Kama kawaida Mjengwa anaficha rangi yake ndani ya mistari hajui tuna
darubini kali. Busara alikosa spika wala si hao warusha masumbwi, na
huyo na kanuni zake ndio wa kujadili
On 9/6/13, Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:
> Ndugu zangu,
>
> Hivi Watanzania ni watu wenye kupenda ' Vurugu Mechi'? Maana, magazetini
> leo habari kubwa na picha ni ' vurugu mechi' bungeni.
>
> Ni picha ya aibu. Shabaan Robert alipata kuandika, tena miaka 50 iliyopita,
> kuwa isifike mahali wazungu wakarudi wakatukuta bado hatujamulikiwa na
> nuru, kwamba Waafrika bado tunapigana hadharani!
>
> Shaabani Robert alikuwa na maana ya kuwa hayo ni mambo ya kishenzi na
> hayapaswi kufanywa na watu wastaarabu.
>
> Na afadhali wasomaji wa magazeti kwa lugha ya Kizungu leo hawakuonyeshwa
> picha za sisi Waafrika tulivyo hata baada ya miaka 50 ya uhuru. The Citizen
> na Daily News wao walipamba sura za mbele za magazeti yao kwa habari kubwa
> ya JK na PK ( Kikwete na Kagame) walivyokutana Kampala jana.
>
> Habari za aibu ya bungeni zilipewa nafasi ya pili tena bila picha. Pongezi
> kwa wahariri wa magazeti hayo kwa kutufichia aibu yetu.
>
> Na Daily News wao wametoka na kichwa kizuri cha habari; " MPs, police in a
> shameful flurry of fists"
>
> Kwa kweli ni aibu. Kwa nini tumefika mahali hapa? Kwamba watu wazima
> Bungeni wasitumie mazungumzo katika kumaliza tofauti zinazojitokeza badala
> ya kushikana mashati, kuburuzana na hata kupigana makonde.
>
> Na mitaani leo kona nyingi nimewasikia watu wakizungumzia ' Senema ya jana
> Bungeni'. Na kilichowavutia sana ni hiyo ' Vurugu mechi' na hususan
> masumbwi na kupigana ngwala!
>
> Na wengi hawakujikita kwenye nini hasa msingi wa vurugu mechi hiyo.
> Wamefurahishwa tu na ' Vurugu mechi', basi! Na hakika, magazeti
> yaliyopambwa na picha za vurugu mechi ile leo yameuzwa ' kama njugu'.
>
> Na bwana mmoja mtaani nimemsikia akitamka; " Sasa tunataka kuona masumbwi
> ya wabunge wa upinzani dhidi ya wa CCM!"
>
> Tumefika pabaya, kwamba habari za aibu za watu wazima kupigana na kushikana
> mashati hadharani ndizo zinazowavutia wasomaji watu wazima!
>
> Hivi watoto wetu tunawafundisha nini?
>
> Kwamba katika nchi hii unaweza kuwa maarufu na hata ukafika mbali kwa
> kurusha ngumi badala ya kuwa na uwezo wa kujenga hoja kwa kutumia kichwa,
> mdomo au kalamu.
>
> Si tunajua, tuna hata mwanasiasa katika nchi hii aliyerumshia ngumi
> mwanahabari hadharani, na tangu siku hiyo akajipatia umaarufu na hata
> kupewa jina la ' Tyson'!
>
> Ndio, ni katika nchi zetu hizi za hovyo hovyo ambapo ngumi zinaweza
> kukupeleka hata IKULU!
>
> Usiku Mwema.
>
> Maggid.
> Dar es Salaam.
>
> --
> Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
> Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda;
> mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
> Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
>
> TEMBELEA Facebook yetu:
> http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
>
> For more options, visit this group at:
> http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Mabadiliko Forums" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
> To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
> Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment