Saturday, 22 June 2013

Re: [wanabidii] Mbowe kutoukabidhi ushaidi wa video ni kosa la jinai: Je kuukabidhi ni salama?

Muhingo,
Hivi polisi ndiyo hawahawa walio ua Mwembechai,Mwembetogwa nk? Hivi
ndiyo hawa waliokuwa wanapongezwa kwa kupiga watu Kariakoo kwamba ni
wafuasi wa Sheikh Ponda? Kama ndiyo hawa nadhani wanatimiza kazi yao
au Mkuki kwa Nguruwe!




Walewale.

On 6/21/13, ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com> wrote:
>
> Ilipotoka hapa jamvini kuwa mwenyekiti wa CHADEMA Taifa amesema anao ushaidi
> wa picha kuonyesha kuhusika kwa Polisi katika urushaji wa bomu katika
> mkutano wa chama chake huko Arusha mimi nilikuwa mmoja kati ya watu wa
> Mwanzo kumtaka atoe ushaidi huo mapema. Hadi sasa hajautoa. Nimesikia
> kupitia vyombo mbali mbali vya habari kuwa kutofanya hivyo ni kosa la
> jinai.
>
> Hata kabla ya sheria kusema hivyo kila mtu anaona kuwa kutoutoa ushaidi huo
> ni kuizuia sheria kumuandoa mhalifu katikati ya jamii na hivyo kuhatarisha
> usalama na amani. Mtu huyo anaweza kufanya jingine la hatari na lazima Mbowe
> atalaumiwa.
>
> Sasa nimesikia pia kupitia vyombo vya habari kuwa CHADEMA hawaiamini Polisi
> ndiyo maana hawataukabidhi ushaidi huo.
>
> Naomba kuuliza swali: Kama mtu ukiona huwaamini Polisi na kisheria
> unalazimika kuwakabidhi ushaidi; jema ni lipi kufanya. Kutoutoa ushaidi
> ukakabiliwa na kosa la jinai au kuutoa ushaidi huo ukachezewa? Jamii
> inasemaje na sheria zinasemaje.
>
> Si kusudi langu kumsaidia Mbowe kuhusu kutoaminika kwa jeshi letu la Polisi
> ila nasema tu matukio yanayojulikana kwetu wote ambayo jeshi letu la Polisi
> hata lenyewe haliwezi kujiamini:
> 1             Dr Mwakyembe akiwa bado mzima wa Afya aligundua njama za
> kumdhuru. Akakusanya ushaidi wa kutosha akalikabidhi jeshi la polisi (kwa
> maneno yake na kama alifvyonukuliwa na vyombo vya habari). Jamii haijui
> kilichofanywa na Polisi hadi Dr Mwakyembe anaumwa ugonjwa wa ajabu na hakuna
> anayejua kama hakuna uhusiano wowote kati ya Polisi kutofanya lolote na
> kuumwa kwake.
> 2            Dr Ulimboka alitekwa na kuteswa msituni. Alitoa maelezo ya
> kutosha. Gazeti la MwahaHalisi lilitoa ushaidi wa kutosha mpaka nikakumbuka
> habari moja kwenye Biblia ambapo mfalme alikwenda kupigana akamuomba Mungu
> wake kuwa ukiniongoza nikashinda kitakatojitokeza cha kwanza nikirudi
> nitakutolea sadaka. Aliporudi binti yake pekee alikuwa wa kwanza kumlaki na
> mfalme alimtoa kafara. Nilifikiri sasa Polisi watawachunguza waliotajwa
> kumdhuru Ulimboka bila kujali ni akina nani. Hadi sasa hakuna kilichofanyika
> na umma kuelezwa.
> 3            Mwaka 2005 Polisi waliua wafanya biashara. Wakatangaza kuwa
> wameua majambazi waliomwibia mfanya biashara Fulani. Polisi hao wakaonyesha
> maiti za wafanyabiashara kuwa ndio majambazi. Ilipogundulika kuwa hawakuwa
> majambazi na kuwa waliuawa kikatili bila sababu na kuwa hela nyingi
> walizokuwa wameuza madini hazionekani Polisi wakikosa ushahidi wa
> kudhibitisha kuwa hao ndio wauaji. Ushaidi uko kwenye television wakikiri
> kuwa wameua hao. Polisi wakakosa ushaidi.
> 4            Mwandishi David Mwangozi aliuawa. Kabla haijajulikana aliyemuua
> mtu mmoja mkubwa wa Polisi alisema Mwangozi ameuawa na wanachama wa CHADEMA.
> Tayari maandalizi ya kuwashughulikia yalianza. Mda huo CHADEMA wakatoa
> ushaidi kuonyesha muuaji wa Mwangosi. Mkubwa huyo aliyekuwa na ushaidi wa
> CHADEMA kuua alikuwa amesimama pembeni Mwangosi akiuawa. Polisi wamekosa
> ushaidi wa kufanya lolote na hakuna hatua hata za kinidhamu zinazochukuliwa
> dhidi ya wakubwa/Mkubwa huyo.
> 5            Hivi karibuni Polisi wamepewa habari Fulani kuwa Chama Cha
> Siasa kinaandaa vijana kwa kusingizia kuwapa mazoezi ya 'ukakamavu' Wakadai
> mazoezi wanayofanya ni zaidi ya ukakamavu. Na kwanza kwa nini uwapeleke
> kambini. Kimya tunachoshuhudia huenda wanafanya uchunguzi au yameishia
> hapo.
> 6            Hivi Karibuni Mr Lwakatare alikamatwa na kufunguliwa kesi ya
> Ugaidi. Kwa kuichunguza kesi hiyo ilibidi wote aliokuwa akiwasiliana nao
> wakamatwe ili iweze kuwa kesi ya ugaidi sawasawa. CHADEMA ilitoa orodha
> hiyo. Tumeishia kusikia kuwa kuchukua habari hizo kwenye mtandao ni kosa la
> jinai. Wala sio kuwakamata magaidi wengine. Sasa mahakama imemuondolea
> mashtaka hayo. Lwakatare amekaa lupango siku 90 plus. Ubatizo na kipaimara
> alichopata, tusubiri kidogo tutajua. CHADEMA wajiandae.
> Ukiyachunguza hayo niliyoyataja utakubaliana na Mbowe na CHADEMA kuwa
> ushaidi walio nao hautakuwa salama kuukabidhi Polisi. Je waukabidhi potelea
> kote mhalifu asishughulikiwe au wakatae mpaka utakapokabidhiwa kwenye mikono
> salama.
>
> Jamii inasemaje?
> Sheria inasemaje?
> Haki inasemaje?
> Katiba inasemaje?
>
> Elisa Muhingo
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>
>

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment