Thursday, 19 September 2013

[wanabidii] Re: [Mabadiliko] Happy Birthday Mjengwablog; Miaka Saba, Na Tunasonga Mbele...!

Hongera sana mwenyekiti kwa miaka saba. nami nafarijika moyoni kuwa
mmoja wa waliochangia jasho langu katika blog yetu hii. nikiwa
msaidizi wa mwenyekiti tangu october 2011 hadi niliposimamishwa
ghafla.
ni kweli kazi ya blog ni ngumu na yenye changamoto nyingi.inabidi
kuamka saa kumi na moja alfajiri na labda kulala sasa 6 usiku. haina
week end wala sikukuu.mjengwablog imejitahidi sana kutoa picha halisi
ya maisha ya watu wa kawaida tangu kyaka hadi nyeregete.
na wapo wenye kutaka blog iandike wanayotaka na wanavyotaka wao.ni
changamoto. katika uwepo wangu mjengwablog na sasa nikiwa
nimesimamishwa wakati wa matatizo haya nimejifunza mambo mengi juu ya
maisha na watu tulivyo.ni changamoto hizohizo anazosema mwenyekiti.
hongera sana mjengwablog kwa kutimiza miaka saba.

On 9/19/13, Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:
> Ndugu zangu,
>
> Kwa mwanadamu, hakupaswi kuwapo na ukomo wa kujitahidi kufanya yalo mema
> kwa jamii yako.
>
> Na katika kujitahidi kuyafanya yalo mema, basi, mwanadamu uwe tayari
> kukumbana na changamoto nyingi. Na kama ilivyo kwa maji ya mto,
> yanapokutana na mwamba, basi, kasi yake huongezeka maradufu.
>
> Leo blogu yako hii ya Mjengwablog imetimiza miaka saba. Miaka saba si haba.
> Ni umri wa mtoto kuanza shule.
>
> Kwa niaba ya timu nzima ya Mjengwablog nachukua fursa hii kuwashukuru kwa
> dhati ' WanaFamilia' wote wa Mjengwablog kwa kuwa nasi katika hali zote.
> Hivyo basi, kutuunga mkono.
>
> Naam, ni miaka saba ya kuwa mtandaoni karibu katika kila siku inayotujia na
> kupita. Ni miaka saba ya mapambano magumu ya kuitumikia jamii na
> kuhakikisha kuwa tunabaki hai.
>
> Maana, unapoamua kuitumikia jamii bila kuegemea upande, basi, ina maana
> pia ya kujiweka katika mazingira ya hatari sana. Yumkini kuna maua mengi
> ya upendo yanaweza kurushwa kwako, lakini, kuna mishale michache ya sumu
> ambayo pia itarushwa kwako. Kwamba kuna maadui pia.
>
> Na ukimwona nyani ametimiza miaka saba , basi, ujue kuna mishale kadhaa
> ameikwepa. Lakini, na anavyozidi kuendelea kuishi, yumkini kuna mishale
> mingine inaandaliwa. Na nyani hatakiwi kuishi kwa kuogopa mishale ya
> wanadamu. Vinginevyo, ajitundike mtini, afe.
>
> Lililo jema na kutia faraja ni kutambua, kuwa kuna walio wengi wenye
> kufaidika na kazi hii ya kijamii ambayo Mjengwablog inaifanya. Ni hawa
> ndio wenye kututia nguvu ya kuendelea kuifanya kazi hii pamoja na
> changamoto zake nyingi.
>
> Ndugu zangu,
>
> Ilikuwa ni Jumanne, Septemba 19, 2006. Ni siku hiyo ndipo kwa mara ya
> kwanza niliingiza picha ya kwanza kwenye mjengwablog na kuashiria uzinduzi
> wa blogu. Ni picha hiyo inayoonekana hapo juu. Niliipiga eneo la Kinondoni
> Shamba. Tangu siku ya kwanza, niliweka wazi kwenye fikra zangu, kuwa
> Mjengwablog iwe jukwaa litakalomtanguliza mtu wa kawaida. Iwe sauti ya wale
> ambao sauti zao hazisikiki.
>
> Na Mjengwablog ikawa chachu ya kuanzishwa kwa gazeti la michezo na burudani
> la ' Gozi Spoti', ikawa chachu pia ya kuanzishwa gazeti la ' Kwanza Jamii'.
>
> Na kuna miongoni mwetu wenye kufikiri, kuwa mwenye kumiliki gazeti ni
> lazima awe Mhindi au Mtanzania ' mweusi' Mfanyabiashara tajiri. Nakumbuka
> kuna hata ambao hawakuwa tayari kuchangia kiuandishi kwenye ' Gozi Spoti'
> na ' Kwanza Jamii' kwa vile linamilikiwa na ' Mswahili mwenzao!'Na hata
> kupata matangazo kukawa na ugumu mkubwa. Gozi Spoti lilisimama kuchapwa
> baada ya mwaka mmoja mitaani. Kwanza Jamii, nalo likasimama kuchapwa.
> Likarudi tena baada ya kuingia ubia na Shirika la Daraja. Baada ya miaka
> miwili na baada ya aliyepelekea kuingia ubia kuondoka nchini na kurudi
> kwao Uingereza, basi, Kwanza Jamii nalo ' likaandaliwa' mazingira ya
> kuondoka mitaani.
>
> Hata hivyo, Kwanza Jamii, gazeti dogo, ambalo naamini ni muhimu kwa
> jamii, limerudi tena kupitia mtandaoni. Mipango iko mbioni kuliimarisha
> zaidi katika siku zijazo.
>
> Ndugu zangu,
>
> Changamoto zipo ili tukabiliane nazo, na si kukata tamaa. Mjengwablog
> inatimiza miaka saba leo kwa vile tulishaamua, kuwa tutapambana hadi
> risasi ya mwisho. Hivyo pia, tutapambana hadi pumzi ya mwisho.
>
>
>
> Maana, tunaamini kuwa kazi tuifanyayo ni yenye manufaa kwa jamii pana. Na
> tuna haki ya kuifanya. Tunavumilia sauti zenye kutushutumu na kutukosoa.
> Kuna tunayojifunza kutoka kwa wakosoaji wetu. Tunawashukuru sana na
> tunawaomba waendelee kutukosoa kila wanapoziona kasoro.
>
> Lakini, kuna wachache pia wenye kuonyesha zaidi chuki kuliko kukosoa.
> Hawaipendi
> kazi tuifanyao wala kuithamini, ni kawaida. Lakini, faraja ni kutambua kuna
> wenye kuipenda na kuithamini kazi yetu.
>
> Hapa chini ni mmoja wa watu hao;
>
> *Maggid,**
> Iringa.*
>
> *Wow. Siamini kama ni miaka saba tu. Mjengwa Blog was the first TZ blog
> that really hooked me. And it is still hooking me. In a blogging world
> fixated with celebrity, gossip and slander, Mjengwa Blog is a rare and
> fresh piece of sanity with a window ont**o the real Tanzania. Bravo Mwenye
> Kiti, umefanya kazi kubwa hadi hapo ulipo. Na wala usipate wazo lolote lile
> la kustaafu. Wanakijiji wenzako bado tunakuhitaji na kukutegemea uendelee
> hivyo hivyo. Aluta continua...*
>
> * *
>
> *Jimmy Innes ( UK)*
>
>
>
> Ahsanteni sana.
>
> Maggid Mjengwa.
>
> Mwenyekiti Mtendaji.
>
> Mjengwablog.com
>
> --
> Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
> Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda;
> mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
> Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
>
> TEMBELEA Facebook yetu:
> http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
>
> For more options, visit this group at:
> http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Mabadiliko Forum" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
> To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
> Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment