Friday, 20 September 2013

Re: [wanabidii] WATANZANIA NA HUJUMA DHIDI YA NCHI YAO

umesema kweli

Wole Soyinka alisema vizuri sana na waTz wanapaswa kulielewa hili: "ni jinai kukaa kimya wakati mambo ndani ya nchi hayaendi sawa". FIKIRI: Mchanga unasafirishwa nje, wanyama hai wanaibiwa kupelekwa nje, takribani tembo 30 wanauawa kila siku na pembe za ndovu zinasafirishwa nje, madini yanaibiwa/kutoroshwa nje, mikataba ya hovyo, utoroshaji wa fedha kwenda kuficha kwenye mabenki ya nje uko juu na watawala wetu wanajua na wanaambiwa - wako kimya! misamaha ya kodi kwa wageni kibao, ufisadi, rushwa ndiyo usiseme, mauaji ya raia k.m waandishi wa habari, kuvamiwa, kuumizwa na hata kuuawa kwa viongozi wa dini, kumwagiwa tindikali, kukandamizwa kwa demokrasia, umasikini limekuwa ni jambo la kujivunia, elimu imeshuka na asilimia ya ujinga kuongezeka, dhuruma kwa haki za binadamu k.m pension za wazee wa iliyokuwa afrika mashariki n.k., mahakama nazo zimekufa ganzi - siasa mpaka mahakamani, wezi wakubwa wa rasilimali za nchi hawafungwi badala yake wanawombwa warudishe tu walichoiba kwa wakati wao, madawa ya kulevya limekuwa jambo linalogeuzwa geuzwa tu - hatua mathubuti na za haraka hazichukuliwi utadhani ni jambo la heri! tunaambiwa majina ya wauza unga wanayo na tumesikia wakubwa wakisema "majina yakitajwa waheshimiwa wabunge hawaponi!" - ni hatua zipi zinachukuliwa na za haraka dhidi yao- hakuna, na taifa linaangamia! watu wanyamaze? wasiseme? kusisitiza kunyamaza wakati taifa linaangamia ni dalili ya adui ujinga kutawala na adui umasikini  aongezeke ili tuzidi kuwa wombawomba na kuendelea kupigia magoti mafisadi wachache wa ndani kama siyo mabeberu wa nje wanaoiba rasilimali zetu kupitia mikataba ya ovyo iliyowekwa na wenzetu - waTz wenzetu tuliowaamini na kuwapa mamlaka watuongoze - wamesahau cheo ni zamana, wamesahau kabisa! taifa linaangamia, watu wakae kimya! wasiseme! tunavunja katiba 1977 28 (1); 30 (2) (b).

From: mngonge <mngonge@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Friday, September 20, 2013 9:52 AM
Subject: Re: [wanabidii] WATANZANIA NA HUJUMA DHIDI YA NCHI YAO

Tuliowaamini ndiyo wahuhujumu wakuu wa nchi yetu. Mtu anaposaini mkataba na mwekezaji wakapeana ten percent kwa hasara ya walalahoi wa nchi hii. Na kisha fedha hiyo akaificha ulaya, mtu huyo ni mtumwa kwa huyo aliyempa fedha hata kama madaraka yake ni makubwa. Pia mtu akiisha kuwa ombaomba ni vigumu sana kuwa na siri maana una shida na anayetaka kukusaidia lazima umridhishe kwa kulieleza tatizo lako na hata kumuelezea kisa na mkasa cha tatizo.

Tukumbuke dunia ya leo ni kijiji, matukio mengi kama vile wanapopigana wakulima na wafugaji ulimwengu mzima unayaona kupitia satelite, sijui hizo nazo tunaziita siri?. Tuache kuwasingizia wakuliama na machinga wetu kwamba hawana uzalendo au wanatoa siri nje, wanaotoa siri nje ni hao hao tuliowaamini.

Watanzania wa kawaida (walalahoi) hawana siri yoyote ambayo wazungu hawajui hawa jamaa wanatujua vizuri sana kupitia viongozi wetu, tafiti, shida tulizonazo na mengine mengi. Uzalendo hauwezi kuwepo kama tofauti ya tajiri na maskini ni kubwa sana na kama hakuna demokrasia na utawala wa kisheria. Nchi yenye watu wanaopenda virushwa rushwa ni vigumu sana kuwa na siri au uzalendo. Tunakotaka kufika ni huko kwenye uzalendo na nchi yetu lakini wanaohubiri kwenda huko ndo wanaoweka vikwazo. Tusiwasingizie wapinzani, kwani hata wasiposema dalili zote zinaonyesha tuendako si kuzuri kama vile umaskini na njaa,  hizo zinazoitwa siri havitajulikana kwa watu wa mataifa mengine.

2013/9/19 ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com>
Mtu mmoja ametoka Mouritious (sp?) akaniambia jinsi nchi ile ilivyoendelea wakati haina raslimali zinazoeleweka nikashangaa. Viongozi wetu wanahangaika kwenda Marekani ambako uchumi wake hatuwezi kuuiga kwanini wasiende kujifunza huko?
Sisi tuna raslimali nyingi za kuendeleza nchi yetu kwa nini bado tunaombaomba mpaka Obama aje aseme mfanye hivi?
Kwahiyo:
1) Watanzania wanaolalamika sio kuwa sio wazalendo hapana wana sababu ya kusema na ni haki kuwasamehe wakisemea pasipostahili.
2) Wanaotoka nje na kutusemea mazuri waongo au wana lao. Wanajua kuwa Tanzania haifaidi dhahabu zake. Pwani yake (Bandari), Mbuga zake. tena wabaya kuliko wanaotutukana maana wanatusifu kuwa tumeendelea wakati wanatusaidia chakula badala ya Tracta kulima ardhi yetu yenye rutuba. Wanatumia pamba yetu kututengenezea vyandarua. Wanaona jinsi tusipoelewa sera nzuri na tunazikataa kwa sababu zimetolewa na wapinzani. hatuwezi kuwashukuru kwa kutusifu ila tukiona mwanzo wa masahihisho na kuhakikisha ufisadi unakoma basi atakayetusema vibaya tumzomee. kabla ya hapo huwezi

From: mutabaazi lugaziya <mjlugaziya@mail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, September 19, 2013 9:41 AM
Subject: Re: [wanabidii] WATANZANIA NA HUJUMA DHIDI YA NCHI YAO

Habarini za asubuhi,
 
In fwact, nakubaliana na YM na EM "ät the same time",kwa kiasi fulani.
 
Haitokei watu wa Ulaya, hata watu wa kawaida, wanapotembelea kwa mfano nchi yetu, ukawasikia "wakizinanga" serikali za kwao. Hata zile tunazozifahamu kwa ubabaishaji km Italy au zile kandamizi kama Korea au China.
 
Ukiacha mabavu ya hizo nchi mbili za mwisho, wenzetu wana taratibu zao zinazotawala uendeshaji wa siasa za nchi. Ukivurunda, unaondoka kwa ama hiari, au kwa kupitia kura. Ebu fikiria, nchi inapokumbwa na matatizo, kipimo cha uthabiti wa serikali ni kupitia uchaguzi wa dharura (snap elections). Hili serikali za huko hazina nguvu wala namna ya kulikataa.
 
Majeshi, mahakama na taasisi zote za umma au za dola, ni mali ya wananchi na sio wanasiasa/serikali.Mazingira haya hushamirisha uhuru wa kweli, na ndugu zetu hao, hawahangaiki kupita wakibeza serikali zao. Kwanza zinaongoza kwa kufuata taratibu walizokubaliana na kujiwekea. Anayetoka nje ya mstari, yeye na chama chake wanatimuliwa.
 
Yote niliyoyataja hapo juu huku kwetu ni kinyume. Chinua Achebe aliandika jinsi wanaijeria wawili au watatu kila baada ya kusalimiana hujikita katika kujadili nakisi zao za kitaifa, kama ambavyo waingereza wanavyoongelea hali ya hewa! Hivi Maro hili hulioni hapa kwetu? Panda kwenye daladala au pitia sehemu zenye mikusanyiko, km Mwenge, Tungi, nk.
 
Wole Soyinka akasema ni jinai kukaa kimya wakati mambo ndani ya nchi hayaendi sawa.
 
Haina sababu ya kuwasimanga wapinzani ili wasiongelee mapungufu ya serikali. Hiyo haswa ndio kazi ya upinzani, na kuipigia makofi na kuishangilia, ni kinyume cha wajibu huo. Watu wanapoongelea matatizo yao, haina maana wamekosa uzalendo. Wanaangalia fursa za kuondoka hapo walipo.Wapinzani wanachofanya ndiyo njia pekee itakayowawezesha kuingia madarakani kwa njia sahihi. Wasipofanya hivyo, wataingiaje madarakani. Kwa kupindua nchi?
 
"The man dies in him who remains silent when things in the country go astray" Wole Soyika. "The Man Died"
 
Ndio nimeingia,
 
MJL
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment