Ndugu zangu,
Bado inaunguruma milio ya ' ngoma za vita' kwenye Ukanda wetu wa Nchi za Maziwa Makuu.
Ngoma hizi ni za kuzimwa haraka kabla ya waliomo na wasiomo wakalazimishwa kuchanganyika kucheza. Na hakika ni ngoma ya vita vya kiwendawazimu.
Mama Mary Robinson, Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Nchi za Maziwa Makuu ametua kwenye ukanda wetu. Ana ujumbe mmoja tu katika kupata suluhu ya vita ya Congo; MAZUNGUMZO.
Na kawaida ya wanadamu hawazungumzi kulimaliza jambo wakiwa wamesimama. Huitafuta MEZA. Ndio, meza ya mazungumzo. Yaweza kuwa meza ya duara au mstatiri, lakini, lililo muhimu ni MEZA.
Kabla ya ujio wa Wareno hatukuwa na neno meza. Hili ni neno la Kireno, linatamkwa ' Mesa'.
Mama Mary Robinsson anatukumbusha umuhimu wa MEZA. Na ni ukweli, kuwa kwenye mgogoro wowote mwanadamu ni nadra sana akaikimbia meza ili kupata suluhu ya mgogoro. Maana, hata ukipigana vita, bado utaihitaji meza kumaliza vita.
Wenye kupiga na kufurahia ' ngoma za vita' hawajapendezwa na msimamo wa Mama Mary Robinson. Wao wanataka ' Vita ipiganwe leo' wakiamini shughuli yote inaweza kuisha kesho.
Hawajui, kuwa Mama Mary Robinson anaposhauri Serikali ya DRC Congo izungumze na M23 kuwa ana uelewa mpana na wa kina wa historia ya Congo. Kimsingi M23 ni tone tu kwenye dimbwi la matatizo ya Congo yenye chimbuko la kihistoria.
Tusingependa kuona tena mamilioni ya raia wasio na hatia na hususan akina mama na watoto wakitembea maelfu ya kilomita kukimbia makazi yao. Kuishi ukimbizini ndani na nje ya mipaka ya Congo. Tusingependa tena kusikia maelfu kwa maelfu ya akina mama na watoto wakibakwa mchana wa jua kali kwa sababu ya vita. Tusingependa kuona picha za raia wasio na hatia wakiuawa au kujeruhiwa kwenye vita vya kiwendawazimu. Vita ambavyo vingeweza kuepukwa kama hekima na busara ingetangulizwa.
Ni imani yangu, ni imani ya wengi pia, kuwa juhudi za Mama Mary Robinson za kuzikutanisha pande zote kwenye meza ya mazungumzo zitazaa matunda.
Na kwa kuanzia, tunataraji Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi za Maziwa Makuu unaotarajiwa kuanza kesho pale Kampala utafanyika, na hivyo, kuwa hatua ya kwanza muhimu kwa wahusika kuikaribia meza.
Mungu Ibariki Afrika.
Maggid.
Iringa.
0754 678 252
http://mjengwablog.comhttp://mjengwablog.comBado inaunguruma milio ya ' ngoma za vita' kwenye Ukanda wetu wa Nchi za Maziwa Makuu.

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment