Duuh,hivi mpaka leo hawajakupa Udc wa Wilaya yoyote Mpya,Bibie?.Yaani mpaka wakiondoka Madarakani hawajakupa Ukuu wa Wilaya,watakuwa wamekuonea sana,maana ajaye hatumjui kama atapenda Mbwembwe na maneno yako au hapana.
--------------------------------------------
On Fri, 3/13/15, 'lesian mollel' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] ZITTO NDIO UJUE MUOSHA UWOSHWA TENA WAKATI WA KUOSHWA ULIPULIWA
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Friday, March 13, 2015, 12:16 AM
katabazithe lady
who always write millions of pontless words, we hate
youuuuuuuuuuuuuu
From: 'frank
chalamila' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com>
To:
"wanabidii@googlegroups.com"
<wanabidii@googlegroups.com>
Sent:
Thursday, March 12, 2015 9:08 AM
Subject: Re:
[wanabidii] ZITTO NDIO UJUE MUOSHA UWOSHWA TENA WAKATI
WA KUOSHWA ULIPULIWA
duniani kuna mambo
On Thursday, March
12, 2015 5:49 PM, 'Happiness Katabazi' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com> wrote:
ZITTO
NDIO UJUE MUOSHA UWOSHWA TENA WAKATI WA KUOSHWA
ULIPULIWA
Na Happiness
Katabazi
MACHI 10 Mwaka
huu, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mziray
alitoa uamuzi wa kumfukuza mahakamani kwa gharama ombi la
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe lililokuwa
Linaomba Mahakama hiyo itoe amri ya Kuzuia CHADEMA isiketi
vikao Vyovyote kumjadili wala Kumvua uanachama.
Jaji Richard Mziray Katika
uamuzi wake Katika Kesi hiyo ambayo mlalamikaji ni Zitto
Kabwe dhidi ya Bodi ya Wadhamini ya Chadema na Katibu Mkuu
wa Chadema ambapo Madai ya Msingi ya Zitto alikuwa
anaiomba Mahakama hiyo itoe amri ya Kuzuia Chadema
isifanye vikao Vya kumjadili na kutoa maamuzi uamuzi wowote
dhidi yake.
Jaji Mziray
alisema Kabla ya Kesi hiyo ya Msingi kuanza kusikilizwa
wadaiwa hao waliwasilisha jumla ya mapingamizi ya awali
matano.
Jaji Huyo alisema
mahakama yake imeamua kutolea uamuzi mapingamizi mawili tu
Kati ya matano na kwa Sababu hiyo Mahakama yake imekubaliana
na mapingamizi mawili ya Mawakili wa wadaiwa na ndiyo
itayatolea uamuzi na mapingamizi yaliyosalia haitaitolea
uamuzi.
Pingamizi la kwanza
lilowasilishwa na Wakili wa wadaiwa Peter Kibatara na John
Malia ,waliomba Mahakama hiyo iifute Kesi ya Zitto .
Pingamizi la pili kesi ya
Zitto ilifunguliwa Katika Mahakama hiyo kimakosa kwasababu
Kesi yake hiyo Zitto Alipaswa aka ifungue Katika masijala ya
Wilaya ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kwa maana
kwamba Zitto alipaswa kufungua kesi yake msingi katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi na siyo Kuifungulia Masijala Kuu ya
Mahakama Kuu (main registry)
Jaji huyo alisema (Main Registry) zilianzishwa
kwaajili ya kuendesha Kesi Maalum na zaidi zaidi Kesi za
Kikatiba , hivyo akatupilia mbali kesi ya Zitto kwa
gharama.
Jaji Mziray
amesema amekubaliana na pingamizi la Chadema lililotaka
mahakama hiyo iifute kesi ya Zitto kwasababu haikupaswa
kufunguliwa Mahakama Kuu na kwamba ilipaswa kufunguliwa
katika mahakama za ya Hakimu Mkazi(Subordinate Court).
Ikumbukwe kuwa, mwaka jana
Zitto Kabwe aliweka pingamizi mahakamani kuzuia kikao cha
Kamati Kuu ya chama hicho kumjadili mpaka pale
shauri lake litakaposikilizwa na Baraza Kuu la
Chama hicho.
Zitto hukujua Hilo.
Binafsi nimefurahishwa na
uamuzi huo wa Mahakama Kwani uamuzi wa haki na uliokidhi
matakwa ya kisheria na pia uamuzi huo pia umetoa Funzo kwa
Mawakili wakurupukaji kama Wakili wa Zitto, Albert Msendo
ambao wanatabia ya kukurupuka Kufungua Kesi mahakamani bila
kwanza kujipa muda wa kutafari kisheria Je Kesi hiyo hiyo
anayotaka kwenda Kuifungua Katika Mahakama anayokusudia
Kuifungua, Je Mahakama hiyo Ina mamlaka ya kusikiliza Kesi
hiyo ya mteja wake?
Pia
uamuzi wa Jaji Mziray pia umetoa Funzo wasomi wa Sheria wa
kufahamu madhumuni ya kuanzishwa Masijala Kuu ya Mahakama
Kuu na kwamba masijala ile ni Maalum kwaajili ya
kushughulika na Kesi Maalum Kama za Kikatiba na nyingine
zenye upekee.
Licha Ibara ya 13(5)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, inakupa haki ya kukata
rufaa Mahakama ya rufaa kupinga uamuzi huo wa Mahakama
Kuu.
Mimi binafsi siku
shauri ukate rufaa kwasababu ni wazi Chadema tena wakiwemo
viongozi wa juu wa Chama hicho na baadhi ya wafuasi wake
hawakutaki na hawakuitaji tangu muda mrefu kwa kile
wanachokidai Kuwa muda mrefu wamekubaini wewe sisi watoto wa
mjini tunakuita wewe ni sawa na ' Chaja ya Kobe'
kila simu unaichaji, yaani Simu ya Nokia ,Huwawei na simu
nyingine zote Betri zake unaichaji yaani umekuwa ukiisaliti
Chadema kwa Chama ambacho wanapingana nacho kimtazamo na
kisera.
Kwanini
unang'ang'anie Mpenzi asiyekupenda?Chadema
hawakutaki, wamekuchoka kwa kile wanachodai wewe
unawavurugia Chama chao, achana nao endelea na ule mipango
yako ambayo unafikiri ni Siri wa kwenda kujiunga rasmi na
Chama chako ulichokiasi kwa siri cha ACT.
Taarifa zilizopo ulikuwa
umejipanga umejipanga kuama Chadema kwa mbwembwe na Lundo
la wanachama na taarifa hizo zinaenezwa na baadhi ya
wanachama wa ACT na watu wako wa karibu na baada ya kuama
ufanye Kama anavyofanya Nape Nnauye na Abdulahaman Kinana
kuzunguka nchi nzima kuinanga Chadema.
Kwa hiyo Kama taarifa za Mpango huo wa kuama
Chadema ni za kweli basi huna budi kuipongeza Mahakama
Kuu kwa uamuzi wake wa Jana Katika Kesi yako
iliyotupwa.
Kwani uamuzi
huo ni Kama umekurahisishia kukufunganisha virago Chadema
au uende kukata kupinga Katika Mahakama ya Rufaa, au
uende Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,
ukafungue Kesi hiyo iliyotupwa Jana na Mahakama Mahakama Kuu
maana Jaji Mziray Kasema Kesi yako Ulipaswa ukaifungulie
Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na siyo Katika
Masijala Kuu ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Kama
Huyo Wakili wako Albert Msendo alivyokuingiza
'Chaka' utafikiri sio msomi wa Sheria Akaamua
Kufungua Kesi yako iliyotupwa Jana Katika Mahakama iliyokuwa
haina mamlaka ya kuisikiliza Kesi yako.Kihoja cha aina
yake.
Uamuzi wa Mahakama
Kuu wa Kuitupa Kesi ya Zitto na uamuzi wa Chadema wa
kumfukuza uanachama Zitto binafsi naufananisha na '
Kumkata Ng'ombe Mapembe na mwisho wa siku Ng'ombe
anayekatwa mapembe anabakia kuonekana kama Sungura.
Namuuliza Zitto hivi wale
waliokuwa 'wanakubust' kwenye Sakata la Escrow Mbona
wameshindwa kukusaidia 'kufanya maghumashi ' ili
Kesi yako hii isitupwe na Mahakama? Na Mbona wale waliokuwa
wanakubusti wameshindwa kuizuia Chadema isikuvue uanachama?
Tambua sasa Ndio
wameishakubwaga sasa wamekaa pembeni wanakutazama unavyo
zama Baharini kisiasa wanakucheka wala hawakuokoi,wanaenda
Kutafuta mwanasiasa mwingine ambaye bado haja chafuka waanze
kumtumia.Kweli Ndege Mjanja unasa Katika Tundu bovu.Zitto
alijifanya mjanja sasa Kanasa Kwenye mtego.Kiko wapi?
Maana Tayari baadhi ya wabunge
na wewe Katika majadala wa Escrow mlipayuka sana bungeni na
kuushambulia Mhimili wa Mahakama wazi wazi tena bila
vielelezo Kuwa Mahakama inanuka na majaji wake ni
wachafu.
Tufanye basi ni
kweli Mahakama imeoza na Majaji wake ni wachafu ,iweje yeye
na wale waliokuwa 'wakimbust Zitto' Kwenye Escrow
wameshindwa kumhonga Fedha Jaji Mziray ili atoe uamuzi wa
kumpendelea Zitto?
Zitto na
Mbunge wa NCCR- Mageuzi , David Kafulila Ubunge wao ulikuwa
umeshikiliwa na Mahakama na Kafulila ameshitakiwa na
Lugemalila Mahakama Kuu kwa kesi ya madai ya fidia na bado
Kesi zao zinaendelea ila Kesi hiyo ya Zitto imemalizika
Jana.
Lakini ndiyo walikuwa
vinara wakuu paka matope Mhimili wa Mahakama na kuwaundia
watu mashitaka kuhusu Escrow kuwa ni wezi ,mafisadi
mashitaka ambayo mwisho wa siku Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa iliwafikisha watu katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu kwa kosa la kupokea rushwa kutoka Katika
akaunti ya Tegeta Escrow kinyume na Kifungu cha
15(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11 ya
Mwaka 2007.
Zitto,Kafulila
,Deo Filikunjombe kupitia vinywa vyao kila kona walikuwa
waliaminisha umma Kuwa Fedha zile ni za umma na zimeibwa na
baadhi ya watu waliowataja Kwenye ripoti ya PAC ambayo
Mwenyekiti wa Zitto Kabwe.
Wasomi wa Sheria nikiwemo Mimi niliandika
makala za kupinga wazi wazi kiwa Katika Escrow Hakuna kosa
la wizi kisheria baadhi ya watu wenye akili timamu
walinielewa ila kwa wale Bendera Fuata upepo Hawakutaka
kunielewa.
Lakini Desemba
Mwaka Jana , Rais Jakaya Kikwete Katika mkutano wake na
wazee wa Dar es Salaam Katika hotuba yake alisema Fedha za
Escrow Si mali ya umma na Kama siyo mali ya umma umma
haiwezi kuwashitaki wa nafariki wa Fedha zile kwa makosa ya
wizi Kama tulivyokuwa tumeaminishwa Ujinga na baadhi ya
wabunge na Kamati ya Zitto na Kafulila Kuwa Fedha za Escrow
ni mali ya umma na zimeibwa kwa Magunia.
Watu wenye akili timamu na tunaoona mbali na
kufahamu mhimili wa Mahakama ni nini na unafanyaje kazi ,
tulipowaona hao wabunge wa Mahakama wanapoteza muda mwingi
kupayuka majukwaani badala kuongeza nguvu katika kesi zao
tuliishia kujisemea moyoni msemo huu: ' Usimtukane
Mamba Kabla ujavuka Mto.
Binafsi Nina Imani na Mhimili wa Mahakama hapa
nchini Kama kuna watendaji wake wanafanya vitendo Vya utovu
wa Maadili ,wanafanya vitendo hivyo wao Binafsi na
hawajatumwa na mahakama hivyo haikuwa vyema kwa baadhi ya
wabunge wetu wakati wa kujadili ripoti ya PAC kuusisha
Mhimili wote wa Mahakama Kuwa unalea na kukumbatia mafisadi
wa Escrow na kwamba majajaji Wawili ni mafisadi pale
Mahakama Kuu ilipotoa amri ya Kuzuia suala la Escrow
lisijadili we bungeni.
Ibara ya 107A(1) ya Katiba ya nchi ambayo
inasema Mhimili wa Mahakama ndiyo una jukumu la kutoa
maamuzi ya haki Katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa Kuwa Mahakama haifanyi
Kazi zake kwa mashinikizo , siasa chafu au kutazama sura au
Cheo cha Mtu Bali inafanyakazi kwa kufuata Sheria na Kanuni,
tusubiri uamuzi wa Mahakama Kuu katika Kesi ya Madai ya
Kashfa ya Lugemalila dhidi ya Kafulila, Kesi ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali mstaafu ambaye Enzi alikuwa Mwanasheria
Mkuu alishiriki kikamilifu kuandaa Mabadiliko makubwa ya
Sheria za nchi hii na Kada wa CCM, Andrew Chenge '
Mtemi Chenge ambaye anakusudia Kuwasilisha ombi lake la
Mahakama Kuu la kuomba Mahakama hiyo iseme Je Sekretarieti
ya Maadili ya Viongozi wa Umma Ina mamlaka ya kusikiliza
shauri linalomkabili la kuvunja Maadili ya uongozi wa umma
au laa.
Kwani Licha ya
Chenge kuwasilisha amri ya zuio iliyotolewa Mahakama Kuu
mwaka Jana inayokataza Taasisi zote za umma zisijadili
suala la Escrow hadi Kesi za Msingi zilizofunguliwa na
kampuni ya IPTL mahakamani hapo zitakapotolewa uamuzi.
Sisi wasomi wa Sheria
tunasubiri kwa shahuku kubwa uamuzi huo wa Mahakama
utakaotolewa Kwenye Kesi hiyo ya Chenge kwasababu
utaandika historia mpya ya kisheria (Precedent) Kuwa Je ni
kweli Bunge au Taasisi zao zote za kiserikali zina mamlaka
ya kisheria ya kukataa kutekeleza amri hiyo ya Mahakama
iliyotolewa na Mahakama Kuu Katika Kesi ya IPTL iliyozuia
Bunge na Taasisi zote za kiserikali zisijadili suala la
Escrow hadi Kesi za Msingi zilizofunguliwa na Escrow
zitakapomalizika mahakamani au la.
Pia tunasubiri uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya
Dar es Salaam, Katika Kesi iliyofunguliwa na Kampuni ya
Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kumfungulia
mashtaka Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR- Mageuzi), David
Kafulila.
Kafulila
amefunguliwa kesi ya madai katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar
es Salaam na IPTL kwa kushirikiana na Kampuni ya Pan African
Power Solutions (T) Limited (mlalamikaji wa pili) na
Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hizo, Harbinder Sigh Seth
(mlalamikaji wa tatu).
Katika kesi hiyo namba 131 ya mwaka 2014,
walalamikaji kwa pamoja wanaiomba mahakama imwamuru mbunge
huyo awalipe fidia ya jumla ya Sh.bilioni 310 kwa madai ya
kutoa kashfa dhidi yao kwa kuwatuhumu kujipatia Fedha
kutoka Akaunti ya Escrow, kwa njia zisizo halali.
Siku Mahakama Kuu itakapotoa
uamuzi wa Kesi hii , ndipo tunafahamu Alichokuwa akikisema
Kafulila kuhusu kampuni ya IPTL Kuwa imepita Fedha Kwa njia
haramu hadi kusababisha Baraza la mawaziri kubadilishwa
kwasababu waziri mmoja alitimuliwa Kazi ambaye ni Profesa
Anna Tibaijuka na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini
,Professa Sospeter Muhongo ,Mwanasheri Mkuu wa Serikali Jaji
Fredrick Werema na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na
Madini Eliachim Maswi kusimamishwa kazi kwa kashfa ya
Escrow.
Muhongo Katika
hotuba yake ya kujiudhuru alisema anajiudhuru kwasababu ya
fitna, majungu, Chuki za kisiasa na wafanyabiashara ila
anaimani aliifanya Kazi yake kuitumikia taifa kwa uzalendo
wa Hali ya juu ni ukweli au uzushi. Ni suala la muda tu,
Tuipe Mahakama nafasi ifanyekazi yake.
Niitimishe kwa kukubaliana na Msemo wa msomi wa
Sheria Tundu Lissu na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
Kuwa Hakuna aliye maarufu kuliko Chama chao.
Lissu alikuwa akimaamisha
Zitto siyo maarufu kuliko Chadema na Msemo huo umethibitika
Kuwa ni kweli Zitto siyo maarufu kuliko Chadema Kwani tangu
walimpomvua Zitto Cheo cha Naibu Katibu Mkuu, Chama hicho
hakijafa na Katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa imeongezeka
idadi ya mitaa na vitongoji Kwa kupata ushindi.
Hivyo Zitto ambaye zaidi ya
makala zangu Tatu nilishakutaadhalisha Kuwa Umaarufu wako
umeporomoka kwa kasi ya ajabu na uamuzi huo wa Mahakama
Kuu ambao umeitupa Kesi yako Katika Hatua za awali kwasababu
ya makosa ya kiifundi wa Sheria ' Technicalities' ,
taarifa ya Chadema iliyotolewa kwa waandishi wa Habari
kupitia Mwanasheria wa Chadema kuwa.
Uamuzi wa Jaji Mziray umeipata tiketi Chadema
ya kutangaza Kumvua rasmi uanachama kwasababu moja ya
Ibara ya Katiba ya Chadema, inasema masuala yanayohusu chama
,mwanachama yoyote wa Chadema hataruhusiwa kwenda Mahakamani
kushitaki, na endapo mwanachama yoyote atafungua kesi
mahakamani basi Mwanachama Huyo Atakuwa amejifukuzisha
uanachama.
Na Kama Ibara ya
Katiba ya Chadema inasema hivyo basi Zitto Aliyataka
Mwenyewe kwa kuamua kuvunja Katiba ya Chama Chake na
kukimbilia
Mahakamani.
Pole Zitto uliipenda Chadema lakini Chadema na
Katiba Yao hawakutaki hata kukuona kwasababu ulivunja
Katiba ya Chadema. Lissu,Freeman Mbowe, Peter Kibara,
Dk.Slaa na wana wana Chadema wengine waliapa kuilinda
Katiba ya Chadema hivyo Hawakuwa Tayari kuiona Zitto na MTu
mwingine akiifunja Katiba ya Chadema halafu wasimchukilie
hatua.
Nakutakia kila
lakheri Zitto.Hiyo ndiyo Sheria imetumika kuitupa kesi
yako na Chadema kukuvua uanachama kwasababu umevunja
Katiba kama leo sheria ni mbovu minasema hata kama sheria
ni mbovu ndiyo sheria zilizopo tunataka wa tuziheshimuwa
.
Na sisi Wenyeji wa Mkoa
wa Kagera tunasemaga ' Sheria Timzano' , yaani
sheria siyo mchezo.
Zitto
umekuwa mahiri sana na mstari wa Mbele kushupalia wenzio
Wafukuzwe uwaziri, madaraka mbalimbali na kweli kupitia
Kauli zako na ripoti zako zimeumiza Wengi wakiwemo wakina
Profesa Muhongo, Profesa Anna Tibaijuka, William Ngeleja
,Eliachim Maswi ambaye alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati
,Mwanasheria Mkuu wa zamani Andrew Chenge na Mwanasheria
Mkuu aliyejidhuru kwa Sakata la Escrow ambalo ulililishia
Bango Kuwa kukusanya taarifa ambazo zingine zimetiwa
mashakama hadi sasa Jaji Fredrick Werema na wengine
Wengi.
Mbunge wa Mtera,
Livingstone Lusinde Katika mjadala wa Escrow Bungeni alisema
anashangazwa na ripoti ya PAC ambaye Mwenyekiti wake Zitto
imeshindwa kumtaja Zitto naye alipata mgao wa Escrow na
vielelezo akavitoa Bungeni na Mbunge wa Sengerema(CCM),
William Ngeleja naye hivi karibuni amenukuliwa akisema Zitto
naye alipokea Fedha za Escrow lakini cha ajabu hajajitaja
wala kuchukuliwa Hatua Kama wao.
Na baadhi ya walioumizwa na ripoti zako ambazo
wengine wanadai baadhi ya ripoti zako zimekuwa na nia
Mbaya dhidi Yao wamekuwa wakikulalimikia sana na Kusema
wakati ukifika na wewe utaadhibiwa na Mungu hapa hapa
Duniani.
Na kweli kwa tamko
la Jana la Chadema lilotolewa na Lissu ni wazi kabisa Mungu
amejibu Maombi ya watu wale ambao wanadai uliwahumiza kwa
uzushi na wengine sikufichi nikiwemo Mimi uamuzi wa Chadema
wa kukuvua uanachama umenifurahisha sana Kwani kupitia
makala zangu ikiwemo makala
Yangu ya Aprili
12 mwaka 2012 gazeti la Tanzania Daima lilichapisha makala
yangu iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho 'Zitto
Kabwe ,Mbona U msahaulifu?
Maudhui ya makala hiyo nilikuwa namuelezea
Zitto kumbe na yeye ni jamiii ile ya baadhi ya wanasiasa
wale wale wenye hulka za kinyang'au ambao wanakasumba ya
kuzungumza uongo mbele ya umma, ili umma uwapende na uamini
kuwa kiongozi huyo ni mtu safi na mtetezi wa wanyonge,ana
heshimu sheria na Katiba ya vyama vyao kumbe siyo kweli.
Ieleweke wazi hapo nyuma Zitto alipata bahati ya kupata
umaarufu ndani ya jamii kwa kile kilichoelezwa ni
mwanasiasa kijana ambaye ana misimamo thabiti na asiyeyumba
katika kile anachikiami.
Sisi waumini wa sheria tunasema tuhuma zitabaki
kuwa tuhuma hadi pale zitakapothibitika na mahakama au vikao
husika vya chama chake.Lakini kwa kuwa mungu ni mwema kadri
siku zinavyozidi kwenda mbele atazidi kutuonyesha kama kweli
Zitto ni mwanasiasa msafi ,mhadilifu kuliko wanasiasa
wenzake wanaotoka katika vyama mbalimbali vya siasa.
Na kweli utabili wangu huo
umetimia hivi karibuni Kamati Kuu ya Chadema, ikatangaza
kumvua nyadhifa zote ndani ya chama hicho kwa kile
kilichodaiwa kuwa wamebaini kuwa Zitto anakisaliti chama
chao.Hali iliyosababisha baadhi ya wanananchi kuanza
kumtazama tofauti Zitto.
Itakumbukwa kuwa Zitto alikuwa msatili wa mbele
kushinikiza baadhi ya watumishi wa serikali na viongozi
wakiwemo mawaziri na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wawajibishwe
kwa kile alichokuwa akikidai kuwa wameshindwa kutekeleza
majukumu yao na wengine wamekuwa wakikabiliwa na tuhuma
mbalimbali na kweli kuna mawaziri waliondolewa kwenye baraza
la mawaziri kwasababu ya tuhuma hizo zilizokuwa zikiibuliwa
na Zitto na mwisho wa siku zikaungwa mkono na wananchi.
Waswahili wanamsemo wao usemao
'linalomkuta Boko na Mamba pia litamkuta kwasababu wote
wanaishi majini'. Kwa hiyo yaliyowakuta baadhi ya
mawaziri kwa kuondolewa kwenye baraza la mawaziri kwa
kigezo cha tuhuma tu...ndicho ambacho kimemkuta Zitto
mwaka jana kwa Kamati Kuu ya chama chake kumvua nyadhifa
zake zote kwa tuhuma kuwa ni msaliti, na Jana Chama Chake
kumtimua rasmi uanachama.
Katika makala yangu iliyochapishwa Katika
Gazeti la Tanzania Daima Jumapili, Desemba 15 Mwaka 2013)
ilikuwa na kichwa ha Habari kisemacho ( ZITTO KABWE
UNAJIANDALIA ANGUKO) . Katika makala hiyo nilimuomba sana
Zitto aache tabia ya Kuzusha mambo yanayolitikisa taifa
wakati akaitwa na mamlaka husika anashindwa kutoa
ushahidi.
Niliandika makala
hiyo baada ya Zitto kushupalia Kuwa Una ushahidi wa Majina
ya baadhi ya viongozi walioficha mabilioni ya Fedha Kwenye
Akaunti nchini Uswiss Lakini aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa
Serikali ,Jaji Fredrick Werema alimuita ofisini kwake ale
kiapo na Kisha atoe hivyo vielelezo alivyonavyo ili serikali
Iweze kuchukua Hatua, Zitto alikuwa akimkwepa Jaji Werema na
alishindwa kutoa vielelezo hivyo na kuhesabika ni mtu Mzushi
na anayejitafutia Umaarufu wa kisiasa kwa kuchafua wenzie
kwa tuhuma za uzushi.
Gazeti la Tanzania Daima Jumapili toleo la
Novemba 28 mwaka 2011, ilikuwa na kichwa cha habari
kisemacho ;ZITTO AWALIPUA MAWAZIRI :ASEMA HAWAFANYIKAZI
,WANAWAUWAZA URAIS.
Lakini
Gazeti la Mwananchi Jumapili la Machi 25 mwaka 2012,
lilichapisha habari iliyokuwa na kichwa habari kisemacho
ZITTO: NITAGOMBEA URAIS 2015.
Leo kikowapi? Chadema imekupiga Ngumi za uso
kwa kukufukuza rasmi uanachama na umeshindwa kuzikwepa.
Mbona wale waliokuwa
wakikutumia ovyo ovyo HIvi sasa wamekutelekeza Jangwani
Unatakiwa na Jua hawakupi hata Maji ya Kunywa ili usife na
kiu?
Maana ulikuwa Hodari
sana wakushawishi na Kuzusha na kutaka wanasiasa wenzio na
watendaji wa serikali wachukuliwe Hatua ikiwemo kufukuzwa
Kazi.
Nimalizie kwa
kumwambia Zitto hivi, 'Muosha ,uwoshwa' tena wakati
wa kuoshwa ulipuliwa'. Sasa na wewe sasa umeoshwa maana
ulizoea kuosha wenzio.
Sasa
na wewe Zitto ulikuwa mahiri sana wa kuosha wenzio yaani
kuwafukuzisha kazi watu sasa na wewe jana Chadema kupitia
wanaume wasomi wa sheria yaani Lissu, Peter Kibatara na
Mallia wamekuingiza jando la wanaume la ukubwani siyo jando
lile la watoto wadogo wa Kiume.Hongereni Mawakili waliokuwa
wakiiwakilisha Chadema mahakamani Katika Kesi hii.
Na hiyo ni rasharasha, Mvua
kubwa Kama ile iliyonyesha kule Nzega ikasababisha taifa
kutikisika inakujia Katika medani ya siasa maana sikufichi
Zitto kaa utambue kuwa una maadui wengi na umeumiza baadhi
ya watu bila hatia .
Na
ukumbuke wale uliowaumiza nao wana Mungu na walikuwa
wakikishe wakisali kumuomba Mungu alipe kisasi kwa watesi
wao.
Nafikiri ulisahau kuwa
wale watu uliosababisha wakapoteza ajira zao kwa mdogo na
makelele yako na uzushi wako kuwa nao wana Mungu na Mungu
wao siyo kilema anayetembelea baiskeli ya walemavu yenye
miguu mitatu na ni kipofu.
Kwa taarifa yako Mungu wao ni Mungu mwenye Siha
nyema siyo kilema wala kipofu anaona na kusikia na anatembea
kwa kutumia miguu yake na ni kijana pia anafanyakazi zake
kisayansi na anatembea na IPAD iliyounganishwa Internate
anajibu maombi haraka ,amesikia kilio chao na sasa Mungu
ameanza kuwalibia kisasi kwako kupitia Mahakama na Chadema
ambapo kesi yako imetupwa na uanachama wa Chadema umevuliwa
kwahiyo hivi sasa siyo Mbunge mwanachama wa Chadema,na
umaarufu wako uliokuwa mao kipindi kile ulitokana na wewe
kwanza kuwa mwanachama wa Chadema na kisha majukumu mengine
ambayo uliwahi kuyafanya.
Na kwa uamuzi wa Chadema wa jana dhidi yako ni
wazi hata yale mawazo yako uliyoyatoa bungeni wakati
ulipomaliza kuwasilisha ripoti ya PAC kuhusu Escrow
ulivyosema eti umeimiss UKAWA, ifute mara moja kwani kwa
uamuzi wa Chadema wa kukuvua uanachama ,hawakutaki
usiwafuate fuate na UKAWA yako weendelea na ACT yako ambayo
siyo Mwanachama wa UKAWA.
Mwisho Niitimishe kwa kumtaka Zitto arejee
Msemo arejee Msemo usemao(Yaliyomkuta Mamba na Boko pia
yatamkuta kwasababu wote wanaishi Kwenye Maji.
Kwa maana kwamba yaliyowakuta
wanasiasa wenzake na viongozi wa serikali kwa kuvuliwa
madaraka makelele yake na yeye Jana yamemkuta kwa Kesi yake
kutupwa na kufukuzwa uanachama kwasababu na yeye pia yupo
Kwenye siasa na anaishi Duniani,usikasirike ,furahia Kwani
ni wakati wa Mungu sasa kukulipa kutokana na mambo uliyokuwa
unawafanyia wenzio wakaumia kwa namna yoyote ile.
Nakushauri nenda kafanye Kazi
za taaluma uliyosomea achana na siasa maana hadhi yako na
Umaarufu uliokuwa nao wakati upo Chadema haurudi tena.
Zitto siasa uliifanyia papara
na daima mwenye pupa hadiriki kula tamu kwasababu kwa umri
wako ikasababisha ukawachua wengine wanalazimisha kuaribiwa
mustakabali wa Maisha Yao kutokana na siasa zako za
kuwalipualipua watu,siasa zilizojaa utashi
binafsi,ubabe,Umaarufu wa haraka haraka Pasipo kuzingatia
Kuwa siasa ni Uwanja uliojaa kila aina ya Mabadiliko yasiyo
tabirika Kama Mabadiliko ya Hali ya hewa.
Sasa wewe hakutaka kukuubali
ukweli Kuwa siasa zile ulizokuwa unafanyia wenzio Je
ulitarajia na wewe yangekukuta kama yaliyowakuta wahanga wa
siasa zako Kama Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye Kutwa
ulikuwa unashinikiza Atukuzwe Kazi Kwani ameshindwa Kazi na
unakusanya saini ya kumng'oa bila mafanikio, Lowassa,
Ngeleja, Muhongo, Tibaijuka na wengine.
Vilio ,masikitiko na maombolezo Yao binafsi na
vya watu wao wa karibu dhidi yako hukunisikia Je Leo nani
atakufariji kwa yaliyokukuta ?
Ama kweli Leo yametimia Muosha Uwoshwa tena
wakati wa kuoshwa ulipuliwa.
Yaani yule
Muosha maiti kule Mochwari ipo siku nayeye ufariki Dunia na
maiti yake inaoshwa wana watu wengine.
kuwapungumza wenzio kwa Mabaya huku ukiwa
umeleta Katika Kiti cha Enzi ambayo wewe ulifikiri Enzi hiyo
haina mipaka wala mwisho kuwajenga hisia za Utawala wako
Kwenye hisia zako
Ukajenga nchi ya
kusadika yaani wewe ndiyo mtawala, na wala Ukawa siyo
msikivu ,hisia zako ndizo zikawa zinakutawala na kufanya
maamuzi ya Moja kwa Moja ya kuwathiri wale wote kwa
Bahati Mbaya Katika fani zao za Maisha wakawa ni wenye
kukutana na wewe Mithili ya kimbunga sasa na wewe Leo
Imefika siku yako.
Pengine
hili litakuwa nifundisho kwa wanasiasa vijana wenye hamu ya
kupata Umaarufu na utashi binafsi katika medani ya kisiasa
chini ya kisingizio cha uzalendo wa nchi hii Kumbe ni
wanafki na wao ni wachafu wanatuhumiwa kwa ufisadi.
Hukuwafaa Chadema, Chadema
ndiyo Chama Kikuu cha upinzani,Kama Zitto angelikuwa ni
Msafi na kwa hayo aliyokuwa anawaaminisha Watanzania Kuwa
yeye ni Mtetezi wa wanyonge na Mpenda haki kikweli kweli
basi Chadema wangemkumbatia na wasinge mfukuza uanachama.
Zitto akufaa Chadema ,ACT
mnatarajia atawafaa kwa lipi ? Watanzania Tujiulize sasa
Zitto alikuwa mbunge, Mwenyekiti wa kamati ya PAC, Naibu
Katibu Mkuu Chadema Kwani sasa vyeo vyote vimponyoke Mara
Moja wakati alikuwa akijitapa yeye ni Mpinga ufisadi na
anayeshimu Katiba ya Chadema?
Mfano mzuri leo hii nani atasikiliza nyimbo
zako na midundo yako ni sawa na miziki ya ilipendwa ambapo
miziki ya zilipendwa mtu usikilizwa wakati anataka
kujikumbuka enzi za muziki ule ulivyotamba lakini siyo
kama muziki mpya.
Historia itakukumbuka kwa mazuri na mabaya
yako utambukwa nayo, itakuwa ni vizuri zaidi ukapumzika
siasa wewe ni kijana msomi unafani yako ya uchumi ni ushauri
wa bure rudi nyumbani kwenu kazungumze na wazee wakupe
ushauri na wakuombee dua uende ukaanze Maisha katika Kazi
mpya isiyo ya kisiasa kwani siasa imeishakupa mkono wa
buriani. Buriani Zitto siasa kwa kheri.
Aidha Bendi ya Wananjenje ina wimbo wao maarufu
wa mduara unamaneno yafuatayo ( Boko wala wa wenziooo ,Tiii
....Boko nawe utaliwa weee) Sasa Zitto ulizoea kula vya
wenzio yaani kufukuzisha wenzio kazi na kuwapatia kadhia
kwenye majukumu yao sasa na wewe jana umeliwa yaani
namaanisha (Chadema) imekufuta uanachama na Mahakama Kuu
imetupa kesi yako.Naomba kutoa hoja.
Mungu ibariki Tanzania
Chanzo:
Facebook: Happy Katabazi
Blogg:
www.katabazihappy.blogspot.com
Machi 11
Mwaka 2015
0716 774494.
Sent from my iPad
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to
this Forum bears the sole responsibility for any legal
consequences of his or her postings, and hence statements
and facts must be presented responsibly. Your continued
membership signifies that you agree to this disclaimer and
pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message
because you are subscribed to the Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe
from this group and stop receiving emails from it, send an
email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment