Tuesday, 4 August 2015

Re: [wanabidii] FAIDA NA HASARA ZA LOWASA KUHAMA CCM NA KUHAMIA CHADEMA

Ukiisoma makala hii kwa makini unaweza kumalizia (conclude) kuwa:
1) CCM inawezekana ikanufaika
2) Mgawanyiko ndani ya Chadema kuhusu ujio wa Lowasa utakuwa msingi wa kukijenga upya chama kwa kuwatumia wale waliopinga ujio huo.
3) Watanzania itabidi tusubiri kwa vipindi viwili vya uchaguzi kwa Chama hicho cha upinzani kumtambulisha mtu anayeweza kuwa rais (na akaaminiwa) kutoka chama hicho (naamini Dr. Slaa atakuwa hawezi tena kugombea).
4) Kama CCM itafanya marekebisho ya msingi basi Tanzania itakuwa Botswana nyingine (Chama tawala kimebaki madarakani na hakina uwezo wa kutoka).

--------------------------------------------
On Tue, 8/4/15, 'lang'itomoni lokomoi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] FAIDA NA HASARA ZA LOWASA KUHAMA CCM NA KUHAMIA CHADEMA
To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Tuesday, August 4, 2015, 12:22 PM





FAIDA NA HASARA ZA LOWASA KUHAMA
CCM NA KUHAMIA CHADEMA

Katika sakata hili la Lowassa
kuhamia Chadema kuna vitu vya
kuzingatia;



1. Mpaka sasa hakuna yeyote anayejadili sera ya kilimo,
elimu , afya ,
miundombinu, uwekezaji , mambo ya nje, ulizi na usalama,
michezo na utamaduni,
hali ya hewa, nishati na madini, muungano na mambo mengine
muhimu kwa taifa.

Hili ni kosa, lakini si kubwa sana kwa vile ilani za
uchaguzi hazijaanza
kutangazwa.

Hata hivyo, hapa tunajifunza kuwa ratiba ya kuchagua mgombea
kabla ya kuwa na
ilani sio sahihi. Inafanya mijadala ijikite kwenye
personalities rather than
real issues.



2. Kila upande unaweza kuathirika au kunufaika na maamuzi ya
Lowassa kwenda
Chadema kama ifuatavyo;



i) CCM

Faida

a) Kupunguza lawama za kuitwa chama cha mafisadi.
Chadema  na Ukawa wameshaanza kuondoa
neno ufisadi na mafisadi kwenye kauli zao. Kauli yao mpya ni
kubadili mfumo.
Hata hivyo bado Chadema wana kibarua cha kuelezea
wataubadili vipi mfumo kwa
sababu mfumo sio chama cha siasa.



b) Kutoa fursa kwa wanasiasa wasio waaminifu kwa chama
kukikimbia na kuacha
wale walio tayari kukipigania chama. Rafiki wa kweli
hujulikana kipindi cha
changamoto.



c) Kupata fursa ya kuingiza wimbi kubwa la mamluki ndani ya
upinzani kwa
kisingizio cha kumfuata Lowassa. Hawa watapewa hero's
welcome na kuaminiwa
kirahisi.



Hasara

a) Siri zake za maandilizi ya uchaguzi zitafahamika kwa
upinzani. CCM
italazimika kufanya mabadiliko makubwa kwenye mikakati jambo
ambalo
litakigharimu chama.



b) Kupoteza baadhi ya watu ambao fundamentally wanaamini
Lowassa ndio mtu pekee
nchini mwenye uwezo na haki wa kuongoza. Ingawa kundi hili
ni la watu wasioelewa
maana ya chama lakini lipo. Hawa watamfuata Lowassa kokote
anakoenda, wanasema "ulipo,
tupo".



i) Chadema

Faida

a) Kupata mgombea tajiri ambaye ni high profile
politician.



b) Kupewa siri za CCM.



c) Kupokea wafuasi wa Lowassa.





Hasara

a) Kujenga sura ya kuthamini umaarufu na pesa kuliko misingi
ya Chama.



b) Kukiri de facto kuwa hawakuwa na uwezo wa kuishinda CCM.
Hapa watahojiwa je
mtu mmoja ndio amewaletea uwezo? Je , kama mtu huyo ana
nguvu kubwa kuliko
Chama, mtamdhibiti vipi akiwageuka huko mbeleni?



c) Kuwakatisha tamaa wanaojitolea kwa ajili ya Chama.
Kitendo cha Slaa kukatwa
na kutokusikilizwa kitawafanya watu kama kamanda Mawazo
wakae chini na
kutafakari kazi wanayojitolea inalenga kubadili nini? Wengi
wa wanaojitolea kwa
nia njema huongozwa na misingi na itikadi ya Chama. Chama
kinapotoka nje ya
misingi , kinahatarisha kupoteza au kuwavunja nguvu watu
hawa.



d) Kupunguza kuaminiwa na wananchi. Sura iliyojengeka ni
kuwa Chadema inacheza
tu mchezo wa siasa na hailengi hasa kuboresha maisha ya
mtanzania. Mtu yeyote
anayewapa pesa za uchaguzi watamtukuza ilimradi tu washinde.
Kauli hizi za
Mbowe hazijapokelewa vizuri na watanzania.



e) Kutumia nguvu kubwa kusambaza ujumbe mpya. Siku zote
inafahamika ujumbe wa
chadema ni kupinga mafisadi. Sasa kuna mabadiliko, tatizo
sio mafisadi ila
mfumo. Hii itahitaji resources nyingi kuwaeleza watu mpaka
waikubali. Kwahiyo
muda wa kuzungumzia masuala mengine ya maisha ya kila siku
utakuwa mdogo kuliko
wa kufafanua mabadiliko haya ya msimamo. Hii inaatarisha
Chadema kuonekana
Chama kinachotafuta madaraka bila kuwa na mkakati wa
kuongoza nchi na kuboresha
maisha.



f) Iwapo Chama hakitashinda uchaguzi kitakosa misingi ya
kukiendeleza. Kitabaki
kuonekana chama cha wajanjawajanja. Watu wa Lowassa ambao
wameahidiwa vyeo
serikalini itabidi watake vyeo kwenye Chama. Chama
kitachukuliwa na watu
wasiokijua wala kukijali kwa dhati.



3. Pamoja na kwamba watu hudhani siasa ni mchezo, lakini
siasa ni taaluma.
Katika haya yanayoendelea, mwenye taaluma zaidi ndiye
atayejipatia faida zaidi
kuliko hasara.



4. Sisi kama watanzania tunachotakiwa kuomba ni Mungu
aendelee kuilinda nchi
yetu iwe na amani na umoja kama taifa









--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment