Tuesday 5 March 2013

[wanabidii] Re: Vijana Tanzania tuinuke na kuwa sehemu ya mabadiliko ya kweli

Ahsante kwa kuuliza swali kama Ukosefu wa ajira ni fursa au Tatizo .

Miaka michache iliyopita Ukosefu wa Ajira kwangu lilikuwa ni tatizo
kubwa nikafikiria kuanzisha kitu ambacho kitakuwa kinatoa fursa za
ajira kwa njia ya matangazo ya bure kwa watu mbalimbali kwanza ikawa
ni Tanzania , nikavuka afrika mashariki , Nikavuka Afrika sasa hivi
Niko Mabara yote - Kazi yangu ni kutafuta fursa za ajira sehemu
mbalimbali duniani kuziweka kwenye mitandao kwa ajili ya watu kusoma
na kuchangamkia nafasi hizo - mimi ninachopata ni asilimia fulani ya
hela kutokana na matangazo yanavyoonekana na yanavyotembelewa sehemu
mbalimbali duniani na kupitia hiyo moja ya Blogu hiyo ina niingizia
shilingi milioni moja ya Kitanzania kwa mwezi , inaweza kuongezeka ila
haipungui zaidi ya hapo .

Kwa nchi za wenzetu hayo matangazo yanayoonekana kwenye blogu na
tovuti kadhaa yanatengenezwa hiyo ni ajira kwa wengine , mtu
anayefanikisha matangazo ( sales marketing ) nae analipwa hiyo ni
ajira ya pili , mtu wa content ( maudhui ) nae analipwa ni percent
kidogo kidogo lakini kwa mwezi ni nyingi lakini hutegemeana na aina ya
matangazo na ukubwa wa matangazo hayo na muda ambao tangazo
linaonyeshwa .

Nimeeleza kwa ufupi kidogo kwa lugha nyepesi lakini kama kuna vijana
wanapenda kujifunza mambo mbalimbali ya tehama na jinsi wanavyoweza
kutumia taaluma zao za Tehama kujitengenezea ajira tunaweza kuendeleza
mjadala huu hata naweza kujitolea kuwafundisha bure vitu mbalimbali
ili tuweze kufikia malengo .



On Mar 5, 11:26 am, Fred <fredrick197...@yahoo.com> wrote:
> Kila mwana jamii anatakiwa kuwa sehemu ya mabadiliko.
> Ni ukweli ulio wazi kila mmoja hawezi kuwa mwanasiasa, mwendishi wa habari,
> IT personnel.... Ila kila mmoja ana kipaji na potentiality ambayo anayo na
> ikitumika vilivyo inakuwa productive.
> Fursa bado zipo, inaweza zisiwe za while color jobs katika gov offices au
> private sector... Kuna fursa nyingine kibao kwa watu waliofunguka macho.
> Vijana hatupaswi kuwa watu wa kulalamika siku zote, inataiwa tuwe sehemu ya
> suluhisho katika changamoto zilizopo.
>
> Kwa wasomaji wa biblia Daud alipata fursa ya kumuu Goliath baada ya Goliath
> kuwa tatizo. Vijana tuamke tuone matatizo yaliyopo kama fursa za
> kuyashughulikia na in-turn hiyo inatupatia ajira.
>
> A. R. Benard anasema kuna matatizo mengi duniani kuliko idadi ya watu na
> kila tatizo ni fursa... Je sisi kama vijana tunaangalia ukosefu wa ajira
> kama tatizo au fursa?
> Kushindwa ku-deliver kwa baadhi ya watu katika public office tunaona ni
> tatizo au fursa?
> Kila mtu akiona inawezekana na kuchukua hatua kufanya vitu vitokee mambo ya
> maana yatafanyika, hayatakuwa na tija kwetu kama vijana ila yatakuwa na
> matokeo na so as mguso kwa jamii nzima inayotuzunguka.
>
>
>
>
>
>
>
> On Monday, March 4, 2013 9:38:47 AM UTC+3, Hildegarda Kiwasila wrote:
>
> > Nani ajitume afanye au alete mabadiliko? wachache sana. Tuna Swahili
> > culture ya kualamika tu, kutokuona vibanzi vyetu bali vya wenzetu, kutafuta
> > kutatua matokeo (effects) sio chanzo au visababishi (causes). Kuchangia
> > maandamano ambayo yataharibu mali na usalama wa watu na kuchangisha hela
> > kufanikisha au kuchangia arusi za mahela kuliko kuchangia dawati, uniform
> > za mwanao asomae au kumkatia kadi ya afya ya elfu 2 kutibiwa kwa mwaka.
> > lakini kunywa pombe lita kadhaa kwa siku, kuvuta sigara na kununua magazeti
> > ya udaku-elfu tano+ utamaliza kwa siku. Pikipiki ya music na honi za
> > ajabuajabu za mapambo ya makelele (askari wanaona lakini kama hawaoni)
> > lakini sio kulima shamba ktk customary land uliyoachiwa na wazee. Unaiuza
> > ardhi hela unamalizia upuuzi na ufahari usio masuala ya maendeleo endelevu.
> > Unaona mifano kwa wenzako waathirika na pombe, bhangi, uzinifu-bado unavuta
> > bangi au kumwia unga na kuvamia ngono sio salama.
>
> > Inafurahisha hata mazoezi ya mbio za marathon- zilizokwisha weekend
> > Kilimanjaro wabongo wanalaumu serikali kutokuwaandaa vizuri!!??
>
> > Yaani wewe mkimbiaji wa marathon kuamka asubuhi mapema kutoka nyumbani
> > kwako pale ulipo, kufanya zoezi kukimbia mbio za urefu husika daily asubuhi
> > na jioni au mara moja kama desturi-Eti Serikali ije kukuamsha, ikuandae
> > vizuri vipi zaidi ya kuweka usalama njia ya kukimbilia?  Mazoezi kila
> > siku-Ujimbi daily. Hata mazoezi ya kukimbia ili football uicheze vizuri
> > NIL. Mbongo unasubiri wiki moja kabla vinguke kutoka Kenya hawajaja ndio
> > ufanye zoezi. Unapitwa ndani ya nchi yako na mlima ni wako mwenyewe!! Yaani
> > u mnene, mzito, huna zoezi, hujitumi-serikali haikuhudumii!??
>
> > Amka ujisomee ufaulu mtihani-Serikali mbaya!! Usiende samaki samaki kunya
> > beer bali maktaba hadi inapofungwa saa 4 usiku chuo au shuleni
> > kwako-Serikali na waalimu.  Fuga kitaalamu zingatia ushauri wa Kituo cha
> > Ufugaji wafikao kijijini kwako, Mifugo ya Mifano ya Sokoine, Kilimo cha
> > mfano-Naliendele, Ilonga, Tabora etc-hatujazoea hivyo. Mifugo ikipungua
> > nitaonekana masikini. Fuga nyuki kama alternative livelihood-tuletewe
> > mahindi ya chakula matunda siku hizi hakuna mitini. Hadi lini chakula cha
> > msaada kitafika na mvua zinanyesha kiasi na maua yanachanua na unaweza
> > ukawawekea maji nyuki kutundika kideli katika mti wakaweka asali bila
> > kuwalipa hela hao nyuki wa kuuma na wasiouma.
>
> > Gazeti la Habari leo 3/3/2013 front page inatoa picha ya watoto wa kimasai
> > kijiji cha Kambala Mvomero Morogoro wanasoma nje ya mti, baadhi yao wamevaa
> > mavazi ya kienyeji -khanga, mgolole bila viatu. Hivi ni pombe kiasi gani
> > baba anakuywa kwa siku na tumbaku ya kunusa ashindwe kununua per term
> > uniform, viatu, bag used/mtumba ya mtoto kubebea vifaa vyake. Kuuza mbuzi 2
> > kila mfugaji kuchangia standard 1, chumba na madeski, choo wilaya itoe
> > mabati, mbao, misumari kuezekea. Mwaka ujao-mbuzi 2 kwa std 2 mpaka kufika
> > std 7-NO, hatuwezi kuchangia kwa zababu tunalipa kodi-tunahamahama etc.
> > Enzi za misaada ya elimu bure kutoka communist countries haipo tena wala
> > kutoka EU, USA. Wao kwao wanamatatizo, Profesa anaendesha baiskeli kwenda
> > University kubana matumizi ya kodi ya parking gari, kukwepa msongamano.
> > Sisi, mlundikano wa mifugo kuonyesha utajiri sio kuchangia wala kuogopa
> > uharibifu wa mazingira kwa kizazi kijacho. Inanikera!!
>
> > Hatujitumi kuchangia ujenzi lakini vijana tunabomoa mito kutengeneza
> > tofari za kuchoma tunauza sio kuchoma tupeleke shule. Utakuta shule ya
> > vidudu Umasaini ni ya nyasi zinazovuja au wanasomea chini ya mti lakini
> > tajiri hapo ana ng'ombe 4,000, mbuzi 1000, punda 6, kondoo 200 na wa namna
> > hiyo ni 5% ya kaya zote mfano wanafika boma  5-10. Shule na elimu sio
> > priority; kujitumwa uzalishe kupitia kilimo na bustani (nyanya, machungwa,
> > nanasi etc) sio pia. mashamba ya mananasi Kiwangwa etc yameshauzwa. Ya
> > machungwa Muhoro Rufiji hakuna ni fence za wenye uwezo wamenunua waje
> > kuuzia wawekezaji wajao. Kwa sasa kila mtu ana pikipiki na bajaji za
> > kuwakata miguu vijana kwa accident.
>
> > Tuliunda kamati za wazee washauri za kijiji wazee na wale wa Kata ambapo
> > vijana wote hukusanyika ofisi yao ya Kata ya Mikumi toka vijiji mbali mbali
> > vya Kata. Nilimweleza Mh Kingwagala humu.
>
> > Vijana waliwachagua washauri wao wenyewe na kuingiza viongozi vijiji kama
> > waangalizi. Mafunzo ya kila aina pamoja na ujasiriamali Veta ikaja
> > kufundisha. Kupeleka wataalamu kutoka kila kona ya sekta muhimu(Kilimo,
> > Misitu, Nyuki, SACCOS) Afya-KCMC, daktari wa Health Centre, Kilosa Hospital
> > na zahanati zilizopo, NGO za vijana (YOPAC DSM), Legal NGOs etc na kuwa na
> > kamati ya ushauri ya wilaya. Ofisi ya vijana kila kijiji yenye makala kibao
> > na ya Kata ya vijana yenye kila kitu vya kiofisi, mahala pa kukutania,
> > choo, na maktaba kubwa fenced. Study tours within Ward and villages and
> > outside the district; mtaji wa kuanzia shughuli-Wapi, vyote vilikwenda na
> > maji vijiji vyote. Makundi mtafaruku, badilisha kiongozi huyu chagua
> > mwingine wao wenyewe malumbano na tamaa haziishi, kila mtu anategemea awe
> > kiongozi labda atatafuna afaidike.
>
> > Hili tatizo kuu TZ. Wazee wamechoka kuwashauri maana hawashauriki.
> > Wakibanwa sana-wanamchukia huyo mzee na kumuona mnoko kumtenga. Vijana wapo
> > ktk USHABIKI na kushabikia vitu vya mpito visivyo na tija na kujituma
> > kuzalisha mali-ya kupata kisent leo, kulewa na kuvuta sigara. Saidia wale
> > ambao wameonyesha utayari hata kama 2 wawe mfano kwa wengine ambao nao
> > wajiunge 2 au zaidi sio waingie kundi la hao wa mfano kuliharibu.
>
> > Vijana waige mfano wa vijana wa Kihehe-Ilula au wale wa Kiha kutoka
> > kigoma-Salasala DSM au wa kaya za Lushoto juu wanavyozalisha nyanya,
> > karoti, hoho etc kujaza fuso kuleta Dar-kila nyumba busy 24hrs Lusho. Au
> > Pare/Upareni year round biashaya ya ndizi za mbege, nyanya, vitunguu,
> > maembe, sugarcane mollases na mchele. Morogoro, Rufiji na Kibaha ilikuwa
> > zamani matunda sasa zimelala. Ardhi ni majumba, miji inakula mashamba,
> > viosk na miembe inaishia kukatwa kujenga majumba au kuchoma mkaa. Mbona
> > ulaya kuna Miji na mashamba-kulikoni bongoland kila mahara watu waambie huu
> > sasa mji kusiwe mashamba na mifugo mhame? hii ni balaa nyingine
> > itatumaliza. Vizee vitauza visichana ili wapate kula mashamba yao sasa ni
> > plots za majumba. Vijana ndio ujambani na kushabikia maandamano ya kufukuza
> > mawaziri. Ikiwa kila utakayezozana nae nyumbani kwako utamfukuza-utaishi na
> > nani. Angalia tatizo-tatua kiendelevu. Angalia-Jirani atakufurahia
> > unapofukuza watu ktk familia yako lakini kuja kukucheka baadae. Utakuwa
> > mjinga. Na ndio hayo ya vijana kushambikia maandamano wafukuzwe
> > viongozi/wajiuzulu. Huko umevunjika mguu nani atakutimia na kukulisha daima
> > utakapokuwa kilema?
>
> > Ikiwa sasa wazee huuza ardhi kiholela, kukaribisha wahamiaji haramu
> > kimagengo, viongozi wa vyama huwashauri vibaya kwa maandamano yaletayo
> > uharibifu kutokana kwamba kwenye mamba na kenge wapo!! Ni yupi
> > watakayemsikiliza nao wanapandishwa mori wa vyama vya siasa au au udini?
> > Ufisadi nao unaudhi na kila mtu ana tamaa za kupata aonekane.
>
> > Rudisha compulsory JKT kwa std 7 & iv (service men and women). Nimeombea
> > hili daima Mungu analisikia sasa. Form VI na university pia. Cheti cha JKT
> > kigezo kimojawapo cha kupata ajira au kukubaliwa course ya mafunzo. Huko
> > fikra za utaifa, kujijua na kupenda maendeleo ya taifa msemayo hapa
> > itarudi. Otherwise-nchi inaelekea ktk disaster Yona hakuna jinsi.
>
> > Mungu ibariki TZ.
>
> > --- On *Sun, 3/3/13, Yona F Maro <oldm...@gmail.com <javascript:>>* wrote:
>
> > From: Yona F Maro <oldm...@gmail.com <javascript:>>
> > Subject: [wanabidii] Re: Vijana Tanzania tuinuke na kuwa sehemu ya
> > mabadiliko ya kweli
> > To: "Wanabidii" <wana...@googlegroups.com <javascript:>>
> > Date: Sunday, 3 March, 2013, 7:23
>
> > Hatuwezi kuwa wote kwenye meza ya mabadiliko na kupigania mabadiliko
> > wengine waonyeshe mabadiliko kwa kutumia fursa zilizokuwepo kuanzia
> > bidhaa kwa ajili ya kuuza kwenye masoko na kutengeneza ajira zaidi kwa
> > vijana wengine , kwa wale wa TEHAMA wajiunge kwenye vikundi au waende
> > COSTECH kuna kitengo cha kuwezesha vijana wa TEHAMA katika
> > kijiendeleza na kuendesha biashara zao wafike pale waone wenzao
> > wanafanya nini .
>
> > Hatuwezi wote kuwa wanasiasa au kungangania kuwa kwenye vyama vya
> > siasa hapana tutumie taaluma zetu kujiendeleza na kuendeleza wengine .
>
> > On Mar 2, 11:53 pm, Fred Alphonce <fredrick197...@yahoo.com<http://mc/compose?to=fredrick197...@yahoo.com>>
> > wrote:
> > > Nataka kuona vijana wa Tanzania tunainuka na kuwa chachu ya mabadiliko
> > ya kweli katika jamii zetu.
> > > Tunahitaji mabadiliko ya kifikra katika
>
> ...
>
> read more »

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment