Wednesday 12 October 2016

[wanabidii] VIJANA WAHIMIZWA KUJISHUGHULISHA KULETA TIJA

Habari za asubuhi,

Tafadhali pokea CODES hapa chini.

TABIA ya vijana kutojishughulisha katika miradi mbalimbali yenye tija kumeeelezwa kuwa moja ya vyanzo vya kudorora kwa uchumi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama katika ufunguzi wa kongamano la kitaifa la vijana lililofanyika katika ukumbi wa shule ya msingi Allience Mjini Bariadi.

Alisema kumeanza kujitokeza hali ambapo vijana nchini kutokupenda kujishughulisha katika miradi mbalimbali ya kiuchumi na hivyo kushindwa kuondokana na umaskini na pia kuchangia katika pato la taifa.

Alisema kuwa vijana wanaongoza kwa idadi kubwa lakini wanashindwa kujishughulisha kuhakikisha wanapata maendeleo ambayo yanaweza kulisaidia taifa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida (kushoto) akisalimiana na mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama (kulia) alipowasili katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi kufungua kongamano la vijana.

Mhagama alisema katika Kongamano hilo ambalo limeandaliwa na Mkoa wa Simiyu, kuratibiwa na Taasisi ya utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kwamba kuna fursa nyingi lakini vijana wanakuwa wagumu kuzichangamkia na matokeo yake kubaki wakiilalamika serikali kuwa haiwajali.

Alibainisha kuwa serikali itaendelea kusaidia makundi ya vijana yanaoonesha nia ya kujiendeleza

Aidha alifafanua kuwa itawaongezea mtaji wa shilingi milioni 30 kwa kikundi cha vijana cwalioanzisha kiwanda Maziwa cha Meatu pamoja na kile cha Chaki kutokana na jitihada zao walizofanya na matunda kuonekana.

Awali kabla ya kumkaribisha mgeni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka alisema lengo la serikali mkoani hapa ni kuhakikisha linainua pato la mkoa na kuchangia katika pato la taifa kwa kuwawezesha vijana wake kutengeneza bidhaa zinazotokana na malighafi zinazozalishwa mkoani hapa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama na Naibu wake Mh. Anthony Mavunde wakisalimiana na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na ESRF mara baada ya kuwasili kwenye kongamano la kitaifa la vijana lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.

Alisema zaidi kwamba wanalengo la kuhakikisha mkoa unaingia katika tano bora ya uchangiaji wa pato la taifa.

Amehimiza viongozi kuwasaidia vijana kuwaongoza, kuwaelekeza na amewataka vijana kuwa na uthubutu na kuungana kwa pamoja.

Pamoja na harakati za kiuchumi vijana wametakiwa kuwa na mwendo wenye maadili mema ili kuendelea kuwa na afya bora na kukwepa magonjwa yanatokanayo na ukosefu wa maadili.

Amesistiza kuwa kauli mbiu waliyoanzisha ya "Bidhaa moja,wilaya moja" itumike ipasavyo ili kufanikisha maendeleo yao na ya wilaya.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama akitoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano la vijana Simiyu lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida alisema ushiriki wa vijana katika viwanda vidogovidogo kunaweza kukuza uchumi kutokana na viwanda hivyo kutoa ajira na pia kutengeneza mnyororo wa thamani katika mazao ya wakulima ambako vijana ndiko wanakotarajiwa kuonesha ushujaa wao.

Hata hivyo alisema ukuaji wa uchumi kwa sasa bado ni changamoto kwa wananchi wanaoishi vijijini kutokana na baadhi ya huduma kutowafikia kwani asilimia 7 inayopanda kiuchumi huwa haitafsiriki kufikia makundi yote ya kijamii .

"Tumekuwa tukiendesha tafiti nyingi lakini tunaona kipato chetu kinaendelea kushuka hasa katika wananchi wanaoishi vijijini hivyo kuwepo kwa viwanda kutaweza kuwainua kiuchumi wananchi kutokana na bidhaa zao ghafi kuuzwa katika viwanda"Alisema Dk. Kida.

Nao wafadhili wa Kongamano hilo UNDP wamesema wametenga fedha kwa ajili ya kuwasaidia vijana katika programu zao za maendeleo.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akizungumza machache awali kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama kufungua kongamano la kitaifa la vijana lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.

Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Vijana, Wazee, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Moudline Castico akitoa salamu kwa vijana kutoka visiwani Zanzibari kwenye kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.

Meza kuu mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama, Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Vijana, Wazee, Wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Moudline Castico (wa tatu kulia), Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Dk.Titus Kamani ( wa pili kulia), Mkuu wa Programu, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama (kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida (kushoto), Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Anthony Mavunde (wa pili kushoto) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (wa tatu kushoto).

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya kuondoa Umaskini wa Wizara ya Fedha na Mpiango, Mudith Cheyo (kulia) na Naibu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Wizara ya Fedha na Mipango, Maduka Kessy wakifuatilia hotuba mbalimbali wakati wa kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.

Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida akiwasilisha mada ya mageuzi ya kiuchumi yanayohitajika kuboresha maisha ya vijana pamoja na hali ya uchumi nchini kwa makundi ya vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini walioshiriki kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.

Bw. Abdallah Hassan (kushoto) na John Kajiba wa ESRF wakifuatilia jambo kwenye kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.

Mkuu wa Programu, Shirika la Maendeleo UNDP, Amon Manyama akizungumzia mchango wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN/UNDP) katika Maendeleo Endelevu ya Vijana wakati wa kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.

Sehemu ya umati wa vijana na wageni waalikwa waliohudhuria kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.

Naibu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Wizara ya Fedha na Mipango, Maduka Kessy akiwasilisha mada ya fursa za vijana katika uchumi wa viwanda pamoja na Mpango wa pili wa Maendeleo wa miaka mitano 2016/17-2020/21 kwenye kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.

Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ufundi Stadi-VETA Leah Dotto akiwasilisha mada iliyozungumzia mchango wa elimu ya ufundi stadi katika kufikia Tanzania ya viwanda katika kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.

Afisa Mwandamizi wa Idara ya Maarifa na Ubunifu wa ESRF, Abdallah Hassan akizungumzia fursa mpya ya kilimo biashara kwenye kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.

Pichani juu na chini washiriki wakiuliza maswali kwa wakufunzi na viongozi wa serikali katika kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.

Pichani juu na chini ni umati wa makundi ya vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Vyuo Vikuu waliohudhuria kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.

Mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama na Naibu wake, Mh. Anthony Mavunde katika picha ya pamoja na mdhamini mkuu wa kongamano hilo UNDP, waratibu ESRF pamoja na wawasilishaji mada kwenye kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.

Mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka katika picha ya pamoja na wawasilishaji mada, ESRF pamoja na UNDP kwenye mabango ya viwanda vilivyoanzishwa na vijana cha Meatu Milk na kiwanda cha kwanza Tanzania cha kutengeneza Chaki cha mkoani Simiyu

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Anthony Mavunde wakimtunza mwanakikundi wa ngoma za asili cha Wanaisanga kutoka Maswa mwenye uzoefu wa kucheza na Chatu wakati wa burudani kwenye kongamano la vijana Simiyu lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.

Mwanakikundi wa ngoma za asili Wanaisanga kutoka Maswa mwenye uzoefu wa kucheza na Chatu akionyesha umahiri wake wa kucheza na chatu kwenye kongamano la vijana Simiyu lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.

Kutoka kulia ni Naibu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Wizara ya Fedha na Mipango, Maduka Kessy, Mkuu wa Programu, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama, Mtafiti Mshiriki ESRF, Dr. Oswald Mashindano, Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dr. Tausi Kida, Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu ESRF, Margareth Nzuki wakifurahi burudani ya ngoma za asili ya kucheza na Chatu wakati wa kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.

Wageni waalikwa wakiendelea kufurahi burudani ya ngoma za asili kwenye kongamano la vijana Simiyu.

Zainul A. Mzige,
Operation Manager,
MO BLOG,
+255714940992.

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment