Saturday 1 December 2012

[wanabidii] RE: WIZARA YA MALIASILI NA SHIRIKA LA TANAPA CHIMBIENI WANYAMA MAJI

Mimi nadiriki kusema Tanzania inaingiza fedha nyingi sana kutokana na Hifadhi za Taifa Tanzania lakini sielewi fedha hizi zinaenda wapi na zinafanya kazi gani nchini. Wizara na Shirika la Tanapa vinaendeshwa kisiasa. Watu wanaangalia fedha inayoingia inufaishe familia zao lakini hawajali wanyama wanaoingiza fedha hizo. Hivi Tanzania ilivyo na vyanzo vingi vya maji inakuwaje Wasomi wa Wizara ya Mali asili na utalii na Shirika la Tanapa wanaangali wanyama wakifa kwa kukosa maji kwenye mbuga za Katavi na Mahale.

 

Kwa nini fedha zinazoingia zisichimbe maji toka ardhini yakaweza kuponyesha Wanyama wanaokufa hifadhini. Au Serekali ya CCM imebweteka na misaada toka nje hivyo inasubiri waletewe mafungu ya misaada toka Marekani na kwingineko. Wizara ya Mali Asili na utalii tumieni akili mlizopewa na Mwenyezi Mungu chimbeni maji ardhini kuokoa maisha ya Wanyama wanaotuingizie fedha mnazoiba na kwenda kuzificha Ulaya.

 

Hii ni aibu kuona wanyama wanakufa wakati Dunia iko juu ya maji. Mbona watu binafsi tunachima maji nyie kama Wizara na Shirika mnashinwa nini kuchimba.maji. Mtakosa Wanyama wa kuuza mpate fedha na familia zenu. CCM kuweni wabunifu sio kungoja masaadfa kwa kila kitu duh mnaboa.

Mkereketwa

Lengai Ole Letipipi

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,2 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment