Saturday 17 January 2015

Re: [wanabidii] RAIS MSTAAFU MWINYI ANAVYOMZUNGUMZIA JANUARY MAKAMBA

Motive ya mawakala wanaotumia dini kwa ajili ya kupata uongozi wa kisiasa ili kutekeleza 'their hidden agenda', sooner or later itajulikana tu.


From: 'ngupula' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
To: mngonge franco <mngonge@gmail.com>; wanabidii@googlegroups.com
Sent: Saturday, January 17, 2015 6:05 PM
Subject: Re: [wanabidii] RAIS MSTAAFU MWINYI ANAVYOMZUNGUMZIA JANUARY MAKAMBA

Kama Tanzania itaanza kuzungumzia Makamba kama rais I guess the whole country would be a bunch of stupid people.

mngonge franco <mngonge@gmail.com> wrote:

Nafikiri wakati mwingine tunatumia nguvu zetu na muda kuandika uzushi. Haya kweli ni maneno ya mzee Mwinyi? Mzee mwinyi amdisuss January Makamba ili iweje sana sana anaweza kutoa comment ya sentensi moja au mbili. Nakumbuka maneno ya Emmanuel Mganda kwamba some the so called presidential candidates should be labelled as " DEAD ON ARRIVAL"  hakuna hata haja ya kupoteza muda kuwadiscuss

2015-01-15 17:17 GMT+03:00 MABADILIKO CHADEMA <mabadilikochadema@gmail.com>:
HIVI NDIVYO RAIS MSTAAFU MWINYI ANAVYOMZUNGUMZIA MAKAMBA.

Nimefarijika kuyasoma mazungumzo baina ya Padri Privatus Karugendo na Ndugu January Makamba, mmoja wa viongozi mahiri wa zama za sasa.Nawapongeza kwa kuamua kuyaweka mazungumzo yao katika rekodi ya maandishi. Hakika tumejifunza mengi kuhusu na kutokana na historia na falsafa ya maisha ya Ndugu Makamba pamoja na fikra zake kuhusu Tanzania ijayo.

Jamii inanufaika tunapowafahamu kwa kina viongozi wetu. Utaratibu huu wa Padri Karugendo ni jambo jema na inabidi uendelezwe. Binafsi nilikuwa namfahamu Ndugu Makamba kama kiongozi ndani ya Chama chetu na kwenye Serikali. Fursa ya kusoma mazungumzo yake imenisaidia kumfahamu zaidi kama mtu lakini pia kufahamu fikra zake. Nimefarijika kwamba nchi yetu na Rais wetu Kikwete ameendeleza utamaduni aliouanzisha Mwalimu Nyerere na kuendelezwa nami wa kuwaamini vijana na kuwapa fursa za uongozi ili kuwaandaa kuiongoza nchi yetu. 

Nilimteua Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Mbunge na Naibu Waziri akiwa na umri wa miaka 38 tu na baadaye Waziri wa Wizara muhimu ya Maji, Nishati na Madini akiwa na umri wa miaka 40 na baadaye Waziri wa Fedha. Sikufanya hivyo kwasababu tu ya umri wake bali kutokana na kuamini katika msingi wa kuandaa viongozi wa vizazi vijavyo kwa kuwapa majukumu katika Chama na ndani ya Serikali. Kwa kusoma mazungumzo ya Padri Karugendo na Ndugu Makamba ni dhahiri kabisa kwamba Ndugu Makamba aidha ameandaliwa au amejiandaa vizuri kuwa kiongozi mkubwa. Kazi hii ya kuandaa viongozi lazima iendelee kufanywa. Kiongozi mzuri ni yule anayetengeneza viongozi wengine wapya.

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


0 comments:

Post a Comment