Saturday, 7 September 2013

[wanabidii] Re: [Mabadiliko] Uchambuzi Wa Habari; Spika Ndugai Ameyakoroga..!

Maggid bwana, sijui umabadiliko na busara ndani ya kj huwa anaviona
kutumia darubini gani? Hakuna mswada wa serikali unatinga bungeni bila
baraka za rais Mjengwa. Busara zinazotakiwa sasa ni zangu, zako na
wengine walio nje ya mfumo ovu, kurekebisha mambo. Kama ni kusubiri
busara za rais basi kihama ndugu yangu

On 9/7/13, Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:
> Ndugu zangu,
>
> Kwenye Daily News ya leo kuna habari hiyo ( Pichani) yenye kuhusiana na
> Muswaada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
>
> Ukiyaangalia yaliyotokea ndani ya Bunge hivi majuzi na hatimaye muswaada
> husika kupitishwa kama ulivyopitishwa jana, basi, kwa mtazamo wangu,
> ninachokiona ni kuwa, inahitajika busara ya ziada kuokoa jahazila Katiba
> kuzama. Maana, haionekani vema kwa Muswaada kupitishwa ukishuhudiwa na
> wabunge watatu tu wa upinzani. Wengine wote wameususia.
>
> Na hapa ninayemwona anaweza kuingilia kati na kuokoa jahazi hili ni Rais
> mwenyewe; Jakaya Kikwete.
>
> Maana, watu wazima tukubali, kuwa pamoja na kupitishwa muswaada husika,
> nyuma yake umeacha manung'uniko yatakayosalia kwa miaka mingi na hivyo
> basi, kutia doa kubwa mchakato huu mwema ambao Rais wetu aliuasisi,
> akausimamia na umeleta matumaini ya kufungua ukurasa mpya kwa nchi yetu kwa
> miaka mingi ijayo.
>
> Maana nahofia pia, kuwa ni heri kuwamo kwenye jahazi hili Wazanzibar wengi
> walioridhia kuliko Wazanzibar wengi wenye manung'uniko. Wenye kunung'unika
> wanaweza kutoboa jahazi na chombo kikazama. Na wao wenzetu wanaweza kuamua
> kuogelea kivyao.
>
> Hivyo basi, hayo yenye kufafanulika yafafanuliwe, kwa uwazi, na hata
> ikibidi, kwa muswaada kurudishwa tena Bungeni kabla ya Rais kuusaini ukawa
> sheria. Kama tumetoka mbali kwenye safari yetu hii, ni kwa nini basi
> tuogope kusimama na kurudi nyuma kidogo ili tuinyoshe njia yetu
> iliyopinda.
>
> Tuchukue mfano, lile la vurugu mechi ya majuzi Bungeni lingeweza kuepukwa
> kama Spika Ndugai naye angeliendea kwa taratibu na bila jazba. Maana,
> waliotaka kuongea wangeongea.
>
> Na kama kuna aliyekaidi jambo Spika angemwacha na kumpa adhabu ambayo
> ingeanza kutumika katika vikao vilivyofuatia. Na kukaidi kwa muhusika
> kungekuwa na maana tu ya muhusika kupoteza kisiasa badala ya kupata zaidi,
> maana, adhabu ingefuatia, na jambo lisingekuwa kubwa vile la mpaka kuitwa
> polisi ndani ya ukumbi wa Bunge. Na polisi wale wangefanyaje maana nao
> wamejiona wako kwenye shinikizo.
>
> Hakika, yaliyotokea ndani ya Bunge ni mambo ya aibu na wananchi
> tusingependa kuyaona tena. Hata kama yanafanyika kwa wengine, lakini si
> utamaduni wetu.
>
> Na hili la nafasi ya Spika na yanayotokea Bungeni linasisitiza umuhimu
> ambao tayari Tume ya Warioba imeshauona, wa kuwa na Spika na Naibu wake
> wasio wanachama wa vyama vya siasa.
>
> Maana, ni vigumu pia kwa Spika, ambaye pia ni Mbunge, kwenda kinyume na
> matakwa ya chama chake. Anahitaji kuwa na ujasiri wa kuwa na misimamo yake.
> Na hatari yake, hutokea kwa Spika hata kuonekana anajipendekeza kwa chama
> chake.
>
> Naam, bado tuna nafasi ya kurekebisha kasoro iliyojitokeza kwenye safari
> hii muhimu kwa nchi yetu. Safari ya kutengeneza Katiba Mpya kwa miaka 50 na
> zaidi ijayo. Hivyo basi, ni safari inayotutaka kutoangalia maslahi ya vyama
> na watu, bali ya taifa.
>
> Mungu Ibariki Tanzania.
> Maggid Mjengwa,
> 0754 678 252
> http://mjengwablog.com
>
> --
> Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
> Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda;
> mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
> Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
>
> TEMBELEA Facebook yetu:
> http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
>
> For more options, visit this group at:
> http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Mabadiliko Forums" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
> To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
> Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment