Sunday 2 October 2016

[wanabidii] MOTO UMEUNGUZA MASHAMBA NA MAKAZI KIMBIJI ,WILAYA KIGAMBONI SIKU YA KUPANDA MITI

MOTO UMEUNGUZA MASHAMBA NA MAKAZI KIMBIJI ,WILAYA KIGAMBONI SIKU YA KUPANDA MITI


Tukio la uzuni na majonzi la kuunguzwa makazi na mazao limewapata wakazi na wamiliki wa maeneo ya ardhi katika Kata ya Kimbiji mtaa wa Ngobanya wilaya Kigamboni,mkoa wa Dar-es-salam siku ya tarehe 1 Oktoba 2016 baada ya watu wasio julikana kuchoma moto
uliosababisha kuungua kwa mazao na miti pamoja na makazi kule Kimbiji-Ngobanya, wilaya Kigamboni,mojawapo ya mashamba yalioungua lilikuwa na miti aina ya mitiki 140 na nyumba
ndogo ambayo ni makazi,moto huo ulizuka mchana wakati wenyewe waliustukia tu na uwenda
umesababishwa na watu wenye vitendo vya kuchoma moto maneo ,taarifa za moto huo zililipotiwa kwa viongozi wa kata hiyo ya Kimbiji akiwemo mwenyekiti wa serikali za mtaa wa
Ngobanya bwana Ismail Mahembe kwa taarifa zaidi simu 0713846688

0 comments:

Post a Comment