
            anayefahamika kwa jina la Ben Saanane ameachwa kwa madai
            yeye amekiri
            mbele ya hiyo kamati tendaji kwamba ni kweli alinuia
            kumchafua Naibu
            Katibu Mkuu wa chama na kukivuruga chama. Wakati tuhuma zake
            zinafananana za Mchange na Mwampamba.

            3. Mkakati wa John heche navibaraka wake umejikita
            kutukuza ukanda
            ndani ya chama tena wa wazi wazi.Ukanda huu
            umejidhihirisha kwenye
            kutoa hukumu batili za tuhuma kama ifuatavyo.

            Vijana waliohukumiwa wote niwale wanaotokea Mbeya, Mbozi
            na Kibaha.
            Wakati Vijana wa Kilimanjaro wameachwa kwa madai wao wametoa
            ushirikiano.

            Waliohukumiwa ni:
            _Mtela Mwampamba-Mbozi, Mbeya
            _Habib Mchange-Kibaha, Pwani
            -Juliana Shonza-Mbozi, Mbeya
            -Joseph Kasambala – Mbeya mjini (kasimamishwa)
            - GWAKISA Mwakasendo –Rungwe, Mbeya (kasimamishwa)

            Pamoja na wanachama watatu waliopo Mbeya mjini waliofukuzwa
            uanachama.

            Waliosamehewa ni:
            _Ben saanane-Kilimanjaro
            _Exaud Mamuya-Kilimanjaro.

            Hii ni dhamira ya wazi kabisa kwamba CHADEMA sasa ni
            chama cha
            kikanda, Viongozi wa CHADEMA wanatumika kutangaza ukanda kwa
            watanzania.

            Kwa maana hiyo wale wote wasio wa kaskazini ndani ya Chadema
            tusitegemee kutendewa haki.

            MAMBO NILIYOMSHAURI HECHE NA KUMUONYA:

            Ndugu waandishi wa habari, Sisikama vijana tusigeuze
            siasa kuwa ajira
            wala chombo cha kuendeshea maisha, ni moja ya vikwazo
            katika kukuza
            demokrasia ya kweli, maana wengi wanaendekeza njaa na
            uhitaji wa
            maisha yao ili kupindisha ukweli.

            Moja ya maswali yangu kwa Mwenyekiti ni kitendo cha
            kubinafsisha gari
            alilotoa Naibu Katibu Mkuu kwa ajili ya BAVICHA na badala
            yake
            akalifisadi, akafanya mali yake binafsi na kumuweka Mdogo
            wake Chacha
            Heche kuwa dereva wake, nimekuwa nikipinga matumizimabaya ya
            rasilimali hiyo kwa manufaa binafsi, na badala yake gari hiyo
            ifanyekazi iliyokusudiwa, huu ni msingi wa kuonyesha
            tofauti yetu na
            wanaotumiarasilimali za serikali (Taifa) kwa manufaa
            binafsi nay a
            familia zao.

            Pia nilimshauri Mwenyekiti awe nakipato halali kama
            katiba ya chama
            inavyosema Sura 10 MAADILI YA VIONGOZI ibara ya 10
            kifungu cha (6)
            kinasema Kiongozi anatarijiwa kujitosheleza yeye
            nafamilia yake kwa
            mapato halali ili kutokuwa ombaomba kwani tabia hiyo
            itadhoofisha
            uwezo wake wa kutoa uamuzi sahihi, ili kuwa mfano bora
            wauwajibikaji
            kwa vijana, kama ambavyo Mwalimu Nyerere alivyosema
            kipimo cha Utuni
            kufanya kazi, badala yake ametelekeza taaluma ya ualimu,
            aliyotumia
            pesa za walipa kodi kwa kusoma na muda wote ni kupiga
            soga bila
            uzalishaji na kujipatia kipato halali, na badala yake
            anategemea
            mshahara usio halali kuishi, ni wazi Mwenyekiti ni cheo
            cha kisiasa na
            hatakiwi kulipwa mshahara, wala kulipiwa nyumba kwa
            mujibu wa kanuni.

            Badala yake majibu anafikiri ni kufanya njama na
            waliopindisha
            taratibu hizo ili alipwe mshahara kwa maslahi yao ya
            kisiasa. Na
            tumekuwa tukilipinga hilo kwani tunataka tuwe mfano wa
            utawala bora
            kwa vitendo na si maneno peke yake.

            MWISHO:

            Ndugu waandishi wa habari,
            Nipokwenye mchakato na wanasheria wangu kushughulikia
            swala la
            kumpeleka mahakani Bwana John Heche na gazeti la Tanzania
            Daima toleo
            namba 2958 kwa kuniita msaliti wa CHADEMA, natumiwa na
            CCM na kuwa
            nina mahusiano (natumiwa) na Wassira tena bila kunihoji
            mimi Juliana
            Shonza. Kwa maana hiyo wamenichafua na kunidhalilisha
            mbele ya umma wa
            watanzania.

            Pili naomba kuweka wazi kwambanatarajia kuomba ufafanuzi
            wa kikatiba
            juu ya shutuma zilizotolewa kwenye vyombo vya habari
            dhidi yangu na
            bwana Wegesa Suguta (John heche) ili aseme ni aminisho
            lipi la
            kuthaminisha na kusakidikisha mtazamo wa maono yake ili
            bongo za
            watanzania zijue ukweli. Mimi Makamu Mwenyekiti wa
            BAVICHA natangaza
            rasmi Mtela Mwampamba na Habib Mchange ni wanachama hai
            na halali wa
            Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

            Hivyo nawaomba waendelee na kazizao za ujenzi wa chama
            kwenye majimbo
            yao na taifa kwa ujumla. Nawaomba wananchi na wanachama
            wote wa
            CHADEMA waendelee kuwa na imani dhidi ya vijanahawa. Kama
            mlivyomwamini Mwampamba na kumpa kura 32000 na kama
            mlivyo mwamini
            Mchange na kumpa kura 10,400 kwenye uchaguzi wa Ubunge
            mwaka 2010.
            Vivyo hivyo naowaombamuendelee kushirikiana nao
            kuhakikisha wanatimiza
            adhima ya ukombozi mwaka2015.

            Wenu katika ujenzi wa demokrasia makini

            Juliana Daniel Shonza

            M/Kiti BAVICHA-Tanzania Bara.

            --
            Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
            <http://www.wejobs.blogspot.com>
            International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
            <http://www.jobsunited.blogspot.com>

            Kujiondoa Tuma Email kwenda
            wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
            <http://us.mc1411.mail.yahoo.com/mc/compose?to=unsubscribe%40googlegroups.com>
            Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

            Disclaimer:
            Everyone posting to this Forum bears the sole
            responsibility for any legal consequences of his or her
            postings, and hence statements and facts must be
            presented responsibly. Your continued membership
            signifies that you agree to this disclaimer and pledge to
            abide by our Rules and Guidelines.



        --
        Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
        <http://www.wejobs.blogspot.com>
        International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
        <http://www.jobsunited.blogspot.com>

        Kujiondoa Tuma Email kwenda
        wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
        <mailto:wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com> Utapata
        Email ya kudhibitisha ukishatuma

        Disclaimer:
        Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
        for any legal consequences of his or her postings, and hence
        statements and facts must be presented responsibly. Your
        continued membership signifies that you agree to this
        disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.




    --
    Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
    <http://www.wejobs.blogspot.com>
    International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
    <http://www.jobsunited.blogspot.com>

    Kujiondoa Tuma Email kwenda
    wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
    <mailto:wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com> Utapata Email
    ya kudhibitisha ukishatuma

    Disclaimer:
    Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for
    any legal consequences of his or her postings, and hence
    statements and facts must be presented responsibly. Your
    continued membership signifies that you agree to this disclaimer
    and pledge to abide by our Rules and Guidelines.




--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
legal consequences of his or her postings, and hence statements and
facts must be presented responsibly. Your continued membership
signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by
our Rules and Guidelines.


--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
legal consequences of his or her postings, and hence statements and
facts must be presented responsibly. Your continued membership
signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by
our Rules and Guidelines.


--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
legal consequences of his or her postings, and hence statements and
facts must be presented responsibly. Your continued membership
signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by
our Rules and Guidelines.



--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
legal consequences of his or her postings, and hence statements and
facts must be presented responsibly. Your continued membership
signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our
Rules and Guidelines.


--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
legal consequences of his or her postings, and hence statements and
facts must be presented responsibly. Your continued membership
signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our
Rules and Guidelines.



--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment