Thursday 20 June 2013

Re: [wanabidii] Re: Vurugu za Jijiji Arusha-Zilikua lazima!!

Yona,
Ni muda mrefu sasa naona unaandika vitu vya kubuni. Uliandika juu ya WAJERUMANI kushawishi watu wa MTWARA kufanya vurugu wakati wewe hujui lolote kuhusu MTWARA. Leo nakushangaa tena unaposema wanaofanya fujo wamepata mafunzo waliopewa mafunzo au kuandaliwa vyovyote vile inavyosomeka. Hili ni jambo la ajbu sana, kwamba hatuna vyombo vya usalama hapa nchini au kama vipo basi vimelala au vimebariki kutendeka kwa fujo hizo. Kama kweli watu wanapewa mafunzo hapa hapa nchini ili walete vurugu basi vyombo vyetu vya usalama havina kazi.
Labda unaweza kutuambia wapi mafunzo hayo yanatolewa na ni nani anayatoa kwa lengo gani?
YONA, nimekuwa nakufuatilia sana tokea uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, ulijitahidi sana kukusanya matokeo ya awali hadi saa sita usiku huku mkipeana moyo na wanabidii wengine kwamba saa ya ukombozi ilikuwa inakaribia. Ghafla ukaacha ujumbe kuwa umechoka unaenda kulala, wanbidii wakajitahidi sana kukushawishi uendelee kuwapa matokeo hadi asubuhi lakini haikuwezekana. Tokea usiku ule ukawa kimya kabisa kwa muda.Na ulipoanza kupost tena unaandika mabo ya ajabu kabisa sijui ni kwa faida ya nani, nilichokigundua ni kwamba usiku ule malengo yako na wanabidii wenzako yalikuwa tofauti.Ndiyo sababu ulipoona yanakwenda ndivyo sivyo ukaamua kuwaambia unaenda kulala hata kama haikuwa kweli.
Mimi nachukia sana fujo na vurugu lakini nachukia sana uzushi na uongo. Nachukia uongo kwa vile imani yangu inakataza kusema uongo.
Tafdhali kama unajua wanapofundishwa vijana wa kufanya fujo vijulishe vyombo vya dola ili kuliepusha taifa na machafuko. Kuandika uzushi ni kuchochea fujo.

--- On Wed, 6/19/13, Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:

> From: Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>
> Subject: [wanabidii] Re: Vurugu za Jijiji Arusha-Zilikua lazima!!
> To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
> Date: Wednesday, June 19, 2013, 10:33 AM
> Ndugu victor
>
> Vurugu nyingi zinazotokea maeneo mbalimbali zinafanywa na
> watu
> waliopewa mafunzo kwa malengo hayo kwahiyo hicho unachoona
> wanachofanya polisi ni haki yao kujilinda wao wenyewe na
> wananchi na
> mali zao dhidi ya watu hao au makundi hayo ya watu .
>
> Nawasihi vijana wenzangu wajiepushe na kufuata mkumbo haswa
> nyakati
> hizi , wengi wenu hamjui chochote mnatumika tu .
>
> On Jun 19, 8:22 pm, Victor Mwita <victormw...@gmail.com>
> wrote:
> > Wadau jama nilikua jijini Arusha kikazi na wakati wa
> mchana kuelekea jioni
> > nililzimika kurudi mahali milipofikia kwa ajili ya
> kuchukua document
> > fulani. Kwa kuwa ilikua mjini nilijikuta katikati ya
> makundi yanayopingana,
> > Upande mmoja polisi wakiwa wanarusha mabomu ya machozi
> kila mahali na
> > makundi ya wananchi wakirusha mawe ovyo hususan
> wakiwalenga polisi.Ilifika
> > mahali dereva wa taxi alikosa njia ya kupita maana mawe
> yalipangwa njiani
> > kuzuia defenda za polisi.
> > Kwa kweli kwa mara ya kwanza nilihisi naweza kupoteza
> maisha. Namshukuru
> > Mungu dereva yule anafahamika so tuliweza kupenya hadi
> tukafika salama na
> > kurudi japo machozi yalinitoka pamoja na kufunga vioo
> vya gari.
> > Mimi najiuliza: Je zile vurugu zilikuwa na ulazima
> wowote? Ina maana
> > wahusika hawawezi kutafuta njia muafaka ya kila mmoja
> kufikia malengo yake
> > (yaani polisi kudumisha ulinzi na raia kuandamana kwa
> amani)
> > Is it really worthwhile kufanya yale waliyofanya? Huku
> ndiko tunakoipeleka
> > nchi yetu? Nahisi bado tunazo busara za kuweza kuishi
> kwa kuvumiliana na
> > kuishi kwa amani because we are very diverse but
> united.
> > Naomba wadau wote tupiganie amani despite our
> differences of opinion.
> > Natamani ningekua na uwezo wa kuwasiliana na uongozi wa
> mkoa wa Arusha na
> > wanasiasa niwashauri wajaribu amani kabla ya kupigana
> > Kwa kweli hali ilinitisha sana sana
> >
> > --
> > Victor Caleb Mwita
> > Ministry of Livestock and Fisheries Development
> > P.O. Box 9152
> > Dar Es Salaam
> > Tel: 0766750673, 0789142275
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
> Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
> for any legal consequences of his or her postings, and hence
> statements and facts must be presented responsibly. Your
> continued membership signifies that you agree to this
> disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the
> Google Groups "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails
> from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>
>

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment