TB imezagaa ni kweli na TZ tusipojiangalia tutaisha. Asilimia 52 ya walio HIV positive wameonekana kuwa na TZ. Cha kuhudhunisha ni zile tabia zetu za kula mama na baba ntilie ambapo mtu anakula na kutemea mezani au katika sahani mifupa. Kitambaa cha kufutia meza hiyo hufutia sahani anayoletea chakula na mikono yake aliyofutia mate ya wengine anashika sahani bila kunawa. Kisha pamoja na sheria za afya-haoshei vyombo vichangiwavyo kwa kusuuza kwa maji ya moto. Anaoshea maji ktk ndoo moja na kusuuza vyombo hvyo ndoo moja maji hayo hayo. Yaani anachanganya TB ndoo ya mwanzo anasuuza humo vyote bila kubadili maji au kuosha kimoja kimoja ktk maji mchirizi-yaani anatawanya TB kwa kuoshea vyote tena mara ya mwisho maji ndoo moja vyombo vyote. Vijana na wafanyakazi hula huko ntilie na wengine mobile food vendors mitaani na maofisini uoshaji ndio hivyo. Chanjo za TB kwa watoto au mashuleni twakimbia. Mnyama-Nyegele (Badger) ambaye hucheua katika majani alayo ng'ombe ndio host wa TB na kutusambazia wote tunywao maziwa bila ya kuchemsha, nyasi tuwapazo mifugo na kuacha mifugo ilambe vyombo vyetu. basi la abiria madirisha kufungwa yote na tunakoholeana toka Dar-Arusha, tunalinda nywele zisipeperuke. Mbanano wa majumba mitaani na haya magorofa yanayozuka na kubana nyumba fupi hewa safi hakuna. Hata cafeteria za vyuo vya wasomi utaona vyombo vinatolewa uvungu wa meza huoni maji ya moto kutiririka kutoka bomba akisuuza kikombe anachokuwekea chai. Yet, kuna wasomi, mamlaka za uwekezaji na afya lakini kichemsha maji cha maji ya hakuna na kila mtu anaona na huyo ni investor hapo kwa wasomi. Koto ni " Changanya TB-Tawanya/sambaza TB". Mungu ibariki bongoland. --- On Sat, 1/12/12, Augustino Chengula <achengula@gmail.com> wrote:
|
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
DELL LATITUDE D 620 & D30
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,2 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment