Ahsante.
Siku hizi kuna watu wanakodishwa kuangua kilio kwenye misiba isiyowahusu, pasipokujuana na wafiwa wala marehemu. Lakini hao jamaa wanalia kweli kweli utadhani ni watu wa nasaba za karibu sana. Wapi! Hapa ndipo Tanzania ilipofikia.
Inafurahisha
From: wanataaluma@googlegroups.com [mailto:wanataaluma@googlegroups.com] On Behalf Of Yona Maro
Sent: 17 January 2015 22:00
To: wanabidii; Wanazuoni; wanataaluma@googlegroups.com
Subject: [TPN] MAMBO YA MUUNGANO NA KATIBA INAYOPENDEKEZWA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMBO YA MUUNGANO NA KATIBA INAYOPENDEKEZWA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
1.0 UTANGULIZI
(SHUKRANI)
WAHESHIMWA WAHARIRI,
Napenda kutumia fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyetuwezesha kwanza kuwepo hapa leo,Aidha kwa kutuwezesha na kujadili Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na hatimaye kwa kupatia Bunge la Katiba tukapata Katiba Inayopendekezwa ambayotunategemea mnamo mwezi wa April Wananchi wapande zote mbili za Jamhuri yetu,baada ya Kuisoma na kuielewa watapata fursa kwa mara ya kwanza katika historia ya Nchi yetu ya kuipigia Kura ya Ndio au Hapana.
Ikiwa watakao piga kura ya Ndio watazaidi asilimia 50 ya kila upande wa Jamhuri,jambo ambalo tunalitegemea sana baada ya ushawishi na taaluma mtakayo itoa,Nchi yetu itakuwa imepata Katiba mpya iliopata ridhaa ya wananchi wote wa Tanzania. Jambo hili si la kubezwa na hasa waipendeleao mema nchi yetu kama nynyi hapa,maana ni wachachae walio thubutu kutunga Katiba shirikishi kama tulivyo fanya sisi.Ni jambo la kujivunia.
Waheshimiwa Wahariri,,
Naomba nitumie fursa hii kuwashukuru nyinyi na wanachi wote kwa namna mlivyoshiriki katika kuhabarisha wananchi mchakato mzima wa Katiba na hatimae sasa tunakatiba inayopendekezwa ambayo sasa inahitaji mchango wenu wa hali na mali katika kuhakikisha inaungwa mkono na asilimia isiopungua 50 ya kila upande wa Jamhuri yetu Muungano wa Tanzania.
Nawaomba mjitahidi kutoa taaluma elekezi kwa kuweka maslahi ya Taifa letu mbele ambao umejengwa katika mkataba wa Muungano ambao ndio uliokuwa msingi mkuu wa kupatikana rasimu na hatimae Katiba Inayopendekezwa
2.0 CHANGAMOTO ZA MAMBO YA MUUNGANO KWA UPANDE WA ZANZIBAR
Kwanza, naomba nishukuru kwa kupewa heshima kubwa na fursa hii adhimu ya kuelezea mambo muhimu ya Muungano ambayo yamekua kama kielelezo cha malalamiko ya Wazanzibar kuhusu Muungano ambayo kwa kiasi kikubwa yamepatiwa ufumbuzi katika Katiba inayopendekezwa. ,
Katika utafiti uliofanywa na iliyokua Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakati wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba mpya. Mambo ya kadhaa yalitajwa kama malalamiko kutoka upande wa Zanzibar kuhusu Muungano kama ifuatavyo:
(i)Serikali ya Tanganyika imevaa koti la Serikali ya Muungano ambalo linaisaidia Tanganyika zaidi kuliko Zanzibar. Taswira hiyo imeifanya Tanganyika kuwa ndiyo Tanzania na Watanganyika ndiyo wamekuwa Watanzania; na Wazanzibari wamebaki kuwa Wazanzibari.
(ii)Mambo ya Muungano yamekuwa yakizidi kuongezeka na hivyo kuathiri uhuru wa Zanzibar (Autonomy) na kufifisha hadhi ya Zanzibar (Identity);
(iii)Kuvunjwa kwa makubaliano ya Hati ya Muungano kwa kuificha sura ya Tanganyika katika Muundo wa Serikali ya Muungano;
(iv)Kumuondoa Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
(v)Kutokuwepo kwa uwazi wa mapato na matumizi ya fedha za Serikali ya Muungano;
(vi)Kutokuanzishwa kwa Akaunti ya Fedha ya Pamoja;
(vii)Kuwepo kwa mkanganyiko wa ugawaji wa mapato na jinsi ya kuchangia gharama za uendeshaji wa shughuli za Muungano baina ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar;
(viii)Kuwepo kwa chumi mbili tofauti zinazoshindana katika nchi moja;
(ix)Zanzibar kutoshirikishwa kikamilifu na Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika masuala ya kupata misaada na mikopo kutoka nje ya nchi;
(x)Malalamiko kuwa viongozi wakuu wa Zanzibar wanachaguliwa Dodoma na sio Zanzibar kwenyewe;
(xi)Zanzibar kulalamika kuwa kuna baadhi ya mambo yamefanywa kuwa ya Muungano kupitia kutungwa kwa sheria na Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa mambo yasiyo ya Muungano na baada ya hapo mambo hayo kupata hadhi ya Muungano;
3.0 NAMNA MALALAMIKO HAYA YALIVYOTATULIWA KATIKA KATIBA INAYOPENDEKEZWA
3.1 Tanganyika kuvaa Koti la Muungano
Katika kutafuta ufumbuzi wa malalamiko ya Zanzibar kwamba Tanganyika imevaa koti la Muungano, Tume iliona kwamba muundo wa Muungano wa Serikali mbili ndio umeifanya Serikali ya Muungano,kwa kiwango kikubwa,kushughulikia zaidi mambo ya Tanzania Bara kuiliko Zanzibar, hasa katika mambo ya maendeleo. Na hivyo kupendekeza Muundo wa Serikali tatu katika Rasimu ya Katiba Sura ya sita Ibara ya 60.
Kwa upande wa Bunge Maalum, ilibaini kwamba utatuzi wa kero za Muungano hautegemei wingi au idadi ya Serikali bali dhamira thabiti waliyonayo viongozi katika kukabiliana na changamoto hizo. Na hivyo kupendekeza kuanzishwa kikatiba chombo kitakachosimamia na kuratibu utekelezaji wa Mambo ya Muungano na Uhusiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kudumisha Muungano. Chombo hicho kitaitwa "Tume ya Usimamizi na Uratibu wa Mambo ya Muungano", majukumu ya Tume hiyo yatakuwa ni pamoja na kuweka utaratibu bora na endelevu wa kushauriana na kushirikiana baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Mambo ya Muungano kwa manufaa ya ustawi wa wananchi wote;kupendekeza na kusimamia utaratibu utakaowezesha uwakilishi wa pande zote mbili za Muungano katika maeneo na masuala mbalimbali kwa nia ya kukuza umoja na mshikamano katika utekelezaji wa Mambo ya Muungano;kukuza na kuwezesha uratibu na ushirikiano baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Mambo yasiyo ya Muungano kwa lengo la kuwezesha kufanana kwa kiwango cha utoaji huduma kwa wananchi wote;kuratibu masuala yenye maslahi kwa Taifa; nakusimamia uwakilishi wa pande zote mbili za Muungano katika masuala ya ajira katika utumishi wa Jamhuri ya Muungano. Aidha, Tume hiyo pia itakua na jukumu la kusuluhisha na kutatua migogoro baina Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na endapo upande wowote haukuridhishwa na uamuzi uliotolewa na Tume, unaweza kupeleka shauri katika Mahakama ya Juu ambayo uamuzi wake utakua wa mwisho.
Hili ni badiliko kubwa katika historia ya Muungano wetu katika kushughulilikia Kero za Muungano.Kwa sasa vipo vikao vinavoongozwa na Makamo wa Rais,lakini hakina mamlaka kama kilivyoainishwa katika Katiba Inayopendekezwa, aidha hakukuwa na Mahkma ambayo ilikuwa inatambulika wazi wazi kushghulikia masuala yote ya Ki katiba zikiwemo Kero pindi ikiwa hazikupatiwa ufumbuzi katika Tume.
Kuanzishwa kwa Tume hii, tunaamini kwa kiasi kikubwa kwamba utakua mwarobaini wa kutatua kero za Muungano na kuondoa dhana kwamba Tanganyika imevaa koti la Muungano. Tume hii imeelezwa kwa kina katika Sura ya Tisa Ibara 127 na 128 za Katiba Inayopendekezwa.
3.2 Kuongezeka kwa Mambo ya Muungano;
Kuvunjwa kwa makubaliano ya Hati ya Muungano kwa kuificha sura ya Tanganyika katika Muundo wa Serikali ya Muungano;,
Katika kushughulikia malalamiko kuhusu kuvunjwa kwa makubaliano ya Hati ya Muungano kuificha sura ya Tanganyika katika Muundo wa Serikali ya Muungano, Tume haikutoa suluhisho kwa kuzingatia Hati ya makubaliano ambayo inalalamikiwa kwamba imekiukwa na badala yake ikapendekeza Muundo wa Serikali tatu katika Ibara ya 60 kama nilivyokwishaeleza, ambayo kimsingi inaenda kinyume na Hati ya makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964.
Kwa upande wa Bunge Maalum, iliipitia Hati ya Makubaliano ya Muungano ya Mwaka 1964 na kubaini kwamba katika makubaliano hayo, Zanzibar ilikubali kuhamishia sehemu ya mamlaka yake kwenye Serikali ya Muungano na iliyokuwa Tanganyika ilikubali kuhamishia mambo yake yote kwenye Serikali ya Muungano. Katika kutafakari muundo wa serikali, waasisi wa Muungano walifikiria kuwa na muundo wa serikali moja au serikali tatu. Lakini waliona muundo wa serikali moja usingekuwa muafaka kutokana na ukweli kwamba Zanzibar ni nchi ndogo iliyokuwa na idadi ya watu laki tatu ikilinganishwa na Tanganyika iliyokuwa na watu milioni kumi na mbili kwa kipindi kile, hivyo ingeonekana dhahiri kwamba Zanzibar imemezwa na iliyokuwa Tanganyika.Hivyo, waasisi waliona ni busara Zanzibar ibaki na utambulisho wake kwa maana ya Serikali na vyombo vingine vya utendaji.
Kwa kuzingatia ukweli huu, na katika kuhakikisha kwamba inatatua kero hii kwamba Hati ya Muungano haivunjwi wala kukiukwa, Bunge Maalum limependekeza Muundo wa sasa wa Jamhuri ya Muungano wa serikali mbili uendelee kwasababu ndiyo unaokidhi matakwa Hati ya Makubaliano ya Muungano ya Mwaka 1964 ambayo ndiyo msingi wa muundo wa serikali mbili kama ulivyooelezwa vizuri katika Sura ya saba Ibara ya 73 ya Katiba inayopendekezwa.
Aidha,kama waumini wa serikali Tatu au Serikali ya Mkataba wangalitaka kwa dhati mapendekezo ya Tume yakubaliwe,basi wangalishiriki kikamilifu katika mchakato mzima wa utungwaji wa Katiba.Kitendo cha kususia kinatoa tafsiri kwamba hawakuwa waumini wa dhati wa serkali tatu wala serikali ya mkataba ambazo zote(tatu na mkataba)hazikupta kuungwa mkono na wananchi wakati wa mchakato wa kukusanya maoni na angalau asilimia 50 ya kila upande wa Jamhuri ambalo ni sharti la Kisheria.
3.3 Kumuondoa Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
Waheshimiwa wahariri,
Malalamiko mengine yalikua ni kumuondoa Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Katika kushugulikia malalamiko haya, Tume pia haikutoa suluhisho kwa kuzingatia Hati ya Makubaliano ya Muungano, na badala yake ikapendekeza kuanzisha Mamlaka za Nchi Washirika ambazo zitakua na marais wake chini ya Serikali ya Jamhuri Muungano. Sura ya sita Ibara 64 na 65.
Kutokana na hoja za msingi za kumjumuisha na kumtambua Rais wa Zanzibar kama miongoni mwa viongozi wakuu wa Jamhuri ya Muungano. Bunge Maalum limezingatia Hati ya Makubaliano ya Muungano ya Mwaka 1964 iliyomtambua Rais wa Zanzibar kama Makamu wa Rais na hivyo kumrejeshea wadhifa huo wa Makamu wa pili wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, mapendekezo haya yanalenga kumwezesha Rais kupata wasaidizi wakuu wa kumshauri katika kutekeleza majukumu yake aliyopewa kikatiba.Rais wa Zanzibar atakua Makamu wa Pili wa Rais na msaidizi mkuu wa Rais kwa mambo ya muungano yanayoihusu Zanzibar. Sura ya nane Ibara ya 107.
Nivyema ikumbukwe kuwa CUF ilikwenda mahakamani kupinga badiliko la 11 la kumuondoa Rais wa Zanzibar kuwa Makamo wa Rais.Leo iweje waheshimiwa wahariri,wawe wapingaji wakubwa wa Katiba inayopendekezwa ambayo imerejeesha nafasi ya Rais wa Zanzibar kama ilivyo katika Mkataba wa Muungano na mabadiliko yake?
3.4 Kutokuwepo kwa uwazi wa mapato na matumizi ya fedha za Serikali ya Muungano;
Waheshimiwa wahariri,,
Kuhusu uwazi katika mapato na matumizi ya fedha za Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Rasimu ya Tume imeanisha katika Ibara ya 231 vyanzo vya mapato tu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano bila ya kuweka masharti ya uwazi wa matumizi wa mapato ambayo ndiyo hoja ya msingi inayolalamikiwa na Zanzibar.
Aidha katika kutatua kero hiyo, Bunge Maalum limezingatia katika Katiba inayopendekezwa masharti kuhusu matumizi ya fedha kwa uwazi kwa kuweka Ibara mahsusi (Ibara ya 250) inayoweka masharti kuhusu misingi itakayoongoza matumizi ya fedha za umma katika Jamhuri ya Muungano ikiwemo uwazi, umakini na uwajibikaji; mfumo wa fedha kulenga maendeleo linganifu; na kuzingatia ustawi linganifu kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
Pamoja na kupatiwa ufumbuzi wa ki katiba,hivi sasa mapato yote yanayokusanywa Zanzibar yanabaki Zanzibar na utaratibu wa kukusanya mapato yatokanayo na hudma kama simu n.k.unatekelezwa katika utaratibu wa kushughuikia Kero za muungano chini ya Makamo wa Rais.Hivyo Katiba Inayopendekezwa itaweka misingi imara zaidi ya mgawano wa mapato.
3.5 Kutokuanzishwa kwa Akaunti ya Fedha ya Pamoja;
Mheshimiwa Rais,
Katika Rasimu ya Katiba ya Tume, suala la kuanzishwa kwa akaunti ya Fedha ya pamoja halikuzingatiwa kabisa na hivyo kufifisha matumaini ya wazanzibari juu ya kutatuliwa kwa kero hii.
Katika kuhakikisha inatatua malalamiko haya ya muda mrefu, Bunge Maalum katika Sura ya kumi na sita Ibara ya 251 ya Katiba inayopendekezwa imezingatia hoja hii na hivyo kupendekeza kuanzishwa kwa Akaunti Maalum itakayoitwa "Akaunti ya Fedha ya Pamoja" ambayo itakuwa ni sehemu ya Mfuko Mkuu wa Hazina, ambamo fedha zote zitakazopatikana kwa njia mbalimbali pamoja na fedha zote zitakazochangwa na Serikali zote mbili kwa kiasi kitachoamuliwa na Tume ya Pamoja ya Fedha, kwa mujibu wa sheria itakayotungwa na Bunge kwa madhumuni ya shughuli za Muungano kwa Mambo ya Muungano.
Nikweli kero hii ilichangia sana katika kudhoofisha Muungano wetu,kwani Tume ya pamoja ya Fedha pamoja na kutoa mapendekezo yake kwa serikali zote mbili,utekelezaji wake umekuwa wa kusuasua.Ni kwakutambua hili ndipo Bunge Maalum la katiba pamoja na mambo mengine,likaweka msingi wa kikatiba wa kwenda Mahakama ya Juu pale ama upande mmoja wa muungano au taasisi au mtu hakutekeleza uamuzi wa Tume ilio chini ya Makamo wa Rais.Hili ni badiliko kubwa la Ki Katiba katika kutatua kero za Muungano.
3.6 Kuwepo kwa mkanganyiko wa ugawaji wa mapato na jinsi ya kuchangia gharama za uendeshaji wa shughuli za Muungano baina ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar;
Mheshimiwa Rais,
Kama nilivyokwishaeleza hapo juu kuhusu uanzishwaji wa Tume ya pamoja ya Fedha, suala hili pia halikuzingatiwa na Tume ambayo ilipendekeza Muundo wa Serikali tatu ambapo Nchi washirika zingekua na mamlaka yake ya fedha kuhusu mapato na matumizi yake isipokua vyanzo vichache vya mapato vilivyopendekezwa kuendesha Serikali ya Muungano. Hata hivyo, hakuna masharti yoyote yaliyowekwa kikatiba endapo mshirika mmoja wa muungano atashindwa au atakataa kuchangia.
Katika kushughulikia mkanganyiko wa ugawaji wa mapato na jinsi ya kuchangia gharama za uendeshaji wa shughuli za Muungano baina ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar. Bunge maalum, katika Sura ya sita Ibara ya 252 limependekeza kuanzisha Tume ya Fedha ya Pamoja, yenye Wajumbe wasiozidi saba watakaoteuliwa na Rais kwa kushauriana na Rais wa Zanzibar. Majukumu ya Tume ya Fedha ya Pamoja ni kuchambua mapato na matumizi yanayotokana na au yanayohusu utekelezaji wa Mambo ya Muungano na kutoa mapendekezo kwa Serikali za pande zote mbili kuhusu mchango na mgao wa kila Serikali mojawapo, kuchunguza kwa wakati wote mfumo wa shughuli za fedha wa Jamhuri ya Muungano na pia uhusiano katika mambo ya kifedha kati ya Serikali hizo mbili pamoja na kutekeleza majukumu mengine ambayo Rais ataipatia Tume au kama Rais atakavyoagiza kwa mujibu wa sheria itakayotungwa na Bunge.
Ukirejea hapo nyuma utaona kuwa utekelezaji wa Ibara hii,unatiwa nguvu na uwepo wa Tume ya pamoja ya Fedha,Tume ya Mambo ya muungano na Uhusiano na Mahkama ya Juu.Ni wazi,pamoja na sheria itakayotungwa na Bunge ambayo itaweka wazi taratibu zote,ikiwa na pamoja na kuchukua hatua kwa wanaopinga kutekeleza matakwa ya Katiba mapungufu yalio kuwepo yatakuwa yamepungua kwa kiasi kikubwa hivyo itasaidia sana kuimarisha Muungano wetu..
3.7 Zanzibar kutoshirikishwa kikamilifu na Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika masuala ya kupata misaada na mikopo kutoka nje ya nchi;
Waheshimiwa wahariri,,
Pamoja na Rasimu ya Tume kupendekeza Zanzibar kupewa mamlaka ya kukopa nje ya nchi lakini iliweka sharti la hiari kwa Serikali ya Muungano hata baada ya kukubaliana na kushauriana na Serikali ya Zanzibar bado inaweza kutoa dhamana ya mkopo huo. Jambo hili lilitafsiriwa na wazanzibari wengi kama litaweka ukakasi na urasimu katika utekelezaji wake.
Katika kuhakikisha kwamba inaondoa sharti hilo la hiari, Katiba inayopendekezwa katika Sura ya kumi na sita, Ibara ya 261 imetoa Mamlaka ya Zanzibar kukopa fedha kutoka katika taasisi za fedha za kikanda na kimataifa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Aidha, endapo mkopo utahitaji dhamana, Serikali ya Jamhuri ya Muungano, baada ya kushauriana na kukubaliana Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar bila kuwa na masharti yoyote itatoa dhamana kwa mkopo unaoombwa.
3.8 Zanzibar kuwa Mamlaka ya kuanzisha uhusiano au ushirikiano na Jumuiya au taasisi yoyote ya kikanda au kimataifa.
Katika kuhakikisha inatoa ufumbuzi wa malalamiko ya Zanzibar kunyimwa uhuru na uwezo wa kujiunga na taasisi za kimataifa, Katiba inayopendekezwa katika Sura ya saba Ibara ya 76 imezingatia maoni ya rasimu ya Katiba kwa kutoa mamlaka kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuanzisha uhusiano au ushirikiano na jumuiya au taasisi yoyoyte ya kikanda au kimataifa. Aidha, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaomba na kupata ushirikiano kutoka kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano endapo katika kufanikisha uhusiano au ushirikiano na jumuiya au taasisi za kikanda na kimataifa utahitaji dhamana au uthibitisho wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Zanzibar kulalamika kuwa kuna baadhi ya mambo yamefanywa kuwa ya Muungano kupitia kutungwa kwa sheria na Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa mambo yasiyo ya Muungano na baada ya hapo mambo hayo kupata hadhi ya Muungano;
Bunge Maalum la katiba lilipitia na kuchambua orodha ya mambo ya Muungano ambpo Tume ilipendekeza mambo 7 kutokana n mfumo wa Muungano wa serikali tatu;Bunge la Katiba limependekeza mambo 16 badala ya 21 yalioko sasa,hivyo kuliondoa kabisa katika orodha ya mambo ya muungano suala la Gesi na Mafut,jmbo ambalo lililalamikiwa sana Zanzibar tokea utawala wa serikali ya awamu ya 5. Hivyo Katiba Inayopendekezwa imetoa uhuru kwa Zanzibar kutafuta na kuchimba mafuta na gesi na mapato yote yatakuwa ni ya SMZ na washirika wake(makampuni ya mafuta na gesi) yatakayo ingia mkataba nayo.
Waheshimiwa wahariri,wapo wanao kejeli eti,kwakuwa Ardhi ni ya muungano,hivyo mafuta hayo yakichimbwa ndani ya ardhi ya Muungano,hichi si kiini macho?Nikweli,kwa mujibu wa Katiba ya sasa na inayopendekezwa,mipaka yote ya nchi,ardhi,maji na anga ni ya jamhuri ya muungano,lakini katiba hiyo hiyo inatoa mamlaka kwa serikali,kuu,manispaa,halmashauri na upnde wa pili wa jamuhuri ya kutunga sheria juu ya matumizi ya Ardhi na umiliki wake.
Ndio maana katika katiba Inayopendekezwa kila ibara ambayo kunahitajika kutwanga kwaheria,jukumu hilo limepewa Bunge kwa mambo ya muungano na Baraza la Wawakilishi kwa mambo ya Zanzibar yasio ya Muungano.
Waheshimiwa wahariri,
Naomba kuhitimisha madayangu,kwa kusema kuwa,hakuna mkamilifu,mana hata katiba y zanznzibar ilioandikwa na magwiji wa sheria,hakuna mgombea binafsi wa Tuje ya uchaguzi haihojiwi popote baada ya kumtangaza mshindi wa ugombea wa Urais.Katiba inayopendekezwa imetoa fursa kwa mgombea binafsi na Tume ya uchaguzi itahojiwa mahakamani kwa mgombea waliomtangaza,pindi walioshindana nae hawakuridhika na matokeo yalio tangazwa
Vitabu vitakatifu,waumini wengi wanaamni ni maneno ya Mola,lakini wapo wanaovikana,kuvikosoa na hata baadhi ya wanao amini nao hufuata yale wanayo yapenda tu.
KWA KUTAMBUA UKWELI HUU,KATIBA INAYOPENDEKEZWA IMEWEKA NJIA KADHAA ZA KUFANYA MABADILIKO PINDI IKIONEKANA KUNA HAJA YA KUFANYA HIVYO.HUU NI MWANZO SIO MWISHO.TUIUNG MKONO KWA KUIPIGA KURA YA NDIO KATIBA INAYOPENDEKWAZA.
NAOMBA MUWAPE WATANZANIA TAARIFA ZILIZO SAHIHI NA ZAIDI ZAKUDUMISHA UMOJA,MSHIKANO NA ZAIDI AMANI YA NCHI YETU.HII NDIO TUNU YETU-TUIENZI KWA GHARAMA YOYOTE.
AHSANTENI.
HAMAD RASHID MOHAMED (MB)
--
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanataaluma Wazalendo" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanataaluma+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment