Ndugu Hamisi.
Naona umelalamika na ukajitahidi kumpakazia Mengi badala ya kujibu hoja zilizoletwa hadharani na sina uhakika kama zililetwa na Mengi tu.
Nakumbuka vyombo vya habari kumnukuu waziri wa Madini na nishati akitamka tamko ambalo usipoliongelea huwezi kueleweka. Eti waTanzania hawana mtaji wa kuwekeza kwenye mafuta na gesi kwa hiyo hana muda wa kuwasikiliza ila waendeelee kuwekeza katika juice na matunda. Kauli hii usipoijibu utaishia kumsafisha Mengi badala ya kumchafua.
Nakumbuka kumsikia Mengi na CEO wa TPSF wakisema kwakuwa serikali ni sikivu itasimamisha ugawaji wa vitalu vya mafuta na gesi ili kwanza (serikali) iandae sera ambayo itaonekana kuwanufaisha waTanzania pia. Mengi alisema Serikali zote duniani huwapendelea wananchi wake hasa katika mambo ya mali asili kama madini. (Kosa la Mengi ni lipi hapo).
Kuna haraka gani serikali kutoa vitalu hivyo sasa badala ya kuandaa sera itakayowanufaisha watanzania?
Kama kwa mfano tanzania ikatunga sera isemayo watanzania wakiungana na kukusanya kiasi fulani cha fedha (serikali) itawadhamini mkopo katika taasisi za fedha za nje na itasimamia uchimbaji hadi mkopo umelipwa.
Au Mtanzania mwenye dhamana kiasi fulani anaweza kudhaminiwa kuwa na hisa katika mradi wa muwekezaji wa nje. au
Gesi ina hisa asilimia kadhaa; muwekezaji kutoka nje aungane na mtanzania kuchimba gesi hiyo na asilimia hizo zitauzwa kwa mtanzania atakayetoa kiasi kadhaa ch pesa.
Unafikiri huyu jamaa wa TPDC alikuwa sahihi katika kusema watanzania hawawezi wana ubinafsi bila sera ambayo Mengi anaiomba? Hivi nani aliwachagua wa tabia hiyo akawarundika Tanzania na waKenya kwao? Mimi nafikiri Serikali ijilaumu kwa watu wake kukosa elimu hiyo ya ushirikiano na ichukue hatua.
Unakumbusha habari za Kilimanjaro hotel ambapo inasemekana Mengi aliomba kuuziwa hoteli hiyo lakini akanyimwa kwa kutotoa chochote na hoteli hiyo kuuziwa mwanasiasa toka nchi jirani?
Sina uhusiano na Mengi wala hatufahamiani. Lakini naona unataka kufanya watu wamthamini wakiyasoma unayoyaandika bila kujibu hoja. Kumbuka walimsikiliza kama ulivyomsikiliza.
Lakini Mengi anafahamika sana kwa kuwatetea wanyonge. Kumbuka ni wengi licha ya unyonge wao. Kama anadhamini kongamano hilo kupitia CHADEMA si dalili ya uhalifu ila wa\tetezi wa wanyonge wanaanza kuungana. Kuwatenganisha ni serikali kuwa na busara naq sikivu kama walivyosema.
Elisa Muhingo
From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Saturday, September 7, 2013 7:25 PM
Subject: [wanabidii] Ubinafsi, Chuki, fitina na ufisadi wa Reginald Mengi kwenye Maendeleo
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Saturday, September 7, 2013 7:25 PM
Subject: [wanabidii] Ubinafsi, Chuki, fitina na ufisadi wa Reginald Mengi kwenye Maendeleo
Hivi karibuni kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa baadhi ya watanzania dhidi ya Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini Mhe. Prof Sospeter Muhongo yakiongozwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) ambae pia ni Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Bwana Reginald Mengi. Malalamiko hayo ambayo yameendelea kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari na kupelekea hata baadhi ya wahusika kutoka wizarani, Idara na Mashirika yake kutakiwa kujibu na kutolea ufafanuzi malalamiko na tuhuma hizo nzito dhidi yao. Moja ya vyombo hivyo ni gazeti la NIPASHE linalomilikiwa na IPP media la tarehe 6 septemba, 2013 katika ukurasa wake wa tatu kuna habari inasema "SERIKALI YAZIDI KUPUUZA USHAURI WA TPSF" Inaeleza habari hiyo kuwa " ..Wakati taasisi ya sekta binafsi (TPSF) ikiishauri kuharakisha sera ya gesi badala ya ugawaji vitalu, serikali imeendelea kupuuza ushauri huo na sasa kupitia Shirika la maendeleo ya petroli Tanzania (TPDC) imetangaza rasmi kuharakisha suala hilo kwa madai ya kuwahi ushindani wa masoko ulimwenguni.."Lakini TPDF nao katika gazeti la UHURU la jana Ijumaa katika ukurasa wake wa tatu imeandikwa habari yenye anuani "MWENYEKITI TPDC: UBINAFSI UNAWAPONZA WATANZANIA. Wengi wanalalamika uwezo hawana, zabuni za vitalu mwezi ujao." katika habari hiyo Mwandishi ameandika kuwa "Mwenyekiti wa Bodi
ya wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) , Michael Mwanda, amesema ubinafsi miongoni mwa watanzania ndio unaowafanya washindwe kunufaika na fursa za kiuchumi zilizopo nchini, zikiwemo mafuta na gesi. Mwanda alisema hayo jana jijini Dar es salaam, alipokuwa akijibu moja ya maswali ya waandishi wa habari juu ya malalamiko ya baadhi ya watanzania kuwa hawapewi nafasi kushiriki katika utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi."Malumbano hayo kupitia vyombo vya habari baina ya pande mbili yaani Mengi na IPP yake na Muhongo na Mashirika yake ambayo yamedumu kwa muda, sasa yanachukua sura mpya baada ya kuwepo kwa taarifa za chini chini kuwa Mwenyekiti huyo wa TPSF na IPP ameandaa mpango wa kuwatumia vijana wa Chama Cha Siasa cha Upinzani (CHADEMA) kufanya kongamano lenye maudhui "rasilimali za nchi na manufaa kwa wazalendo" ambapo kongamano hilo limepangwa kupewa airtime katika kituo maarufu cha television hapa nchini cha ITV ambacho kinamilikiwa na IPP media lakini pia posho, chakula na incentives mbalimbali zimepangwa kutolewa katika Kongamano hilo.Kama ilivyo katika mkakati huo, lengo lililopo nyuma ya pazia la kongamano hilo ni kutaka kuionyesha jamii kuwa Waziri na Wizara kwa ujumla haijali maslahi ya wazawa na kwamba viongozi wakuu wa Wizara husika hawana Utaifa wala Uzalendo (kwa maana ya upendo kwa Taifa) hivyo wanataka kuzitumia nafasi zao ndani ya wizara katika kujitajirisha binafsi na kufanya upendeleo kwa wawekezaji wageni ambao hawana manufaa ya moja kwa moja katika maendeleo ya wananchi.Madhumuni ya andiko langu hili na kuvuta utafakari makini na wa wengi katika suala hili ambalo kama hatua muhimu na za haraka hazitachukuliwa katika kulikabili linaweza kuleta tafsiri hasi kwa jamii na hivyo kuwagawa na kuwavuruga watanzania na hasa kuwafanya wapoteze imani na matumaini yao kwa Serikali, Waziri, Wizara, Idara na Mashirika yaliyopewa dhamana ya usimamizi wa rasilimali za nchi hii.Naomba ikumbukwe kuwa si mara ya kwanza kwa seke seke la aina hii kuzuka ama kuzushwa chini ya uratibu na usimamizi wa Mzee Mengi. Na mara zote amekuwa akitumia nguvu ya ushawishi wa vyombo vya habari anavyovimiliki katika kutafuta kuungwa mkono na hata kuonyesha ubaya wa wabaya wake. Ubaya, malumbano na mizengwe mingi ambayo huzalishwa na kusimamiwa na Mzee wangu huyu asili yake ni Ubinafsi na kuguswa kwa maslahi ya kiuchumi aliyonayo katika Sekta mbalimbali hapa nchini.Hivi karibuni kulizuka sekeseke mfano wa hili la sasa ambalo lilihusu VING'AMUZI na kabla ya hapo TBC, UBINAFSISHAJI WA KILIMANJARO HOTEL, SUALA LA YUSUPH MANJI, SHEIKH AL BASALEHE na katika migogoro yote hiyo Mzee Mengi amekuwa akitumia vyombo vya habari katika kuwakandamiza, kuwazushia, kuwatuhumu na hata kuwadhalilisha wapinzani wake. Nitaomba wanajamvi wakumbuke kuwa Mwaka 2008 kulipokuwepo mgogoro baina ya Mzee Mengi na Al Basalehe, Katika mgogoro huo Mzee mengi alimrubuni Ustadhi Mmoja wa madrasa (jina linahifadhiwa kwa sababu za kimaadili) na kuwatumia wanafunzi wa madrasa hiyo kutunga nyimbo za kaswida za kumdhalilisha Sheikh Al Basalahe na kisha nyimbo hiyo kupewa airtime katika kituo cha ITV, na kwa mfano kama huo akaitumia ITV kuwataja washindani wake kiuchumi kuwa ni MAFISADI PAPA.Sina kumbukumbu kuwa alitumia vigezo gani kuwataja wapinzani wake hao kibiashara kama mafisadi papa, ila kumbukumbu yangu inaniambia aliwataja hadharani na kupelekea baadhi kumpeleka mahakamani na kumfungilia kesi ambazo hata hivyo hazikupata airtime za kutosha kwenye vyombo vya habari na hata mwisho wake haukuwa umefahamika kwa wengi.Tukirudi katika hoja yetu ya vitalu vya gesi ambavyo Mwenyekiti huyo wa IPP na TPSF amekuwa akividai kwa hamu kubwa na kuwatuhumu Viongozi wa Wizara, Wakuu wa Idara na Mashirika yanayohusu Rasilimali gesi na mafuta kuwa hawana hata chembe ya Uzalendo na wabinafsi, nahofu nitaeleweka vibaya kwa baadhi ya watu nikisema kuwa kauli hii haina uhalisia na si ya kweli, na kwamba inalenga kuchochea hisia za chuki na imetolewa kwa misingi ya Chuki, it's simply a hate speech that hate are produced.Kwa mujibu wa TPDC, kuchimba kisima kimoja kwa ajili ya kutafuta gesi na mafuta katika nchi kavu ni dola za Marekani milioni 40 (Tshs. Bilioni 64) na kwa kina kirefu cha bahari ni dola 120 (Tshs Bilioni 190) na pia ili kupata mafuta au gesi baada ya kupata uhakika, mwekezaji anapaswa kuchimba visima vinne hadi vitano, hivyo inahitaji mwekezaji kuwa na mtaji usiopungua dola za kimarekani milioni 600 ~ 800 kiasi ambacho watanzania wengi hawana (MENGI akiwemo) na kwa Kauli ya Mwanda, Mwenyekiti wa TPDC alisema kuwa Watanzania ili waweze kunufaika na rasilimali hiyo, hawana budi kuungana na wabia wenye uwezo wa kimtaji na teknolojia (Suala ambalo Mengi analipinga)Tatizo la kimsingi hapa ni Ubinafsi wa baadhi ya watu ambao wanataka upendeleo kwa maslahi binafsi ya kibiashara kwa nembo ya uzalendo na uzawa. Kumekuwepo na rekodi zenye kusikitisha ambazo zinaonyesha tatizo la msingi linalowakabili hawa tycoon wetu katika mikopo waliyochukua katika mabenki makubwa mbalimbali hapa nchini na hata nje ambapo bado hawajarejesha mikopo hiyo na hivyo kutokopesheka tena kwa miradi mikubwa kama hii ya vitalu vya gesi lakini pia zipo rekodi nyingine zinazoonyesha wametumia mikopo kwa shughuli ambazo hawakuombea mikopo hiyo ikiwemo mikopo kutoka benki ya kilimo (Takwimu zipo)Kama hayo ya mikopo hayatoshi, tayari Kampuni za Mzee Mengi zinashikilia vitalu takribani 59 vya madini vyenye Ukubwa wa mita za mraba 3,752. 37 (sq km) na baadhi ya vitalu hivyo alivyovishikilia ameshindwa kuviendeleza na matokeo yake Serikali inakosa mapato kutokana na kutoendelezwa kwa vitalu hivyo lakini pia watanzania wanakosa ajira na manufaa mengine, najiuliza kama hii ndio tafsiri ya UZAWA ambayo Mzee Mengi anaizungumza, ama ni AINA nyingine ya UFISADI ambayo watanzania walio wengi bado hawajaung'amua kwa kuwa vyombo vya habari haviandiki wala kusema kuhusu habari hizi. Katika attachment ni orodha ya vitalu mbalimbali vinavyomilikiwa na Kampuni za Mzee Mengi hapa nchini.Tunaweza kutofautiana katika mengine lakini katika yale yanayohusu mustakabali wa nchi naomba watanzania tuungane na tuseme hapana. Matumizi ya Vyama vya Siasa, wanasiasa na hata pressure group katika kutetea maslahi ya baadhi ya tycoon wa hapa nchini ni hata nje ni katika makosa makubwa ambayo yanaweza kutuletea madhara makubwa sana hasa kutokana na rasilimali zilizopo hivi sasa hapa nchini. Nitoe ombi kwa Vijana hawa wa CHADEMA, watambue nafasi yao kama vijana na Safari waliyonayo ya kuijenga kesho yao na kusahau posho za siku moja na vyakula. Ni wakati wa kusimamia haki na kuitetea kweli, hata ikiwa kweli hiyo inakinzana na maslahi binafsi.
| Mengi Licence list.xls |
0 comments:
Post a Comment