Tuesday, 4 October 2016

Re: [wanabidii] Chadema yatenga mamilioni kummaliza Prof. Lipumba. Wamuhofia kuvuruga mpango wao wa kuimeza CUF

Lusinde kumbe alikuwa anatoa unabii bungeni????? Kuwa chama kikishindwa mara tatu kinageuka chama cha kigaidi. Inawezekana wapi chama kama CHADEMA kuanza kuwa msemaji wa CYF kana tunavuoona na sasa tuhuma za kutumia fedha ili tu chama fulani kidhoofike. Mpango wao ukifanikiwa huenda vyama viwili vikafa yaani CUF na CHADEMA. No problem. Tutaanza upya.
--------------------------------------------
On Tue, 10/4/16, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Chadema yatenga mamilioni kummaliza Prof. Lipumba. Wamuhofia kuvuruga mpango wao wa kuimeza CUF
To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Tuesday, October 4, 2016, 8:22 PM

CHAMA cha
demokrasia na maendeleo (chadema), kimeelezwa kutenga
mamilioni ya shilling kwa lengo mahususi la kummaliza
kisiasa mwenyekiti
wa Cuf, Profesa Ibrahim Lipumba.Habari za uhakika kutoka vyanzo kadhaa vya taarifa hivi
zinabainisha
wazi chadema kutenga mamilioni hayo kwa lengo la
kuhahikisha, pamoja na
mambo mengine Profesa halejei katika uongozi wa juu wa
Cuf.Kwa mujibu wa taarifa hizo, hofu kuu ya chadema kwa profesa
Lipumba
iwapo ikatokea akarejea kwenye nafasi yake ya mwenyekiti, ni
kuvurugika
kwa mpango wao kabambe wa wa kuimeza CUF, ambao ulianza
kuratibiwa kwa
mafanikio na aliyekuwa mgombea urais wao katika uchaguzi wa
mwaka wa
jana, Edward Lowassa.Mpango huo mpya wa kuimeza Cuf, chadema yenye nguvu ya
kisiasa kwa
upande wa Tanzania Bara na ilikuwa na mpango wa kuunganisha
nguvu za
kisiasa za chama hicho kwa upande wa Zanzibar ili
ikiwezekana, kufikia
mwaka 2020 vyama hivyo viwe vimeungana na kuwa chama
kimoja.Mpango huo mpya ulilenga kuunganisha umaarufu wa wanasiasa
kisiasa wa
wanasiasa wawili pande mbili za muungano, Edward Lowassa na
Maalim Seif
Sharif Hamad, ili kukiwezesha chadema kukamata dola katika
pande zote
mbili za muungano 2020.Hata hivyo hatua ya sasa kurejea profesa Lipumba kutaka
kurejea kwenye
uongozi wa CUF na kwa sababu ya kulindwa nakatiba ya chama
hicho, huku
pia msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi,
akionekana
kubariki hatua hiyo, imezidi kuuchanganya uongozi wa juu wa
chadema,
hali iliyowalazimu kutenga mamilioni ya shilling katika
kuhakikisha kuwa
suala hilo haliwezekani.Mbali na kutenga fedha hizo zinazodaiwa kutoka kwa wale
wanaoitwa
marafiki wa Lowassa ili kummaliza kisiasa profesa Lipumba,
uongozi wa
chadema unadaiwa kujipanga kutumia kila aina ya silaha,
ikiwemo vyombo
vya habari na baadhi ya wasomi nchi kumdhalilisha Profesa
Lipumba ili
aonekana hafai machoni mwa jamii ya kitanzania.Hata hivyo, pamoja na mikakati hiyo ya chadema kummaliza
kisiasa Profesa
Lipumba, kambi ya mwanasiasa huyo, ambayo tayari inakalia
ofisi ya kuu
ya Buguruni, Dar es Salam, imeapa kupambana hadi mwisho,
huku ikiweka
bayana "daima haki itashinda".Kwa mujibu wa kambi ya Profesa Lipumba mgogoro wa sasa ni
baina ya kundi
la waasi nan a wavunjaji wa katiba wakiongozwa na katibu
mkuu Maalim
Seif Sharif Hamadi na kundi la watetezi, walinzi na walinzi
wa katiba ya
chama hicho wakiongozwa na Profesa Lipumba.Kutokana na hali hiyo kundi la Profesa Lipumba linasema wazi
kwamba hata
kama uongozi wa chadema utaamua kukusanya mamilioni ya
shilingi kwa
ajili kwa ajili ya kufadhili kundi la la waasi linaloongozwa
na Maarif
Seif Sharifu Hamadi, ni wazi fedha hizo zitateketea bure kwa
maelezo
kuwa hakuna mahala popote duniani ambako dhulma
ikashinda.Afisa mmoja wa Cuf, aliyeko kambi ya Profesa Lipumba, Abdul
Kambaya,
amekiri kufahamu mpango huo wa chadema kutenga mamilioni ya
shilingi kwa
ajili ya kummaliza mwenyekiti wao, ikiwa ni pamoja
kuhakikisha harejei
tena kwenye uongozi wa juu wa chama hicho."Tunafahamu sana kundi la maarim Seif linaendeshwa na
chadema na wao
ndio wanaoamua cha kufanya. Tunafahamu chadema wametenga
fedha nyingi
sana kwa ajili ya kuhahikisha profesa Lipumba harejei kwenye
uongozi wa
juu wa Cuf, lakini niwahakikishie daima haki itashinda
dhulma tu"
anasema Kambaya na kuongeza"sisi tupo ofisini, wao wapo msituni. Hii ni vita kati ya
watetezi wa
katiba, hivyo basi kamwe hawaezi kushinda vita hii, na ndio
maana
Profesa Lipumba anaendelea na majukumu yakle ya kukisuka
upya chama
chetu, huku wao wakihangaika huko nje, wakidhani Chadema
itawasaidia.Chanzo Tazama
 --

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment