Two wrongs don't make it right, mind you
Deo Gratius
On 6 Aug 2015 23:37, 'Saed Kubenea' via Mabadiliko Forum <mabadilikotanzania@googlegroups.com> wrote:
Mbona hata Mpendazoe alikuwa CCM? Alianzisha chama na kikamshinda?KubeOn Thursday, 6 August 2015, 21:23, 'ananilea nkya' via Mabadiliko Forum <mabadilikotanzania@googlegroups.com> wrote:
Lowassa tusamehe tuliokuhukumu, nikiwamo mimi--
Fred Mpendazoe kwenye gazeti la Raia mwema toleo la 417
la tarehe 5 Aug 2015 kaandika hivi:
NIMEONA ni vema niandike makala hii baada ya kupigiwa simu nyingi sana na wasomaji wa Raia Mwema baada ya Edward Lowassa kuhamia Chadema. Wengi wameomba maoni yangu na wengine uchambuzi.
Katika makala hii mimi nitaeleza maoni yangu tu. Nilikuwa nimeanza kuandika makala juu ya tabia ya unafiki ya wana CCM ambao kila mara hunukuu maandiko kadhaa ya Hayati Mwalimu Nyerere kwenye hotuba zao kwenye majukwaa na mikutano ya kisiasa lakini ukiwaambia wahame CCM wanakataa kata kata. Mimi nilikuwa najiuliza hawa wanamuenzi vipi.
Wakati wa huduma ya Nabii Issa ilipokuwa inafikia ukingoni, siku moja Nabii Issa alikamatwa akawekwa gerezani kutokana na mpango uliokuwa umeandaliwa kwa muda mrefu na mafarisayo na masadukayo ambao wengi wao walikuwa ni viongozi wa dini.
Kwa kifupi, falsafa za Nabii Issa zilikuwa zinapingana na mwenendo wa mafarisayo na masadukayo wakati ule. Humo gerezani au rumande Nabii Issa alikutana na Barnaba ambaye alikuwa amefungwa kwa ajili ya tuhuma za wizi au ufisadi.
Kama ilivyokuwa desturi wakati ule, Pilato alitakiwa atoe hukumu kwa Nabii Issa. Pilato aliangalia tuhuma za Nabii Issa na alibaini tuhuma hazikuwa na ushahidi, hivyo akataka amwache huru. Pilato aliwauliza wale watu waliokuwa wamekusanyika kwamba amwachie nani kati ya Barnaba na Nabii Issa. Umati uliokuwepo pale ukiongozwa na mafarisayo na masadukayo walipiga kelele kwa nguvu, wakisema amwachie Barnaba! Hivyo, Barnaba akatolewa gerezani kwa shinikizo la umati wa watu.
Sababu iliyosababisha mafarisayo na masadukayo na Wayahudi wengine wamtake Pilato amwachie Barnaba ambaye walikuwa wanajua ni mwizi au fisadi ni tabia yao ya unafiki. Tunaambiwa mafarisayo na masadukayo walikuwa na elimu ya kutosha, elimu ya dini na elimu ya kawaida.
Pia walijihesabia haki ya kupitiliza. Tatizo kubwa la mafarisayo na masadukayo ilikuwa unafiki, yaani kuishi maisha ambayo yalikuwa tofauti na walivyokuwa wakihubiri na tofauti na elimu waliyokuwa nayo. Walikuwa ni wanafiki kupindukia.
Mafarisayo walikuwa wakipita barabani wakisali sala ndefu ili waonekane. Kwenye masinagogi walikaa viti vya mbele. Walipotoa sadaka makanisani, walitoa fedha nyingi kwa kuonekana ili wasifiwe.
Walipokuwa wakisali, walisali kwa sauti kubwa ili maneno yao yasikike, walipangilia sala zao vizuri kwa ufasaha ili wasifiwe. Lakini, maisha halisi ya mafarisayo na masadukayo yalikuwa ni machafu, yaliyojaa ufisadi. Mahubiri ya Nabii Issa yaliwakasirisha sana mafarisayo na masudukayo kwani aliweka wazi unafiki wao.
Walikataa mahubiri yake. Hiyo ndiyo ilikuwa sababu kuu ya kumtaka Barnaba atolewe gerezani na kumkataa nabii Issa. Lakini kwa kumkataa nabii Issa, Israel inasumbuka mpaka leo.
Ndani ya CCM, kuna kundi la wana CCM wazee ambao wanatambua kwamba CCM imefika mwisho, imechoka, imekosa mwelekeo na imepoteza sifa na heshima ya kuendelea kuongoza nchi. Wana CCM hawa wamekuwepo ndani ya CCM toka wakati wa hayati Mwalimu Nyerere.
Wanatambua tofauti ya CCM ya leo na CCM ya Nyerere. Wazee hawa katika majukwaa mbalimbali wanaikosoa sana CCM na serikali yake. Je ni nini tofauti ya wana CCM hawa na mafarisayo wa Uyahudi waliomtoa Barnaba gerezani?
Hayati Mwalimu Nyerere aliwahi kuwaambia wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, na baadhi ya wazee ninaowazungumzia walikuwepo nanukuu "Watanzania wanataka mabadiliko. Wasipoyapata, wasipoyaona ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM". Baada ya kuwaambia maneno haya, wajumbe wengi wa Halmashauri Kuu ya CCM wakiwemo wazee wetu walishangilia sana.
Sijui kwa nini walishangilia, kwani tafsiri ya maneno haya ni kwamba kama CCM itashindwa kuleta mabadiliko basi Watanzania watayatafuta mabadiliko hayo kwenye vyama vya upinzani. Aidha, Hayati Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, na wazee hawa walikuwepo "Bila CCM madhubuti nchi itayumba".
Ni bayana kwamba C
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment