Lakini wanaotakiwa kuhojiwa ni wananchi wala siyo huyu aliyetoa tamko hapo juu maana yeye hana tofauti yoyote na hao wanaotuhumiwa kutowashirikisha wananchi. Waandishi wa habari ebu tusaidieni kufanya kautafiti haka kadogo na mtujuze
2013/9/7 Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
--SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema hoja ya wabunge wa vyama vya upinzani kuwa haikushirikishwa kutoa maoni katika Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2013 ni ya uongo.
Kauli hiyo ilitolewa na Makamu wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Idd baada ya kutinga
bungeni jana wakati wa majadiliano muda mfupi kabla ya kuupitisha Muswada huo sheria.
Kauli ya Balozi Idd imemaliza mkanganyiko uliotanda nchi nzima baada ya kambi ya upinzani ikiongozwa na Kiongozi wa Kambi hiyo, Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe (CHADEMA) kususia kikao tangu
muswada huo ulipowasilishwa bungeni na kusababisha kutokea kwa vurugu kubwa jana.
Leo baada ya kipindi cha maswali na majibu kuisha, msululu wa wabunge wa upinzani na wa chama tawala walisimama wakitaka miongozo kutoka kwa Mwenyekiti aliyekuwa akiendesha kikao cha bunge, Jenester
Mhagama ambaye alichukua majina ya wabunge hao nakuwaomba wakae kwani miongozo yao atairuhusu baadaya mjadala wa muswada.
Baada ya kuambiwa hivyo, wabunge wa CCM walitii na kukaa huku wabunge wa upinzani wakitoka bungeni kutokana na msimamo wao waliouweka walipozungumza na waandishi wa habari juzi kwamba hawawezi kushiriki mjadala ambao umechukua maoni ya upande mmoja wa muungano, Tanzania Bara na kuacha Zanzibar.
Hata hivyo, baada ya majadiano kutoka kwa wabunge wa upande wa CCM akiwemo na mbunge wa Jimbo la Vunjo, Augustino Mrema (TLP) ambaye tangu mgogoro huo uanze, amekuwa akiendelea kuchangia ndani ya Bunge akisema yeye ametumwa na wananchi wake kuwawakilisha ndani ya bunge na sio nje waliupitisha muswada huo.
Kupitisha kwa muswada huo, kulimpa nafasi Mhagama kuruhusu wabunge walioomba miongozo yao huku akianza na mbunge wa Jimbo la Sikonge, Said Nkumba (CCM) aliyetaka mwongozo wa Mwenyekiti akisema kwa kuwa Wapinzani walisema Serikali ya Zanzibar haikushirikishwa na Balozi Idd yuko ndani ya Bunge kwani nini asipewa nafasi ili aondoe mkanganyiko uliopo.
Baada ya kumbana nafasi pia mbunge wa Jimbo la Simanjiro, Christopher Ole Sindeka (CCM) aliyetaka mwongozo kwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (CHADEMA) kumpiga Ofisa wa Polisi ngumi ndani ya Viwanja vya Bunge wakati wa virugu.
Hata hivyo, Mhagama alisema anatolea mwongozo mmoja wa Mbunge Nkumba, hivyo kumtaka Balozi Idd ambaye alisema yuko kwa nafasi yake ya ubunge ambayo inampa fursa ya kuwemo ndani ya bunge hilo, lakini pia kwa wadhifa wake wakuwa Makamau wa Pili wa Serikali ya Zanzibar, atoe maelezo juu hoja hiyo.
Balozi huyo alisimama na kusema ni kweli Zanzibar ilishirikishwa kikamilifu katika mchakato wa kutoa maoni kupitia kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Muungano na kwamba aliisaini barua hiyo mwenyewe.
Alisema kwa kuwa yeye ndiye msemaji wa Serikali baada ya Rais wa Zanzibar, Dk Mohamed Shein, wabunge
wasisikilize maneno yanayoletwa kwa njia za panya.
Mbali na Nkumba na Ole Sendeka wa CCM waliokuwa wameomba miongozo kabla ya kuendelea na mjadala, wengine alikuwa ni kutoka kwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe, Mbunge wa
Jimbo la Mkanyageni, Habibu Mohammed Mnyaa (CUF), Mbunge wa Jimbo la Ubungo. John Mnyika (CHADEMA) na wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA).
Majibu ya Balozi Idd yalikuwa ni kama itimisho la mjadala wa kushirikishwa kwa Zanzibar katika kutoa maoni ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013 ambao umepitishwa na wabunge wa CCM na TLP baada ya vyama vingine kuendelea kususa.
Hii inatoka na ukweli kwamba hoja kuu iliyobebwa na wabunge wa vyama vya upinzani vya CHADEMA, CUF na
NCCR-Mageuzi ambao katika hoja hii wana msimamo wa pamoja, ni kuwa Wanzabari hawakupewa nafasi kutoa maoni yao katika marekebisho muswada huo hadi unaletwa bungeni.
Jana, pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi kuomba mwongozo kwa Naibu Spika, Job Ndugai na kufafanua kwamba Serikali ya Zanzibar ilishirikishwa kikamilifu, kambi ya upinzani ilikataa majibu hayo ikisisitiza alichosema Lukuvi amelidanganya Bunge.
Viongozi wa Chadema, Mbowe na Lissu wakiwa na Kiongozi wa NCCR-Mageuzi na CUF baada ya vurugu ile iliitisha mkutano wa waandishi wa habari katika Ukumbi wa Msekwa pamoja na mambo mengine, walisema Serikali kupitia kwa Lukuvi imelidanganya bunge kwa kuwa haliyosema hayakuwa sahihi.
Msimamo huo ndio ulisababisha kutokea kwa vurugu hata ndani ya Bunge baada ya upande huo wa upinzani
kushikilia msiamomo wao huku wakitaka mjadala wa kuhusu muswada huo uhairishwe na huletwe katika bunge la 13 mwishoni mwa Oktoba mwaka huu, ili kutoa nafasi kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kushirikishwa.
Hoja ya kuahirishwa kwa Muswada huo ilitolewa na Mbunge wa Mkoani, Ali Khamis Seif (CUF) muda mfupi kabla ya kuanza kwa mjadala wa muswada huo.
Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/09/smz-yasema-ilishirikishwa-maoni-ya-muswada-wa-sheria-marekebisho-ya-katiba.html#ixzz2eAqr47Rp
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment