Saturday, 7 September 2013

[wanabidii] Ezekiel Maige - Sifurahishwi na yanayoendelea Bungeni

Wapendwa, watanzania wenzangu. Nimetazama kwa mshangao na kutoamini kuhusu kilichojiri Bungeni jana. Kwa Bahati mbaya, binafsi sikuwepo niko Arusha kwenye mkutano wa Ushirika wa Wabunge wa Kamati za Mahesabu ya Serikali kutoka Nchi za SADC (SADCOPAC) na Nchi kadhaa za Africa nje ya SADC. 

Sikuona Sababu kabisa ya kufikia hapo kwani hali hiyo ingeweza kuepushwa. Ingewezekana kabisa kuahirisha muswada na kutoa nafasi kwa Kamati ya Katiba na Sheria kwenda Zanzibar kupata maoni ya wenzetu wa huko.

Najua kuna maelezo mazuri ya kushirikishwa kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Lakini kikanuni, Baada ya Muswada kusomwa mara ya kwanza, unakuwa mikononi mwa Bunge na Kamati ndiyo inayokusanya maoni si Serikali! 

Kwa kuwa hakuna ushahidi wa public hearing kufanyika Zanzibar na kuwasikia wazanzibari wa kawaida (nje ya serikali), basi kulikuwa na Hoja kabisa ya kurekebisha kasoro hiyo kwa kutoa nafasi kwa Kamati kwenda Zanzibar. 

Suala la Katiba ni kubwa hivyo ni vema zikafanyika jitihada za kutosha kuhakikisha tunakwenda pamoja (na wenzetu hasa wenye mtazamo tofauti na Sisi) badala ya kutumia uwingi wetu kwani Mwisho wa safari tukienda Hivi wapo watakaodai Katiba mpya si yao na hivyo kuikosiesha social legitimacy!

Kwa kiti kutomsikiliza KUB nako kulitibua mambo bila sababu. Angepewa nafasi ya kusikilizwa Hata kama Hoja yake isipokubaliwa ingekuwa nafuu sana na shari na aibu ya jana ingeepukika! 

Tumesameheana, lakini tujifunze na tujitahidi sana kwenda kwa maelewano.

Mungu ibariki Tanzania.

Ezekiel Maige,
Mbunge wa Msalala.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment