Thursday, 20 October 2016

[wanabidii] Re: [Wanazuoni] Museveni Analipenda Ua La Boga( Winnie), Analichukia Boga ( Besigye)...!

Mwenyekiti Maggid,

Leo nilihudhuria mhadhara pale SOMA Professor Coulson ameomba kama kuna Mtanzania aweza tusaidia basi kutafsiri kwa Kiswahili kitabu chake Tanzania: A Political Economy yupo tayari kushirikiana nae kwa gharama ndogo sana awe tayari tu kusoma ABC za nadharia ya siasa uchumi aka political economy. Binafsi nasikia vibaya sana kuona uko busy na mambo haya ya akina M7, KB na Winnie, duh na Kalinaki hapa umemweka pia, safi. Ila mie sijui mambo yanayotusonga hapa mengi Tanzania, tuna GMOs debate hapa, tuna masuala ya sera hapa mambo ya ardhi nk tunakaribia badilisha, na kilimo chetu kipo njia panda, ama wewe ukipitia yale ma tikiti maji, nyanya waona poa kuyapata yalivyo?na waweza dai lumbesa pia ukaijaza ile cruza yako! Hivi Wanazuoni sawa labda tungependa hizo story za namna hiyo wanasiasa wetu hawa nani hafanyi hiyo mambo....juzi Magufuli alivyotaja rafiki yake hapa yakazuka maneno, kwa nini kasema hivyo mkweli naye yale yale ama? haya ya kawaida sana kwingineko, hivi hakuna ile dhana ya moving on? 

Niseme kitu kimoja nimekisoma facebook  mtu hajasoma hata Sowing the Mustard Seed lol wewe kipanga wake unajua mambo kibao, mara Kalinaki hahahaha wewe hatari,  leo hii hata Coulson mwenyewe kapewa makavu  ingawa ni mjadala wa reflection yangu si hapa baadae.  Bahati nzuri wewe unatafsiri tu ingawa hata husemi authors na mitizamo yao na limitations na wewe unaweka pia hisia na tafsiri zako pia, ambayo si sahihi na hata waandishi wote hao kwasababu wanaandika matukio yanayohusu watu hai inakuwa ishu. Majuzi nilisema kwasababu ya baadhi ya maeneo ya Sowing the Mustard Seed kitabu kinahitaji reviews, na wadau wengine wali launch version kupinga baadhi ya stories, kazi sasa ukiwatafsiria wabongo hapa na hata hayo wayasema ni sahihi si sahihi kwanini usishangiliwe?

Baada ya hapa  naomba niendelee kuku udhi kuna mengi Uganda ungeweza tuletea basi ya manufaa sip haya ninayoyasoma hapa. Ok tutajadili nini? M7, KB, Winnie? M7 anamwonea KB kisa girl friend? khaaaaa....nina jamaa nilitambulishwa baadae nikaambiwa aaaah wale wale, aliwahi sema ati hamna ishu ya ku debate hawa ugomvi wao ni mwanamke! Hivi ndio unataka kutwambia pia hapa na kutuaminisha? hii sio insult kwa harakati za siasa na demokrasia Uganda? na kutuaminisha kwamba siasa za Uganda zipo hivyo na hakuna mambo ya msingi kabisa ya kudai haki na kwamba yes wakati wa uchaguzi mambo yalikuwa ndivyo sivyo?

Niseme mawili ukileta Wanazuoni bila shaka unatarajia tusome, tufurahi na labda tukasirike pia, huu mjadala dhaifu sana kwa viwango na uelewa na utendaji kazi wako Mwenyekiti Maggid....Maggid una mambo ya muhimu ya nchi kutushirikisha sio haya labda kwingineko yafaa naambiwa blog nayo ni business siku hizi?Sasa wewe wapost uliyosoma kuna walioishi na M7, Winnie, KB na wanajua hizo story more than you know ila wewe hapa watulisha sie wa Tz?  Yawezekana kusema Baha achana na hizi story na wewe post za kwako basi....YES ninazo na ni tofauti na version yako lakini je ni sahihi?

Tunapita kipindi kigumu, labda katika historia yetu, haya tayari tuna habari ya kuanza kuandikia, LGF atatuanzia alinikimbia wakati najiandaa kwenda kumpa HI, nilimwona kaunta pale SOMA ila sikukiona kinywaji halisi alikuwa anapata! Hahahahahahahah. Kulikuwa na stori ya uandike ukiwa na hasira ama ukiwa sober....nadhani Professor Adolf Mascarenhas alikuwa sahihi andika ukiwa na hasira. Na hasira zangu ni Maggid ana mengi ya kutufaidisha sio haya anayotupa hapa, sina taabu kwingineko ila kwa kariba ya Zuoni sidhani kama tunataka ku debate maamuzi ya watu wazima kisa kwa sababu ni wanasiasa. Tujadili sera zao yatosha labda? na kama maisha yao binafsi yanaathiri utendaji na lazima iwe public sawa yawekwe hadharani.

B.BFrom: "Maggid Mjengwa mjengwamaggid@gmail.com [Wanazuoni]" <Wanazuoni@yahoogroups.com>
To: mabadilikotanzania <mabadilikotanzania@googlegroups.com>; Wanazuoni@yahoogroups.com; wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Thursday, October 20, 2016 10:02 PM
Subject: [Wanazuoni] Museveni Analipenda Ua La Boga( Winnie), Analichukia Boga ( Besigye)...!

 
Ndugu zangu, 
Mvuto kwenye kisa cha Yoweri , Winnie na Kiiza unatokana na ukweli, kuwa Yoweri Museveni hakuitarajia adhabu ya yeye ' kulisaliti' pendo la Winnie kwake iwe kwa Winnie kutembea na Kizza Besigye, rafiki wa zamani wa Yoweri Museveni.
Juzi tuliona jinsi Winnie alivyoingia kwenye maisha ya Museveni.
Kiukweli, Museveni wa sasa bado anaonyesha kumpenda Winnie, lakini... Soma zaidi..
__._,_.___

Posted by: Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
Reply via web post Reply to sender Reply to group Start a New Topic Messages in this topic (1)

Have you tried the highest rated email app?
With 4.5 stars in iTunes, the Yahoo Mail app is the highest rated email app on the market. What are you waiting for? Now you can access all your inboxes (Gmail, Outlook, AOL and more) in one place. Never delete an email again with 1000GB of free cloud storage.


.

__,_._,___


0 comments:

Post a Comment