Sunday 23 June 2013

Re: [wanabidii] Tafadhali Usininukuu...

Nakumbuka wakuu wa mikoa wa enzi za Mwalimu mfano Tumainieri Kiweru aliwanyosha watu wa Rukwa, walijenga kwa nguvu uwanja mkubwa wa michezo (Mandela Stadium), pia kilimo kinachosifika huko Rukwa ni juhudi za huyu mkuu wa mkoa alikua akiwahimiza sana.

Sasa swali wakuu wa mikoa, na wilaya wa sasa wanahimiza maendeleo gani? Mzindakaya nae aliwabana Waha huko Kigoma mpaka wakaanza kulima chakula cha kutosha. Mwanzoni walimchukia sana na kumtisha lakini mwisho wa yote wanamshukuru. 

Watanzania tusipopunguza siasa zisizo na tija tutaendelea kubaki nyuma. 

From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Monday, June 24, 2013 2:06 AM
Subject: Re: [wanabidii] Tafadhali Usininukuu...

Ninaongezea mfano wa kusini Nd Kessy ila Lindi (si mbali na Mtwara yote ni Kusini yote yanafanana) kuwa:

Kilomita 65 hivi kutoka Lindi Mjini-ni Lindi Rural -Kuna Mhisani amewajengea wananchi kijiji cha Milola B shule ya vidudu. Utafiti wa DUCE ulionyesha watoto wa kijiji hicho wa umri wa kwenda shule hata wale baadhi wa age 10 hawasomi shule ya Msingi kutokana vitongoji vya Milola B vipo mbali na ilipo shule ya msingi. Wapo wanawinda ndege na kucheza vingoma wapigavyo wenyewe.

Shule ipo kilometa tano kwa vitongoji viwili hivi. Wakati wa majadiliano ikakubalika ikikamilika halmashauri italetwa walimu 2, wanakijiji watalipa mlinzi na mpishi wa watoto. Wazee 2 wametoa ekari 100 shule ijengwe baadae iwe primary school mwaka hadi mwaka wataongeza madarasa; wazazi waishio mbali wasogee wajenge karibu na shule maana eneo ni misitu. Ekari 10 za shule na shamba lake 90 wazazi wasogee wakawiwe wajenge. Mbegu za kulima ili waanze kuuza mazao ya mtama, kunde, mbaazi, ufuta waje wauze waweke hela bank zije kufaa mlinzi na mpishi, madesk, vikombe, mkeka (walipewa bure na mratibu mradi) pia hela za kufungua akaunti na kupiga picha za wahusika wa kutoa hela. wakianza kipindi nyumba haijaanza kujengwa hadi darasa liishe inaweza kuwa misimu 2 ya mvua na miwili ya vuri hivyo hela itaingia na michango itakuwa midogo. Hawakulima, eti mpaka waone shule imekamilika. Kulima ingewafanya wapungunze gharama ya kuchangia masuala mengi.

Shule ikakamilika hawajalima wala kuwa na hela ktk account zaidi ya walizopewa kuifungua. Swali la kushangaza wakati wa vikao kujadili kuhusu wajibu wa wazazi na uongozi kuhusu jengo ambalo wenyewe waliomba wawe na shule na ikaonekane kuanze chekechea. Swali: Hao watoto atawapeleka nani shule na nani atawarudisha? Hao ndio baadhi ya wazazi wa kusini. Huo ndio wajibu kwa watoto. Ujengewe shule, upelekewe na kurudishiwa mtoto. Anauliza swali kama hili anapigiwa makofi. Ujengewe shule halafu mtoto upelekewe na urudishiwe. Ilishangaza wengi hayo maswali na ni mengi ya ajabu ajabu. Inaumiza unapoona pia misitu, mabonde mazuri kijijini asubuhi saa moja vijana wenye nguvu wapo wanacheza hicho waitacho Pool Table. Kulalamika tu hodari lakini tuna mapungufu yetu pia. Fika machimboni huko wanakolalamika kutokufaidika na madini. Hata kule artisanal miners wachimbako wenyewe ni pombe, mabanda ya starehe za kujiambukiza maradhi, video za matusi. Hela weapatazo hawazitumii katika masuala ya maendeleo.
Kwanini  msinukuliwe kama mnasema ukweli. Tukijikanya ndio tutajirekebisha kwa maendeleo yetu pale tulipo sio kujidanganya kwa kutetea na kufifia ujinga. Unapolaumu angalia wewe umefanya nini kusaidia kurekebisha pale ulipo ambako kuna vingi chini ya uwezo wako.

From: Sylvanus Kessy <frkessy@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Sunday, 23 June 2013, 21:09
Subject: Re: [wanabidii] Tafadhali Usininukuu...

MJENGWA
UMESEMA UKWELI MTUPU! VIJANA WENGI hapa MTWARA HATA KAZI HAWAFANYI TENA. WANAJILUNDA VIJIWENI. UKIFIKA PALE AU UKIPITA WANAKUULIZA; "Inatoka au haitoki" ukisema haitoki unapewa TANO. ukisema itatoka utatukanwa na kufukuzwa maeneo hayo.

ELIMU INATAKIWA KWA KIWANGO KIKUBWA. WENGI WA VIJANA HAWA HAWANA ELIMU. BAADHI HATA KUSOMA NA KUANDIKA HAWAJUI AU NI SHIDA. JE WATANUFAIKAJE NA GAS? WANAWEZA KUPATA OFFER YA PUNGUZO LA UMEME NA SI VINGINEVYO. Kazi ipo! 

From: Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
To: mabadilikotanzania <mabadilikotanzania@googlegroups.com>; wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Sunday, June 23, 2013 10:08 AM
Subject: [wanabidii] Tafadhali Usininukuu...

Ndugu zangu,

Nahofia, kuwa Watanzania tumejikita kwenye ndoto ya utajiri wa gesi na mafuta. Hivyo, kusahau kilimo chetu. Hiyo ni hatari kwa uchumi wetu.

Tunafikiria utajiri wa gesi na mafuta kana kwamba katika dunia hii ni sisi tu Watanzania ndio wenye utajiri wa akiba ya gesi na mafuta. Hatujui, kuwa katika dunia hii kuna nchi zilizo na akiba hizo za mafuta na gesi lakini bado uchumi wao hauwafanyi watu wao wawe ni wenye neema tu.

Nao wanafikiria pia kwenye vyanzo vingine vya kuinua uchumi wao ikiwamo kilimo. Na ukweli tunaoishi nao sasa ni huu, kuwa gesi na mafuta bado havijawa uti wa mgongo wa taifa letu. Kilimo kimekuwa na huenda kitabaki kuwa UTI WA MGONGO WA TAIFA LETU. Na ndio UHAI WETU.
Maggid Mjengwa,
Iringa.
0754 678 252
http://mjengwablog.com
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment