--Habarini za asubuhi,
In fwact, nakubaliana na YM na EM "ät the same time",kwa kiasi fulani.
Haitokei watu wa Ulaya, hata watu wa kawaida, wanapotembelea kwa mfano nchi yetu, ukawasikia "wakizinanga" serikali za kwao. Hata zile tunazozifahamu kwa ubabaishaji km Italy au zile kandamizi kama Korea au China.
Ukiacha mabavu ya hizo nchi mbili za mwisho, wenzetu wana taratibu zao zinazotawala uendeshaji wa siasa za nchi. Ukivurunda, unaondoka kwa ama hiari, au kwa kupitia kura. Ebu fikiria, nchi inapokumbwa na matatizo, kipimo cha uthabiti wa serikali ni kupitia uchaguzi wa dharura (snap elections). Hili serikali za huko hazina nguvu wala namna ya kulikataa.
Majeshi, mahakama na taasisi zote za umma au za dola, ni mali ya wananchi na sio wanasiasa/serikali.Mazingira haya hushamirisha uhuru wa kweli, na ndugu zetu hao, hawahangaiki kupita wakibeza serikali zao. Kwanza zinaongoza kwa kufuata taratibu walizokubaliana na kujiwekea. Anayetoka nje ya mstari, yeye na chama chake wanatimuliwa.
Yote niliyoyataja hapo juu huku kwetu ni kinyume. Chinua Achebe aliandika jinsi wanaijeria wawili au watatu kila baada ya kusalimiana hujikita katika kujadili nakisi zao za kitaifa, kama ambavyo waingereza wanavyoongelea hali ya hewa! Hivi Maro hili hulioni hapa kwetu? Panda kwenye daladala au pitia sehemu zenye mikusanyiko, km Mwenge, Tungi, nk.
Wole Soyinka akasema ni jinai kukaa kimya wakati mambo ndani ya nchi hayaendi sawa.
Haina sababu ya kuwasimanga wapinzani ili wasiongelee mapungufu ya serikali. Hiyo haswa ndio kazi ya upinzani, na kuipigia makofi na kuishangilia, ni kinyume cha wajibu huo. Watu wanapoongelea matatizo yao, haina maana wamekosa uzalendo. Wanaangalia fursa za kuondoka hapo walipo.Wapinzani wanachofanya ndiyo njia pekee itakayowawezesha kuingia madarakani kwa njia sahihi. Wasipofanya hivyo, wataingiaje madarakani. Kwa kupindua nchi?
"The man dies in him who remains silent when things in the country go astray" Wole Soyika. "The Man Died"
Ndio nimeingia,
MJL
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment