Sunday, 8 September 2013

[wanabidii] .. Shabaan Robert Alisema; Msema Kweli Atakimbiwa Na Rafiki Zake...



Ndugu zangu,

Ni bahati mbaya sana kuwa tumewekeza katika uongo. Tumekuwa waongo mno. Tuna wanasiasa waongo. Tuna viongozi wa dini waongo na tuna hata wanahabari waongo.

Na duniani hapa kuna aina tatu za uongo; Mosi, kuna uongo wa kawaida usio na madhara sana, hata kama ni jambo baya. Kwa mfano, utamkuta mtu mmekaa nae Kijitonyama, basi, ataongea na mke au mumewe kuwa yuko Mbagala Rangi Tatu! Sasa Kijitonyama na Mbagala Rangi Tatu wapi na wapi! Lakini hakuna atakayekufa kwa uongo huo hata kama ni kitu kibaya.

Pili, kuna uongo wa Kitakwimu. Kwamba takwimu zinatumika kuongopa. Kiongozi anasimama na kuwasomea wananchi takwimu bila uthibitisho. Na kwa vile wengi hatujui hesabu, basi, tunaishia kuongopewa.

Tatu, uongo wa kishetani. Huu ni uongo mbaya kuliko wote. Watu wanaongopa kwenye mambo ya msingi yenye kuhusu mustakabali wa taifa, mtu binafsi na hata afya na uhai wa watu.

Kwa mfano, nesi aliyeambiwa na daktari ampe vidonge mgonjwa aliye taabani kitandani. Lakini kwa vile ndugu wa mgonjwa hawakuacha chochote kwa nesi, mgonjwa ataachwa. Na akifa bado akiulizwa nesi atasema kwa macho makavu kuwa amempa mgonjwa dawa lakini hazikufanya kazi! Nesi hapa ameongopa. Na huu ni uongo wa kishetani wenye kupelekea mauti ya mwanadamu mwingine.

Naam, tumewekeza katika uongo. Tumekuwa waongo mno. Tubadilike.

Maggid.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment