Wednesday, 25 March 2015

Re: [wanabidii] Lowassa ana baraka za Kikwete?

Hawajakutana bara barani hawa-fullstop


From: Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Tuesday, March 24, 2015 6:06 AM
Subject: [wanabidii] Lowassa ana baraka za Kikwete?

Lowassa ana baraka za Kikwete?
Ilikuwa kama tetesi kuwa Lowassa anatarajia kuwania kiti cha urais kumrithi Kikwete baada ya muhula wake kuisha. Tetesi hizo zilisindikizwa na shughuli za harambee kuchangia maendeleo ya asasi za kidini, binafsi hata makundi kwenye jamii. Tetesi hizo ziliwaibua wasaka urais ambao walitaraji kupenyeza majina yao katika mchujo wa chama (CCM) wakati utakapowadia, lakini badala yake walikimbizana na tetesi hizo huku wakijinasibu kutaka kugombea urais 2015. Ikumbukwe kwamba Lowassa bado ni mtuhumiwa namba moja wa sakata la RICHMOND ambalo liliiangusha serikali Bungeni na kumlazimisha rais kuunda upya Baraza la Mawaziri.
Hatimaye walidhibitiwa kwa kuwekwa kiti-moto na hatimaye kufungiwa mwaka mmoja kuendeleza harakati zao huku wakiangaliwa nyendo zao. Ila washangiliaji hawajui ni nini hasa walichofungiwa maana kama kujitangaza walishajitangaza na pia wameendelea kufanya siasa za Chama bila kubugudhiwa na yeyote.
Hata kabla kifungo chao kuisha mzee wa Monduli ameibuka kwa kasi ya ajabu huku makundi ya kijamii yakitumika kushinikiza kukubalika kwake na akilazimishwa kuchukua fomu huku akichangiwa pesa ya ada ya kuchukua fomu ndani ya chama chake. Yamesemwa mengi ndani na nje ya Chama lakini washereheshaji hawajabaki nyuma kukebehi na kunasibu kuwa siyo Lowassa anayetaka kugombea bali ni wanachi....
Haya yote yanafanyika mbele ya Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi. Haya yanafanyika huku kanuni za kuhusu kutangaza nia na ratiba za kuchukua fomu hazikurekebishwa hivyo kuonyesha wazi ukiukwaji wake. Haya yanafanyika sambamba na kujitakasa kwa Lowassa tena kwa tambo nyingi kwamba kujiuzulu kwake kulikuwa kwa lazima ili kuokoa serikali isianguke yote. Na wapambe wake wanapita huku na huko wakisema kuwa 'BWANA MKUBWA' anahusika na "ishu" ile. Hakuna aliyesimama kukemea wala kutoa ufafanuzi wa propaganda zinazoenezwa mitaani. Haiyumkiniki sasa yametimia kuhusu ule usemi kwamba 'Uongo ukirudiwa rudiwa sanahugeuka ukweli'
Ninagoma na pia ninasita kuamini kwamba nguvu kubwa ya Lowassa inatokana na uswahiba alionao na mkuu wa nchi, kwani alishawahi kusema "...mimi na JK hatukukutana barabarani...." Inawezekana sana sisi wananchi tunazugwa kwamba hawa waheshimiwa hawapatani kumbe jioni wanakunywa kahawa pamoja, inawezekana kabisa kwamba Lowassa ndiye chaguo la Kikwete kurithi kile kiti pale magogoni.
Nasema hayo kwa sababu, hatujaona JK kukerwa na tambo, harakati na hatimaye propaganda za kambi ya Lowassa hasa zinapopambamoto kipindi hiki kuelekea uteuzi wa ndani ya Chama na hatimaye Uchaguzi mkuu hapo Oktoba. Chama cha CCM kinaweza kuungana ama kugawanyika kwa kiwango cha kutisha kupitia uteuzi wa mgombea wa Urais mwaka huu.
Kazi kwenu Wananchi kumkubali mteule wa JK au kumchagua mtu makini ambaye hajatumia kununua umaarufu ili apewe nafasi ya kuwa rais wetu baada ya JK.
Bila CCM imara, nchi itayumba. - By Nyerere
Leo nchi inayumba....
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


0 comments:

Post a Comment