Sunday, 1 March 2015

[wanabidii] Fwd: UASI.


Subject: UASI.

                                 UASI.
           (Dkt.Muhammed Seif Khatib)
    Uasi ni kinyume na utii.Binadamu kimaumbile ya kitabia ni mwasi.Maumbile yake,akili yake na maarifa yake anapenda kufanya kila alitakalo bila ya
kizuizi.Binadamu ni mnyama na dunia ni msitu.Mwenye nguvu hutenda atakalo
na alipendalo.Kama alivyo simba na chui katika mbuga hufanya kila alitakalo
ndivyo ilivyo kwa binadamu katika dunia.Wenye nguvu huwaonea wadhaifu. Hilo silo geni kwa viumbe wa majini samaki mkubwa humeza mdogo. Hata katika ulimwengu mataifa yenye nguvu za kiuchumi, kijeshi na kiteknolojia kinachotokea ni kuzivamia dola dhaifu na
kuzichapa.Dunia ya sasa mwanadamu ameunda vyombo vya kimabavu ili amuadhibu yule
anaye asi na asiyetii. Hivi jela kazi yake nini? Polisi anamtumikia nani? Mahakama ipo
kwaajili ya nani?Jeshi na zana zake kwaajili ya nani? Wakuu wa Mahakama, Jela,
Polisi na Jeshi anayeteua nani? Uliwahi wapi kusikia kuwa viongozi hawa wanachaguliwa
kwa kura?Vyombo na viongozi wake wanatumikia watu maalumu.Nia kuu kuwaadhibu wale
wanaoasi.Wale wasiotii.Uasi hakunza leo na jana au juzi. Dunia inaumbwa zaidi ya miaka
4.5 Billioni miaka binadamu amekuwa asi.Waumini wa dini wanazo kanuni za kuwafanya
wawe watii.Dini zimeteremshwa kuudhibiti uasi.Dini ya Kiristo iliyoasisiwa na Issa zaidi ya
miaka 300 iliyopita imekuja kuuvunja uasi wa binadamu.Kitabu chake Bibilia mandiko
yake juu ya upendo na utii.Yesu au Issa aliifanya kazi hiyo kwa kutoa hoja za kutosha lakini
binadamu muasi hakumuamini na shaka sulubu.Kitabu cha Biblia kikawa mwongozo.Makanisa yakawa majengo ya kuabudu na Jumapili ni siku ya ibada. Dini hii
yenye wafuasi billioni mbili imeenea ulaya,Amerika na Afrika.Sina hakika waumini wake
wote hawa ni watii na si asi.Ukiristo ulitanguliwa Judism huko Palastine miaka 1800 kabla
ya kuzaliwa Yesu.Dini hii yenye wafuasi 14 millioni mwasisi wake ni Musa.Ibada zao huwa
katika mahekalu. Ni dini ya zamani yenye malengo ya kuvunja uasi wa binadamu.Kwa kiasi
gani waumini wake ni watii? Karne ya saba huko Saudia katika mji wa Makka Muhammad
akazaliwa.Kwa kutumia kitabu cha Koran kwa sa miaka kumi na mbil akatangaza
na kueneza Uisilamu..Kwa kutumia Koran, viongozi wa dini maimamu na muadhini wafuasi
wakafika sasa billioni 1.5 duniani wanatakiwa wasiasi.Waisilamu siku kuu ya Ibada ni
Ijumaa. Wafuasi Judism ni Jumamosi na Wakristo ni Jumapili. Kwa kiasi gani siku hizi za
ibada kwa kila dini zimesaidia binadamu asi asi? Musa ni Hebrew, Muhammad ni Mwarabu
na Yesu ni Yahudi wote kutoka Mashariki ya Kati.Jee makabila yao na maeneo ya uasisi
wa dini hizo hakuna uasi? Waisilamu wamemegeka kati ya Suni na Shia. Uhusiano wao
ni mbaya ingawa wanaamini Mungu Mmoja,Nabii mmoja na kitabu kimoja.Nao wamekiasi
kitabu chao. Wakristo wanaamini Yesu na Biblia lakini madhebu yapo mengi.Kila kukicha
makanisa yanazuka,Manabii,Mitume na Miungu inatokea na kuhubiri biblia. Huu siyo uasi
kitabu na Yesu. Waisilamu kwa Waisilamu wanauwana na kuchinjana kila kukicha. Wakristo kwa Wakristo wanauwana. Waisilamu wanawachukia Wakristo. Wakristo
hawawataki wa Waisilamu. Utukufu wa dini zao za kuonesha upendo na amani uwapi?
Mwenendo wa mazuri wa Yesu, Muhammad na Mussa haufatwi.Huko Arabuni katika
chimbuko za dini hizi kubwa imekuwa leo uwanja wa mauaji.Binadamu ni asi.Waumini ni asi.
Viongozi wa dini ni asi. Zawadi walioahidiwa binadamu katika vitabu vyao vya dini kupewa
baada ya kufanya mema hapa duniani baada ya mauko yao watazikosa. Hilo wanalijua.
Adhabu watakapewa kwa kuasi hapa duniani waumini wanazitambua. Lakini bado wanaoasi.Mwaka 1992 vyama vya siasa vya upinzani vikaruhusiwa nchini.Kwa vile
binadamu ni asi haikuchukua muda vyama vikajitokeza na kubeba bango la uasi kwa
jina la upinzani. Wote viongozi wa vyama vya upinzani walikuwa ndani ya chamatawala.
Chama kilichowakomboa.Chama kilichowaletea Mapinduzi. Chama kilichowarejeshea
heshima ya utu wao. Chama kilichoanza safari ndefu ya kuwaletea maendeleo katika
maisha yao. Lakini kwa vile binadamu kwa hulka,silka na tabia ni asi, macho yao yakawa
kama yanatongotongo hayaoni. Masikio yakapata komango yakawa hayasikii.Lakini
midomo yao ikapata  nguvu ya kuponda kila kitu kilichofanywa na chama tawala.Hali hii
inaendelea hadi leo. Kama binadamu ameweza kuwa asi kwa dini zao, vitabu vyao, mitume
yao na Mungu wao siuze itakuwa kuasi Chama Cha Mapinduzi? Kama binadamu ni asi
kwa mamlaka inayotawala na haogopi jela,mahakama,polisi,jeshi na vyombo vya utawala
atachelea kukiasi Chama Cha  Mapinduzi?Uasi umo ndani ya damu na mishipa ya binadamu.Chama Tawala kifanye wajibu wake na kitambuwe upinzani wa siasa ndani
ya Tanzania ni sehemu ya UASI wa binadamu.Chambilecho Waswhili husema ' Kelele za
Mpangaji hazimzuii Mwenye Nyumba kulala '

K




Sent from my iPad

0 comments:

Post a Comment