Siku moja Mwalimu Nyerere alimuuliza mwandishi mmoja wa habari huko Nairobu kuwa 'Hivi mtu akikwambia kuwa mimi ni baba yako utakubali' Watu walicheka sana.
--------------------------------------------
On Sat, 1/24/15, 'Happiness Katabazi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: [wanabidii] MUNGU AKULINDE SOSPETER MUHONGO
To: "WANABIDII" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, January 24, 2015, 5:54 PM
MUNGU AKULINDE SOSPETER MUHONGO
Na Happiness Katabazi
LEO saa tano asubuhi, Aliyekuwa Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Muhongo alitangaza rasmi kujiuzuru
nafasi hiyo ya uwaziri kwasababu ya zogo la Escrow.
Tangu mwanzo kupitia makala yangu msimamo wangu niliweka
wazi Kuwa naunga mkono Utendaji kazi wa Profesa Muhongo na
hata Leo hii ninavyoandika makala hii sitabadilisha msimamo
wangu Kuwa Kwangu Profesa Muhongo ni Miongoni mwa Mawaziri
wa Nishati na Madini ambao nimewashuhudia Kuwa ni mawaziri
ambao wameacha alama ya kukumbukwa.
Pia tangu mwanzo nilisema wazi kupitia makala zangu
mbalimbali kwa jicho la Sheria Katika zogo la Escrow Hakuna
Mashitaka ya wizi Kama baadhi ya watu walivyokuwa wakiwa
hukumu Moja kwa Moja watu waliotajwa kwenye
zogo la Escrow Kuwa ni wezi na kwamba Fedha za Escrow
zimeibwa.
Hoja yangu ilipingwa na baadhi ya watu waliokuwa
wakisema Fedha za Escrow ni za umma na fedha hizo za Escrow
zimeibwa na waliiba ni wezi wanastahili kushitakiwa kwa
wizi, ilikuja Kufungwa mkono na Rais Jakaya Kikwete, Disemba
22 Mwaka Jana, Katika mkutano wake na wazee wa Mkoa wa Dar
es Salaam, pamoja na mengine alisema hatukuwa na wizi Katika
Fedha za Escrow na Fedha za Escrow siyo mali ya umma.
Pia mapema Mwaka huu, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa ili wafungulia Kesi ya kupokea
Rushwa kutoka kwa Lugemalila baadhi ya maofisa wa serikali
ambao waliotajwa kwenye zogo la Escrow.
Tusubiri hatima ya Kesi hizo itapofika Tamati na tusubiri
pia ushahidi utakaotolewa na Huyo Lugemalila je
Lugemalila akifika mahakamani atatoa ushahidi wa ni kweli au
si kweli aliwapa rushwa? pia tusubiri utetezi wa washitakiwa
hao na uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es
Salaam, utakapotolewa.
Profesa Muhongo ametaja baadhi ya Sababu zilizomsukuma
kufikia uamuzi huo, Nampongeza kwa uamuzi huo licha
amekuchukua wakati Tayari mashankupe na
mapashukuna wameishalipaka matope jina lake
Mbele ya Jamii.
Waswahili wanasema penye ukweli, uongo ujitenga. Hivyo ipo
siku ukweli wa hili zogo la Escrow utakuja kujulikana nani
muhasisi wake? Kwanini waliliasisi zogo hili?,Muhongo
alishiriki kwa kiasi gani Katika jambo Hilo?Ni kweli Katika
Utawala wa Muhongo Wizara ya Nishati ilipata Hasara na
kwamba Hakuna jambo lolote la maendeleo alilolifanya?
Aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa wakati akitoa hotuba
yake bungeni wakati ajijuzuru pamoja na mambo mengi
alisema ; ' Tukiruhusu kila mwanasiasa ajijuzuru kwa tuhuma
tu ambazo hata hazijathibitika Hakuna mwanasiasa atakayebaki
salama'.
Kweli sasa mantiki ya ubashiri huo wa maneno ya Mzee
Lowassa yameanza kutimia.
Hongera Muhongo kwa uamuzi huo Kwani utakupa fursa ya kwenda
kufanya shughuli nyingine kwa Amani na utulivu kwa watu
wenye akili timamu ambao wanamisimamo usiyoyumba na Kamwe
hawaamini katika majungu na upashukuna.
Mema uliyoyafanya Katika Wizara ya Nishati na
Madini,tutayakumbuka na tutaheshimu mchango wako katika
sekta ya nishati na madini.
Utendaji kazi wako kumbe ulikuwa ukiwakera baadhi ya walafi
.Na watu wanaofikiri sawa sawa tunajiuliza ni kwanini kila
kukicha Mawaziri wa Wizara ya Nishati na Madini hasa katika
serikali ya awamu ya nne wamekuwa wakishambuliwa wazi wazi
na mwishoe wamekuwa wakijiuzuru au kuondolewa katika wizara
hiyo?
Mbona Wizara Kama Wizara ya Maendeleo ya Jinsia na Watoto
hata siku Moja hatushuhuudii wanasiasa uchwara wakikomalia
Kuwa mawaziri wake wameshindwa kazi Kwani kila siku ripoti
zinaonyesha watoto wadogo ,wanawake wanafanyiwa vitendo Vya
kikatiri Kama kubakwa na Kuuwawa?
Ni Wizara ya Nishati na Madini tuu ndiyo inastahili
kumulikwa ? .Jibu ni Jepesi hapa ni manyang'au yenye Nguvu
za kifedha yalizibiwa mirija ya kufanya biashara zao kwa
njia chafu Katika sekta ya Madini na Nishati.
Ikumbukwe Kuwa wale wote ambao mnatumia Hiari na uchafu wa
kila aina kuwachafua wenzenu na kuakikisha wenzenu wanatoka
madarakani kwaajili ya mashinikizo yenu, ipo siku na Nyie
wakati wenu utafika wa kulipwa hapa hapa na Mungu malipo ya
hizo hira Zenu na msije kulia na Mtu.
Nchi hii Ilipofika hivi sasa, majungu, fitna,ushirikina,
uzandiki Ndio umetawala na umeshika hatamu.Watu wasiyo na
hatia na siyo kwenye Nyanja za siasa tu wanaangamia kwa
ushenzi huo.
Imekuwa nchi ya watu tunaopenda Ujinga Ujinga na uzushi
halafu na mbaya zaidi tabia hizo zinafaywa na wanaume amba
wanawake nyumbani eti tunajiaminisha nchi hii itapata
maendeleo kwa haraka.
Wito wangu kwa Watanzania wanaishi nchi za nje na kufanya
kazi katika taasisi za kimataifa nje ya nchi na wamesoma
vizuri ,wasiwe wepesi sana kurudi nchi Kuja kufanyakazi Hasa
za kisiasa kwa kisingizio eti serikali imewaomba sana Kuja
Tanzania kufanya kazi.
Nawaomba mjifunze kwa yaliyowakuta wenzenu ambao walikuwa
wakifanyakazi nje ya nchi akiwemo Profesa Muhongo ambaye
alikuwa akifanya kazi nje ya nchi, serikali ya awamu ya nne
chini ya Rais Jakyaa Kikwete ikamuona wa maana sana,
ikamtaka arejee nchini aje alitumikie nchi na kweli alikuja
kuitumikia lakini malipo aliyoyapata ndiyo hayo mmeyaona.
Ambayo minayafananisha na tabia zinazofanywaga na waswahili
swahili huku mtaani za kumkodishia ngoma ya mdundiko mtu na
kuja kumsuta mtu.
Au kumkodishia mapashukuna kila kukicha wawe
wanamchafua jina lake na kweli wamefanikiwa na waliokuwa
wanatakiwa wadhibiti Hali hiyo wamekaa kimya.
Mke wangu IGP- Said Mwema na Mkurugenzi wa TAKUKURU
,Dk.Edward Hosea wakati Sakata la Fedha za EPA bado
washitakiwa hawajapelekwa Mahakamani na wananchi walikuwa
wakishinikiza wapelekwe.
Viongozi Hao ambao ni makachero wazuri tu walikuwataka
wananchi wawe na subira na Kusema HIvi " Mafisadi ni watu
hatari sana hivyo inatakiwa kwenda nao Polepole". Ni
kweli makachero hao walikuwa walikuwa wakijua wanavyosema na
ndicho kilichomkuta Mtani wangu Muhongo.
Hivyo Muhongo muachie Mungu, yeye ndiyo muweza wa yote,
endelea kulitumikia taifa Lako kwa uaminifu ila kwa taadhari
pia Kwani Tulipofika sasa watendaji waaminifu na
wachapakazi nchi hii HIvi sasa nikama hawatakiwi.
Tusubiri tuletee Waziri wa Nishati na Madini ambaye uenda
anaweza Kuwa malaika kutoka mbinguni ambaye Kamwe hataguswa
na tuhuma yoyote Kama watangulizi wake Wizara hiyo
walivyokabiliwa na tuhuma na kutakuwa kujiuzuru.
Pia tusubiri Huyo Waziri wa Nishati na Madini mpya ambaye
atateuliwa na Rais Kikwete ambaye ataweza kuendeleza
Yale yaliyoachwa na Muhongo na alete mipango yake Mipya
Katika Kipindi hiki kifupi kilichobakia kuelekea
uchaguzi Mkuu Oktoba Mwaka 2015. Na tumpe ushirikiano siyo
kuanza kumchokona.
Mwisho namtakia kila la kheri Mtani wangu Profesa Muhongo
Katika majukumu yake mapya.Hongera kwa uamuzi huo wa
kujiuzuru licha kwa wale walikuwa tunafahamu mchango uamuzi
huo umekusikitisha ila hatuna jinsi.
Wewe siyo wa kwanza kujiuzuru nafasi hiyo kwa Sababu umeona
jina Lako lime nafika. Hata aliyekuwa Waziri wa serikali ya
awamu ya Tatu, Dk. Kitine naye Alifikia uamuzi wa
kujiuzuru uwaziri kwa Madai Kuwa alitafuna Fedha za umma kwa
kisingizio Kuwa Mkewe alikuwa Amelazwa Canada kwaajili ya
matibabu na Katika mahojiano yake na Gazeti la Mtanzania la
Jumapili la wiki iliyopita , Dk.Kitine akifanya mahojiano na
Gazeti Hilo alilitaja kundi la wanamtandao na ndiyo
walioshiriki kumzushia fitna hiyo na walifanikiwa kumchafua
kwasababu walikuwa wakiisoma Rais Benjamin Mkapa alikuwa
akimwandaa Kuwa Rais wa Tanzania Mwaka 2005.
Lakini Kamati ya Bunge ya Wizara ya Mambo ya nje ilikuja
kumsafisha na kunekana ni kweli Mke wake alikuwa ni mgonjwa
na alilazwa huko Canada.
Narudia tena wale wote mabingwa wa kufanya binadamu wenzao
kwa Lengo tu la kupata maslahi Fulani ikiwemo biashara, vyeo
Mkae mkijua ipo siku Mungu atawaadhibu.
Kumbukeni hawa mnao wafanyakazi ufedhuli nao wana Mungu na
Mungu wao wala siyo kipofu wala kiwete anayetembelea
Magongo.Ipo siku Mtalipwa Ubaya mnaofanyia
wenzenu.Aminini hivyo.
Mungu akutangulie Muhongo nenda kafanyekazi na wasomi
wenzio achana na hawa wanaume 'wachambue Michele'
ambao wametawaliwa na husuda na fitna na unafki na vichwa
vyao wanavitumia kwaajili ya Kufugia nywele badala ya
kufikiri.
Mungu ibariki Tanzania
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Januari 24 Mwaka 2015
0716 774494.
Sent from my iPad
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment