Mnasahau mwanajeshi SHIMBO mwaka 2010 alivyokuwa akijaribu kulitumia jeshi kupora haki ya wananchi kutumia sanduku huru la kura kuamua hatma ya nchi yao kuhusu nani awe Rais, mbunge na diwani? Kama siyo baadhi ya wanaharakati kusimama kidete kukemea si tayari alikuwa anatumia jeshi kuogofya wananchi wasijitokeze kupiga kura? Jiulize ni vyama vya upinzani vilimtumia Shimbo au ni chama dola CCM? Baadhi yetu HATUDANGANYIKI maana tuko macho kufuatilia hatma ya maslahi ya wananchi walioporwa mamlaka yao na chama dola.
Ananilea Nkya
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
--------------------------------------------
On Fri, 8/7/15, Edgar Mbegu <embegu@hotmail.com> wrote:
Subject: RE: [wanabidii] Kwa nini jina la Apson Mwang'onda?
To: "Wanabidii Mawazo" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Friday, August 7, 2015, 4:35 PM
#yiv4200429649
#yiv4200429649 --
.yiv4200429649hmmessage P
{
margin:0px;padding:0px;}
#yiv4200429649 body.yiv4200429649hmmessage
{
font-size:12pt;font-family:Calibri;}
#yiv4200429649 Huyu
Dilunga naye, hajawahi kusikia malalamiko ya Vyama vya
Upinzani juu ya namna vyombo vya Dola vinavyotumika vibaya
kwa maslahi ya baadhi ya Vyama?
Date:
Fri, 7 Aug 2015 12:09:16 +0000
From:
wanabidii@googlegroups.com
To:
wanabidii@googlegroups.com
Subject:
[wanabidii] Kwa nini jina la Apson Mwang'onda?
Kwa
nini jina la
Apson Mwang'onda?
Godfrey
Dilunga
JULAI,
mwaka 2012, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya
Usalama wa Taifa Tanzania, Apson Mwang'onda, alinukuliwa
na Gazeti la Nipashe,
akimjibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Kazi Maalumu,
Profesa Mark Mwandosya,
baada ya waziri huyo kuelekeza tuhuma zake za masuala ya
siasa kwa mkurugenzi
mkuu huyo.
Majibu
ya Mzee Apson yalikuwa yakikabili kile kilichoandikwa
na Profesa Mwandosya kupitia kitabu chake; "Sauti ya Umma
ni Sauti ya
Demokrasia" ambamo alikuwa akionyesha namna Apson
alivyoshiriki kumchezea rafu
za kisiasa.
Mwandosya
katika kitabu chake hicho alidai kwamba
alihujumiwa na Apson katika mbio za kuwania urais mwaka 2005
na vile vile
aliendelea kumhujumu katika harakati za kuwania nafasi ya
ujumbe wa Halmashauri
Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa Mkoa wa
Mbeya, mwaka 2007.
Angalau
katika majibu yake, Apson aligusia suala la maadili
ya kazi yake. Kwamba kuhusu kumsaidia Mwandoysa kuusaka
urais mwaka 2005,
ilikuwa ni vigumu, kwa kuwa; "maadili ya kazi yake
hayamruhusu."
Alisema;
"Mimi siwezi kuwa mkuu wa Idara, eti nimuunge mkono
kwenye uchaguzi wa urais, maadili ya kazi zangu hayaniruhusu
hivyo."
Leo
hii, kuelekea Uchaguzi Mkuu hapo Oktoba, 2015, jina la
Apson Mwang'onda linaibuka tena katika mijadala ya siasa
za ushindani wa
kuisaka Ikulu.
Jina
hili lilianza kuhusishwa na mbio binafsi za Lowassa
akiwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na sasa, kwa namna
fulani linaendelea
kuhusishwa na Lowassa huyo huyo akiwa ndani ya Chama Cha
Demokrasia na
Maendeleo (Chadema).
Apson
kwa sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa
Taifa mstaafu, mwenye kuendelea kula matunda ya kazi yake
hiyo ambayo bila
shaka, aliifanya kwa umahiri mkubwa na anastahili
pongezi.
Kazi
ambayo kwa nukuu yake hapo awali, aliifanya kwa
kuzingatia maadili na vile vile kwa sasa, anastahili
kuendeleza maadili,
nidhamu na unyenyekevu wake huo katika wakati huu wa maisha
yake ya kustaafu.
Naam,
katika maisha yake ya kustaafu kama mmoja wa wakuu wa
masuala ya ujasusi nchini bado, kwa sababu za maana na
muhimu, anapaswa
kuendelea kuheshimu kiapo chake cha kudumu.
Kiapo
ambacho anapaswa kukiheshimu kwa kadiri ya maisha
yake.
Hata
hivyo, kutokana na jina lake kuendelea kuhusishwa na
mikakati ya binafsi ya kusaka urais ya mmoja wa wasaka
madaraka hayo makubwa
zaidi nchini, heshima yake kwa kiapo chake hicho katika
maisha yake ya kustaafu
inatia shaka.
Kutajwa
mara kwa mara kwa Mzee Apson katika mapambano
binafsi ya kisiasa miongoni mwa makundi ya wanasiasa
kunafifisha nidhamu ya
kiapo chake hicho na kwa kweli hatua hiyo inapandikiza
nakisi kubwa mno katika
muktadha wa kutii mamlaka ya juu.
Ni
sawa na kusema, baada ya kustaafu, Mkurugenzi Mkuu wa
Idara ya Usalama wa Taifa anaweza kuishi maisha kwa kadiri
anavyotaka, ikiwamo
hata kuthubutu kupuuza mamlaka ya juu zaidi, kwa wakati
husika.
Hebu
tafakari, hali inakuwaje pale Mkurugenzi Mkuu mstaafu
(A) wa Idara ya Usalama wa Taifa anapoamua kutumia uzoefu
wake wa kijasusi
kumpigania mwanasiasa binafsi (A) na vile vile, Mkurugenzi
Mkuu mstaafu (B)
naye anaamua kutumia uzoefu wake wa kijasusi kumpigania kufa
au kupona
mwanasiasa (B)? Hali itakuwaje Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na
Usalama (A) aamue
kutumia uzoefu wake kumpigania kufa au kupona mwanasiasa (A)
katika kuisaka
Ikulu na kisha Mkuu (mstaafu) wa Majeshi ya Ulinzi na
Usalama (B) aamue
kumpigania mwanasiasa (B)?
Katika
muktadha huo, najiuliza kwa nini jina la Mzee Apson
linatajwa?
Na
kwa kweli, wakati najiuliza hivyo, natambua kwamba wapo
viongozi wakuu wa kitaifa wa vyombo vya ulinzi na usalama
nchini ambao maisha
yao ya kustaafu ni mfano bora kwa wenzao waliochukua nafasi
zao.
Kwa
mfano, hakuna shaka yoyote kwamba Jenerali Mirisho
Sarakikya, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (mstaafu)
amekuwa mmoja wa
wakuu wa kupigiwa mfano wa namna ya kuishi kwa nidhamu ya
kuheshimu kiapo
katika maisha ya kustaafu.
Nina
uhakika, pengine siku moja akiwa amekwishakwea Mlima
Kilimanjaro kwa mapenzi yake mwenyewe, na akiwa huko
akasikia Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania anapita jirani na anga la mlima huo,
atapiga saluti ya
utii.
Kwa
maana nyingine, atakuwa anaendeleza nidhamu ya kijeshi
katika maisha yake ya kustaafu.
Hakuna
mgombea urais ambaye mbio zake zimehusishwa na
Sarakikya. Hakuna mgombea urais ambaye mbio zake za kuisaka
Ikulu zimehusishwa
na Jenerali (mstaafu) George Waitara.
Wanatii
viapo vyao, hawataki kutumia uzoefu wao kufaidisha
kundi binafsi la msaka madaraka kwa gharama za ustawi wa
nchi. Wanaweza kutumia
uzoefu wao kutoa ushauri katika mamlaka husika na si kwa
genge binafsi la
kusaka madaraka.
Wanatambua
wakifanya hivyo watakuwa wameweka rekodi
(precedent) mbaya- tena mbaya kabisa- kwa vizazi vijavyo
vitakavyokuwa na
majukumu waliyowahi kuyashika nchini.
Nawasifu
hao na wengine wengi nchini, kwa kuwa sikusikia
majina yao yakitajwa, nimeshangaa kusikia jina la Mzee Apson
likitajwa mara kwa
mara kwenye michuano binafsi ya kisiasa miongoni mwa
wanasiasa. Najiuliza kwa
nini? Kuna lengo gani?
Kwa
kiongozi wa ngazi ya juu mfano wa Apson, maisha yake ya
kustaafu yanapaswa kubeba deni kwa taifa. Ni deni kwa taifa
kwa sababu alitumia nguvu, akili, na kila
mbinu kulitumikia kwa heshima kubwa taifa lake na kwa hiyo,
baada ya kustaafu,
taifa nalo ni lazima lilipe deni hilo na deni husika
linaweza kulipwa kwa njia
nyingi ikiwamo kuhakikisha anapata, bila vikwazo, stahiki
(privileges) zake
kama bosi mstaafu.
Hata
hivyo, inawezekana vipi kuvumilia kutoa stahiki husika
kwa mhusika ambaye tayari sehemu ya jamii inabeba tafsiri
tofauti dhidi yake –
tafsiri inayofanana na mtu anayekusudia kuukata mkono
unaomlisha.
Katika
maisha yake ya kustaafu yeye bado ni alama ya idara
aliyowahi kuitumikia.
Ndivyo
ilivyo, kwamba ingawa amestaafu lakini bado
anaendelea kuwa alama ya taasisi hiyo katika maisha yake
hayo ya kustaafu.
Bado
swali liko pale pale; kwa nini Apson? Kwa nini sio
wengine? Kwa nini siyo Waitara au Sarakikya ingawa wao
walikuwa wakuu wa
majeshi ya ulinzi na usalama?
Hakika,
nadhani ni wakati sasa kwa mamlaka husika kuchukua
uamuzi wa kubadili mwelekeo wa mashua ili kufika katika
kituo stahili.
Kubadili
mwelekeo wa mashua inawezekana kuliko kubadili
mwelekeo wa upepo unaovuma baharini au ziwani.
Aliwahi
kusema Jimmy Ray Dean, mwanamuziki, mfanyabiashara
na mtangazaji wa televisheni kwamba; "I can't change the
direction of the wind,
but I can adjust my sails to always reach my
destination."
Raia
Mwema
Toleo
la 417
5
Aug 2015
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment