Tuesday 5 March 2013

[wanabidii] KUAHIRISHWA KWA MAANDAMANO KUPINGA DHARAU NA LUGHA YA KIFIDHULI INAYOTUMIWA NA SARAH HERMITAGE DHIDI YA TANZANIA

TAARIFA YA HUSETA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSUKUAHIRISHWA KWA MAANDAMANO YA AMANI YALIOKUWA YAMEPANGWA KUFANYIKA SIKU YA  JUMATANO TAREHE 6 MACHI 2013 KUPINGA DHARAU NA LUGHA YA KIFIDHULIINAYOTUMIWA NA SARAH HERMITAGE DHIDI YA TANZANIA 

Ndugu Wanahabari, 

Awali ya yote napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru  kwa ushirikiano mzurimliotuonyesha katika press conference tuliofanya siku ya jumapili tarehe 3 Machi2013 katika hoteli ya Traveltine. 

Kama nilivywaeleza Jumapili kwa takriban miaka mitatu sasa, raia mmoja waUingereza anayetambuliwa kwa jina la Sarah Hermitage amekuwa akiendeshakampeni ya kuchafua heshima ya taifa letu, watu wake, viongozi wake na taasisizinazotengeneza demokrasia yetu. 

Pia nilieleza kwamba taasisi yangu isiyo ya kiserekali na watanzania wengitumesikitishwa na kushoshwa na mwenendo wa Bi. Hermitage na tumeamua kutoahisia zetu za kupinga vitendo hivi. Kwa hiyo tumetayarisha maandamanotuliyotarajia yafanyike Jumatano tarehe 6th Machi kuanzia viwanja vya Mnazimmoja hadI nje ya ofisi za Ubalozi wa Uingereza ambapo tutawasilisha ujumbe wakuitaka Serikali ya Uingereza itamke hadharani kwamba haikubaliani na vitendovya raia wake. 

Mwisho mtakumbuka kwamba niliwajulisha kwamba nilikuwa nimeandika baruaya maombi ya kibali kwa Jeshi la Polisi. Sasa jana nilifanikiwa kuwa na kikao chapamoja na viongozi wa Jeshi la Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam. 

Kwanza nianze kwa kukiri kwamba tulipewa ushirikiano mzuri sana na Jeshi laPolisi ambalo limetushauri mambo mawili ya msingi: 
1.Kwamba kutakuwa na ugeni wa Waziri Mkuu wa nchi ya Denmark na ziarayake ya siku mbili kuanza kesho tarehe 6 Machi 2013 na itukuwa katikamaeneo ya jirani na tulipotarajia kufanya maandamano yetu. Hivyo kunahofu kwamba maandamano yetu yataleta mwiingiliano na ziara hiyo. 

2.Kwamba kwa sababu Ubalozi wa Uingereza ni nchi ndani ya nchi yetu, nivyema kuwasiliana na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ili wawezekuutarifu Ubalozi huo kujipanga kupokea ujumbe wetu.

Kwa heshima na taadhima sisi tumeafiki ushauri tuliopewa na Kamishna Msaidiziwa Polisi, Andrew Salum ambaye ni Kaimu Kamanda wa Polisi (Acting RPC) waKanda Maalum Dar es Salaam na tumeamua kuahirisha maandamo hadi siku yaJumatano tarehe 20 Machi 2013. 

Ni tegemeo letu kwamba Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Jeshi la Polisiwatakuwa wamekamilisha taratibu zote na ushiriki mpana katika muda huo.     

Tunaomba radhi  kwa usumbufu utakaojitokeza. 

Nawashukuru sana. 
Mungu Ibariki Tanzania na watu wake. 

Dagan T. Kimbwereza (Mwenyekiti) 
Human Settlements of Tanzania (HUSETA) 

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment