Tuesday, 10 September 2013

Re: [wanabidii] Serikali yakusudia kuanzisha Mtihani wa Taifa wa Darasa la Pili

Sijui kama kuna mantiki yoyote kitaifa kwa kuwa na mtihani wa kitaifa
wa darasa la pili. Kuanzishwa kwa mtihani huu, sioni kama ni njia
sahii ya kutatua tatizo la kutokujua kusoma na kuandika. Kwa sababu
hao waliojulikana hawajui kusoma na kuandika walivuka mtihani wa
darala la nne na pia mtihani wa darasa la saba. Kwa hiyo kuwa na
mtihani mwingine wa darasa la pili, sifikiri kuwa ndyo itakuwa
imemaliza hilo tatizo.

Kwa mtazamo wangu, ningalipendekeza kufanya yafuatayo:

Kuwa na waliamu ambaowatafuatilia maendeleo ya mwanafunzi kwa ukaribu
zaidi, ikiwezekana kubaini wanafunzi wenye uzito katika kupokea
mafundisho na kuwapa muda zaidi wa kusoma. Kama mtoto ataanza shule ya
awali, huwa kuna mitihani na majaribio, ili kumpima kama mwanafunzi
huyu ameiva katika kiwango kinachostahili kabla hajaruhusiwa kuendelea
na hatua nyingine ya juu. Hii inaweza kusaidia kubaini wanafunzi.

Waaalimu waangaliwe kwa kiasi kikubwa katika kutimiza majukumu yao,
maana kwa uzoefu wangu na taaluma yanguya ualimu, mtoto hujifunza
kusoma na kuandika akiwa katika madarasa ya chini, kuanzia madarasa ya
awali hadi darasa la pili. Kama waalimu watakuwa makini katika
kutimiza wajibu wao, kwa moyo w kujitoa, mtoto akitoka darasa la awali
na kuanza darasa la kwanza, ni lazima ahakikishwe kweli ana uwezo wa
kuingia darasa la kwanza, vinginevyo mtoto huyu aendelee kukaa katiaka
darasa la awali, vivyo hivyo hata katika madarasa mengine ya juu.

Kunaweza kuwekwa alama za ufaulu katika kila hatua moja kwenda
nyingine, na kama mwanafunzi hakufikia alama hizo basi, asiruhusiwe
kuendelea na darasa linalofuata. Yawezekana kwa njia hii tukatatua
tatizo la kuwa na watu wasiojua kusoma na kuandika katika madarasa ya
juu.

Haya ni mawazo yangu na mtazamo wangu kuhusiana na swala hili

Theonest E. Bahemuka
MSc(Chem), BSc(Ed)

On 9/10/13, Jovi kamuntu <jbifabusha@yahoo.com> wrote:
> Hiyo ndiyo serikali ya CCM. Haijui kama kuna Mtihani wa Darasa la 4 na
> kwamba wanafunzi wanavuka vipi kuendelea bila kusoma na kuandika. Je mtoto
> anawezaje kuanza Darasa la kwanza bila kujua kusoma, si kuna shule za awali
> kila shule, binafsi na taasisi pia? Au hizo ni biashara za watu?
>
> Nashindwa kuelewa.
>
> Jovin Bifabusha
>
>
>
> ________________________________
> From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
> To: wanabidii@googlegroups.com
> Sent: Tuesday, September 10, 2013 12:18 PM
> Subject: [wanabidii] Serikali yakusudia kuanzisha Mtihani wa Taifa wa Darasa
> la Pili
>
>
>
> Mtihani mpya wa Taifa utaanzishwa kwa wanafunzi wa darasa la pili nchi
> nzima, ili kuchuja watakaoshindwa kusoma, kuandika na kuhesabu.
>
> Akifafanua uamuzi wa kuanzishwa mtihani wa Taifa wa darasa la pili, Naibu
> Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alisema mtihani huo ni
> sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa matokeo makubwa sasa katika sekta ya
> elimu.
>
> Malengo ya mtihani huo kwa mujibu wa Mulugo ni kuondoa uwezekano wa kuwa na
> wanafunzi katika madarasa ya juu, wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu na
> ili kufikia malengo hayo, watakaoshindwa
> mtihani huo, watarudia mpaka wajue kusoma na kuandika.
>
> Aprili mwaka jana, Mulugo alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi
> ya Elimu Tanzania (TET), alikaririwa akikiri kuwa katika mtihani wa Taifa wa
> kumaliza elimu ya msingi wa mwaka juzi, kulikuwa na wanafunzi wasiojua
> kusoma, kuandika na kuhesabu, waliochaguliwa kujiunga na sekondari.
>
> Kutokana na udanganyifu katika mitihani ya Taifa, Mulugo alikaririwa
> akiagiza wanafunzi walioingia kidato cha kwanza wapimwe uwezo wao wa kusoma
> na kuandika na kuhesabu.
>
> Alikaririwa akisema kwa mujibu wa tathmini, mkoa wa Kilimanjaro uliongoza
> kwa kuwa na wanafunzi wengi wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu.
>
> "Mkoa wa Kilimanjaro una wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika wapatao 660,
> Tanga 490 na Dar es Salaam 208," alikaririwa Mulugo bila kutaja matokeo ya
> mikoa mengine.
>
> "Hili ndilo janga la kitaifa sasa. Si hayo mengine ambayo watu wanasema ni
> majanga ya kitaifa. Lazima tujiulize kwa nini watoto wanamaliza darasa la
> saba wakiwa hawajui kusoma na kuandika na wanafaulu?" Alihoji na
> kuongeza: "Je, siku hizi hakuna tena somo la kusoma na kuandika? Kwa nini
> mtoto amalize shule bila kuwa na maarifa ya KKK (Kusoma, Kuandika na
> Kuhesabu)? Jambo la kusikitisha kuna mpaka baadhi ya wanafunzi wa kidato
> cha tatu, ambao hawajui kusoma wala kuandika. Tulipofikia si pazuri hata
> kidogo, lazima tuwe makini jamani. Tuheshimu Baraza la Taifa la Mitihani
> (NECTA), tupate ufumbuzi wa mambo haya, Taifa hili ni letu sote, lazima
> tuhakikishe linasimama imara," alikaririwa Mulugo. --- viaHabariLeo
>
> Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/09/serikali-yakusudia-kuanzisha-mtihani-wa-taifa-wa-darasa-la-pili.html#ixzz2eToPKScv
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment