Dkt; Muhammed Seif Khatibu:
Nakubaliana nawe kwa 100% kuwa uasi ameumbiwa binadamu, lakini uasi ni nini hasa? Sijaelewa pale uliposema uasi ni kinyume na utii, na binadamuimaumbile, kitabia, kiakili ni muasi anapenda kuafanya kila alitakalo bila kizuizi. Yawezekana napata shida kukuelewa kwa vile tunaishi sayari mbili tofauti kielimu, wewe ni dkt wakati mimi nina elimu ya "ualimu pasipo elimu (UPE)". Naomba univumilie kwa kutoelewa kwangu.
Sikuja kuwa kuanzisha vyama mbadala baada yabunge kutunga sheria kuruhusu jambo hilo. Hayati mwalimu Nyererealiwahi kusema kuwa "wapo walipewa madaraka na yamewalevya", nadhani wewe ni mmoja wao. Wewe na wengine wa aina yako mnadhani mnaweza kufikiri kwa niaba ya wengine, na kuwaambia lolote watanzania wakawapigia makofi, Mungu atakuwa alifanya kosa kujaza ubongo kwenye vichwa vyetu la sivyo angeweka makamasi.
Muhammed, mtu akifiri tofauti na wewe ni muasi? Akimuita mwizi aliyetengeneza mkataba wa kuiba pesa za umma kiudanganyifu ni muasi? Hakika dunia ingegeuka pepo kama kufikiri angeachiwa mtu mmoja au kikundi kidogo tu kwa niaba ya wengine wote. Ingekuwa pepo kwa sabau hapangekuwa na wa kuhoji analosema bwana mkubwa anayechukua kodi zaopasi kuulizwa amezitumiaje (Mungu huyu).
Binadamu aliyelewa madaraka hataki kuulizwa na mtawaliwa, hataki kuona mtawaliwa anafikiria kujikomboa. Kama ilivyokuwa kwa wakoloni weupe ndivyo ilivyo kwa watawala weusi. Wakoloni weupe wlitunyonya na kupeleka mali zetukwao ulaya, wakoloni weusi waliojitolea kuwafukuza wakoloni weupe wanaiba mali za Afrika na kuwapelekea mabwana zao wakoloni weupe. Hawa ndiyo wale wanaodhani kutofautiana nao kimawazo ni uasi, hawa ndiyo kina Muhammed Khatibu.
Walioanzisha vyama mbadala ni waasi kwa vile sheria ile ilikusudiwa kuona vyama vya upinzani vinaundwa na mawe, mbweha, simba, chui, pundamilia na wanyama wengine aliotujalia Mungu kwenye mbuga zetu au wageni toka ulaya na si watanzania. Wakati sheria ile inatungwa Khatibu alikuwamo bungeni lakini leo anaibeza sheria aliyoshiriki kuitunga na kuwaita wanufaika wa sheria ile waasi! Huu ni ulevi uliopindukia, hata sultani aliwaita hivyo wana-ASP, muingereza aliwaita hivyowana TANU, leo sultani mweusi anawaita hivyo walioanzisha vyama vingine kupinga uovu unaofanywa na makaburu weusi. Hawa ndiyo waliolewa utajiri waliotuibia hadi kufikia kuita Bilioni nivijisenti, milioni kumi hela ya mboga isiyofaa kuhojiwa ilivyotumika.
Kwa kukumbusha Khatibu, hata tulipokuwa tunatafuta uhuru tulikuwa na vyama vingi, hata tulipopata uhuru tulikuwa na vyama vingi (znp, zpp, zppp, nk). Hofu ya kutokuwa tayari kuhojiwa na wenye mawazo tofauti ndiyo ilitulazimisha kufuta vyama vingine na kubaki nachama kimoja.
Tuwanyamazie hawa wanaosaka madaraka kwa damu ya ndugu zetu zeruzeru.Tuhuma hizi za damu ya watu ni nzito lakini hazina uzito kwa viongozi wetu wasiotaka kuulizwa lolote na yeyote. Hakuna anayesema kwa kuwa wanajuana wanakopita kusaka madaraka kwa vigagura.
Tuvumiliane tulikubali wenyewe
From: 'Muhammedkhatib' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Sunday, March 1, 2015 10:41 PM
Subject: [wanabidii] Fwd: UASI.
Subject: UASI.
UASI.
(Dkt.Muhammed Seif Khatib)
Uasi ni kinyume na utii.Binadamu kimaumbile ya kitabia ni mwasi.Maumbile yake,akili yake na maarifa yake anapenda kufanya kila alitakalo bila ya
kizuizi.Binadamu ni mnyama na dunia ni msitu.Mwenye nguvu hutenda atakalo
na alipendalo.Kama alivyo simba na chui katika mbuga hufanya kila alitakalo
ndivyo ilivyo kwa binadamu katika dunia.Wenye nguvu huwaonea wadhaifu. Hilo silo geni kwa viumbe wa majini samaki mkubwa humeza mdogo. Hata katika ulimwengu mataifa yenye nguvu za kiuchumi, kijeshi na kiteknolojia kinachotokea ni kuzivamia dola dhaifu na
kuzichapa.Dunia ya sasa mwanadamu ameunda vyombo vya kimabavu ili amuadhibu yule
anaye asi na asiyetii. Hivi jela kazi yake nini? Polisi anamtumikia nani? Mahakama ipo
kwaajili ya nani?Jeshi na zana zake kwaajili ya nani? Wakuu wa Mahakama, Jela,
Polisi na Jeshi anayeteua nani? Uliwahi wapi kusikia kuwa viongozi hawa wanachaguliwa
kwa kura?Vyombo na viongozi wake wanatumikia watu maalumu.Nia kuu kuwaadhibu wale
wanaoasi.Wale wasiotii.Uasi hakunza leo na jana au juzi. Dunia inaumbwa zaidi ya miaka
4.5 Billioni miaka binadamu amekuwa asi.Waumini wa dini wanazo kanuni za kuwafanya
wawe watii.Dini zimeteremshwa kuudhibiti uasi.Dini ya Kiristo iliyoasisiwa na Issa zaidi ya
miaka 300 iliyopita imekuja kuuvunja uasi wa binadamu.Kitabu chake Bibilia mandiko
yake juu ya upendo na utii.Yesu au Issa aliifanya kazi hiyo kwa kutoa hoja za kutosha lakini
binadamu muasi hakumuamini na shaka sulubu.Kitabu cha Biblia kikawa mwongozo.Makanisa yakawa majengo ya kuabudu na Jumapili ni siku ya ibada. Dini hii
yenye wafuasi billioni mbili imeenea ulaya,Amerika na Afrika.Sina hakika waumini wake
wote hawa ni watii na si asi.Ukiristo ulitanguliwa Judism huko Palastine miaka 1800 kabla
ya kuzaliwa Yesu.Dini hii yenye wafuasi 14 millioni mwasisi wake ni Musa.Ibada zao huwa
katika mahekalu. Ni dini ya zamani yenye malengo ya kuvunja uasi wa binadamu.Kwa kiasi
gani waumini wake ni watii? Karne ya saba huko Saudia katika mji wa Makka Muhammad
akazaliwa.Kwa kutumia kitabu cha Koran kwa sa miaka kumi na mbil akatangaza
na kueneza Uisilamu..Kwa kutumia Koran, viongozi wa dini maimamu na muadhini wafuasi
wakafika sasa billioni 1.5 duniani wanatakiwa wasiasi.Waisilamu siku kuu ya Ibada ni
Ijumaa. Wafuasi Judism ni Jumamosi na Wakristo ni Jumapili. Kwa kiasi gani siku hizi za
ibada kwa kila dini zimesaidia binadamu asi asi? Musa ni Hebrew, Muhammad ni Mwarabu
na Yesu ni Yahudi wote kutoka Mashariki ya Kati.Jee makabila yao na maeneo ya uasisi
wa dini hizo hakuna uasi? Waisilamu wamemegeka kati ya Suni na Shia. Uhusiano wao
ni mbaya ingawa wanaamini Mungu Mmoja,Nabii mmoja na kitabu kimoja.Nao wamekiasi
kitabu chao. Wakristo wanaamini Yesu na Biblia lakini madhebu yapo mengi.Kila kukicha
makanisa yanazuka,Manabii,Mitume na Miungu inatokea na kuhubiri biblia. Huu siyo uasi
kitabu na Yesu. Waisilamu kwa Waisilamu wanauwana na kuchinjana kila kukicha. Wakristo kwa Wakristo wanauwana. Waisilamu wanawachukia Wakristo. Wakristo
hawawataki wa Waisilamu. Utukufu wa dini zao za kuonesha upendo na amani uwapi?
Mwenendo wa mazuri wa Yesu, Muhammad na Mussa haufatwi.Huko Arabuni katika
chimbuko za dini hizi kubwa imekuwa leo uwanja wa mauaji.Binadamu ni asi.Waumini ni asi.
Viongozi wa dini ni asi. Zawadi walioahidiwa binadamu katika vitabu vyao vya dini kupewa
baada ya kufanya mema hapa duniani baada ya mauko yao watazikosa. Hilo wanalijua.
Adhabu watakapewa kwa kuasi hapa duniani waumini wanazitambua. Lakini bado wanaoasi.Mwaka 1992 vyama vya siasa vya upinzani vikaruhusiwa nchini.Kwa vile
binadamu ni asi haikuchukua muda vyama vikajitokeza na kubeba bango la uasi kwa
jina la upinzani. Wote viongozi wa vyama vya upinzani walikuwa ndani ya chamatawala.
Chama kilichowakomboa.Chama kilichowaletea Mapinduzi. Chama kilichowarejeshea
heshima ya utu wao. Chama kilichoanza safari ndefu ya kuwaletea maendeleo katika
maisha yao. Lakini kwa vile binadamu kwa hulka,silka na tabia ni asi, macho yao yakawa
kama yanatongotongo hayaoni. Masikio yakapata komango yakawa hayasikii.Lakini
midomo yao ikapata nguvu ya kuponda kila kitu kilichofanywa na chama tawala.Hali hii
inaendelea hadi leo. Kama binadamu ameweza kuwa asi kwa dini zao, vitabu vyao, mitume
yao na Mungu wao siuze itakuwa kuasi Chama Cha Mapinduzi? Kama binadamu ni asi
kwa mamlaka inayotawala na haogopi jela,mahakama,polisi,jeshi na vyombo vya utawala
atachelea kukiasi Chama Cha Mapinduzi?Uasi umo ndani ya damu na mishipa ya binadamu.Chama Tawala kifanye wajibu wake na kitambuwe upinzani wa siasa ndani
ya Tanzania ni sehemu ya UASI wa binadamu.Chambilecho Waswhili husema ' Kelele za
Mpangaji hazimzuii Mwenye Nyumba kulala '
K
Sent from my iPad
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment