Friday 28 December 2012

Re: [wanabidii] Re: KAFUMU AKATA RUFANI - AIBU NYINGINE KWA CCM

Waacheni watumie haki yao ya kimahakama japo kufungua kesi au kukata rufaa huku UKIJUA UAMUZI utakuwaje ni upuuzi na kukosa uzalendo. Kesi hizi zinagharimu pesa nyingi na muda wa thamani ambao ungeweza kutumika kulijenga taifa letu.

Mara baada ya kumalizika uchaguzi wa 2010 CCM walifungua kesi dhidi ya washindi karibu wote wa CHADEMA, na matokeo ya kesi zote walizofungua HAWAJASHINDA HATA KESI MOJA. Ndipo tunapojiuliza, ina maana CCM haina watu werevu na taaluma nzuri ya sheria wanaoweza kuangalia mashtaka kabla ya kukurupuka kwenda mahakamani?

 Ilitegemewa chama tawala kiwe na nyenzo nyingi zaidi ikiwa ni pamoja na weledi na umakini lakini inakuwa kinyume.

CHADEMA katika kesi zote walizofungua dhii ya washindi wa CCM wameshinda zote isipokuwa ile tu ya jimbo la Ukonga, huo ndiyo umakini, hapo CCM wana kitu cha kujifunza.

Bart
Sent from Samsung Mobile



hkigwangalla@gmail.com wrote:


CCM wakikata rufaa mnaita delaying tactic...mbona hamsemi ile ya Arusha?
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

-----Original Message-----
From: mngonge <mngonge@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Fri, 28 Dec 2012 19:05:22
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Reply-To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Re: KAFUMU AKATA RUFANI - AIBU NYINGINE KWA CCM

Hiyo ni delaying tactic ya CCM hawataki uchaguzi uitishwe huku wakijua
wazi kwamba sababu zilizotajwa na jaji haziachi shaka lolote

2012/12/24 Selemani Rehani <srehani@hotmail.com>:
> KAFUMU AKATA RUFANI
>
> Simba aliliambia NIPASHE kuwa rufaa ya Dk. Kafumu ilikatwa kupitia Wakili
> wake, Kamaliza Kayaga, takriban wiki tatu zilizopita, na tayari taarifa
> kuhusu rufaa hiyo zimekwisha andaliwa kwa ajili ya kupelekwa Mahakama ya
> Rufani ili kupangiwa tarehe ya kusikilizwa.
>
> "Wameshafaili na kulipia kila kitu. Notisi (taarifa) zao zimekwisha
> andaliwa. Tunasubiri kupeleka Mahakama ya Rufaa, ambayo ndiyo itapanga
> taratibu lini vikao vitafanyika," alisema Simba.
>
> Uamuzi uliotengua ubunge wa Dk. Kafumu ulitolewa na Jaji wa mahakama hiyo,
> Mary Shangali, Agosti, mwaka huu, baada ya kuridhika na pingamizi la
> mlalamikaji katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mdogo wa jimbo hilo,
> uliofanyika Oktoba 2, mwaka jana.
>
> Akisoma hukumu hiyo, Jaji Shangali alisema kuwa Mahakama imeridhika na hoja
> saba za upande wa mlalamikaji, ambazo alisema zinathibitisha na kuonyesha
> kuwa uchaguzi huo mdogo wa Jimbo la Igunga haukuwa huru na haki.
>
> Alizitaja baadhi ya kasoro zilizosababisha kutenguliwa kwa matokeo ya
> uchaguzi huo ni pamoja na ahadi iliyotolewa na Waziri wa Ujenzi,  Dk. John
> Magufuli, kuhusu ujenzi wa daraja la Mbutu ambalo wakati wa kampeni alidai
> kwamba kama wananchi hawataichagua CCM, daraja hilo halitajengwa. Waziri
> huyo alitoa ahadi hiyo katika kipindi hicho ambacho kulikuwa na shida kubwa
> ya usafiri katika eneo hilo.
>
> Jaji Shangali alisema kuwa pia Waziri Magufuli alitumia nguvu  na kuwatisha
> wapiga kura kwamba kama hawatamchagua mgombea wa CCM, watawekwa ndani, kitu
> ambacho alisema kilitishia uchaguzi huo kuwa huru na wa haki.
>
> Jaji Shangali alisema kitendo kilichofanywa na Mbunge wa Tabora Mjini,
> Ismail Aden Rage (CCM), kwamba mgombea wa Chadema amejitoa katika uchaguzi
> huo, hakikuwa cha kiungwana kwani alitumia lugha ya uongo kwa lengo la
> kupotosha wapiga kura.
>
> Alisema pia Rage alihusika katika vitendo vya kujenga hofu kwa wapiga kura
> baada ya kupanda jukwaani na bastola, hali ambayo iliwafanya wapiga kura
> kuhofia na hivyo kuleta dosari katika uchaguzi huo. Jaji alisema kuwa hoja
> hiyo imezingatiwa na Mahakama.
>
> Jaji huyo alioonyesha kusikitishwa na kitendo kilichofanywa na Imamu wa
> Msikiti wa Ijumaa wa Igunga, Sheikh Swaleh Mohamed, kutangaza msikitini
> akiwataka waumini wa dini ya Kiislamu wasikichague Chadema kwa madai kuwa
> viongozi wake walihusika kumdhalilisha aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga,
> Fatma Kimario.
>
> Kadhalika, Jaji Shangali aliithibitisha kuwa kauli iliyotolewa na Katibu
> Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, kuwa Chadema kimeingiza makomandoo katika wilaya
> ya Igunga kwa lengo la kuvuruga uchaguzi huo mdogo, ilikuwa na madhumuni ya
> kupeleka vitisho kwa wananchi.
>
> Kuhusu madai ya kugawa chakula wakati wa kampeni, Jaji Shangali alisema
> kitendo cha serikali kugawa mahindi ya msaada kwa wakazi wa Igunga katika
> kipindi cha kampeni kimeleta fedheha kubwa kwa wapiga kura. Alihoji, je; ni
> nani aliyekufa njaa katika kipindi hicho na kwamba kulikuwa na umuhimu gani
> kugawa mahindi katika kipindi cha kampeni?
>
> Kesi hiyo ilifunguliwa na Kashindye, ambaye aliwakilishwa na wakili maarufu
> nchini, Profesa Abdallah Safari, akipinga matokeo ya uchaguzi huo kwa
> kulalamikia ukiukaji wa sheria ya uchaguzi.
> CHANZO: NIPASHE
>
> --
> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
> nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> DELL LATITUDE D 620 & D30
>
> 80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
> DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
>
> TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
>
> CALL : 0786 806028
> Free Delivery in Dar es salaam
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

DELL LATITUDE D 620 & D30

80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .

TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY

CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

DELL LATITUDE D 620 & D30

80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .

TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY

CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


0 comments:

Post a Comment