Tuesday 5 March 2013

Re: [wanabidii] Maalim Seif : Wazanzibar hawatokubali kukosekana Z’bar yenye mamlaka kamili

Tatizo lilokuwepo ni kuwa Maalim leo atasema hivyo lakini ukifika uchaguzi ataambiwa saini hapa ili watu wasije kuuliwa , na yeye anasaini watu wanaotaka mabadiliko watamtukana halafu tunasubiri uchaguzi mwingine bas. Hii ndio hali ya Zanzibar yaani ata katika ramani Zanzibar haipo kabisa bora Palestine manake inatajwa mara kwa mara na kua wenzetu wanaipigania nchi yao leo mtu kama hujamwambia kua ni Tanzania basi kwa Zanzibar utajihangaisha bure manake hamna mtu anaejua Zanzibar mie naona safari refu kama pana mafanikio basi si kwa miaka hii naona tutizamie vijukuu na vilembe, wala mtu asikasirike bora uchawi unatibika kuliko unafiq na ndio tatizo letu

2013/3/5 Lushengo Lutinwa <lutinwa@gmail.com>
Nadhani yupo sahihi, Kwanza nashukuru wapemba mmejitahidi kutujengea Kariakoo yetu ingawaje design za majengo mengi yanayomilikiwa na wapemba zimekaa kiz******r mno. Pili anatakiwa ajue kwamba kwa vyoyote vile dalili zinavyoonyesha kwamba, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar una mwisho, and that end is imminent.
Sasa hao jamaa zake atawapeleka wapi?
Nadhani wakati ana-plan kuuvunja  Muungano ili kila mmoja awe na saut,i inabidi pia awe na resettlement plan ya hao ndugu zake.

LL

2013/3/5 Fakhi Karume <fkarume@gmail.com>
Chama cha wananchi CUF kupitia katibu mkuu wa chama hicho ambae pia ni
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad,
kimemuhakikishia   Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
Tanzania , Jaji Joseph Warioba, kwamba Wazanzibari kwa umoja wao
hawatokubali chochote kile ambacho kitasababisha kukosekana kwa
Zanzibar yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa itakayofuatiwa na
mfumo mpya wa ushirikiano na Tanganyika kupitia Muungano.
Maalim Seif aliyasema hayo huko Makunduchi mkoa wa kusini Unguja
alipokuwa akizungumza na wananchi mbali mbali kwenye mkutano wa
hadhara wa chama hicho,amesema kutokana na matukio ya asilimia 66 ya
maoni ya wazanzibar kutaka mamlaka kamili ya nchi yao basi hakun haja
ya kutokuirjesha Zanzibar hadhi yake.

Kufuatia mkutano huo Maalim Seif amesema kuwa kwa sasa  Zanzibar
haiwezi tena kukubali kukosa mamlaka yake ya kuwa na udhibiti wa mambo
ya nje na mahusiano ya kimataifa kwani imechoka na udhalilishaji
inaofanyiwa na Tanganyika kupitia Serikali ya Muungano.

Aidha Maalim ametolea  mifano mbali mbali ambayo  Serikali ya Muungano
imeilazimisha Zanzibar kujitoa  katika Umoja wa Nchi za Kiislamu (OIC)
mwaka 1993 pamoja na hatua ya hujuma iliyofanywa na Waziri wa Mambo ya
Nje, Benard Membe, ya wiki iliopita ya kufuta maeneo ya ushirikiano
yaliyohusu Zanzibar yaliyokuwa yawe sehemu ya makubaliano katika
Mkataba wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Oman.

Sambamba na hayo  Maalim Seif alitaja athari ya Zanzibar kukosa nafasi
ya kufaidika na misaada ya kimataifa katika maeneo yote yasiyo ya
Muungano kwani Tanganyika hutumia jina la Tanzania kujichukulia nafasi
hiyo kwa manufaa na maslahi yake peke yake jambo ambalo limewatoa
imani wazanzibar waliowengi kuendelea na Muungano huu uliopo sasa.

Maalim amefahamisha wazi kuwa  kwa sasa Zanzibar inataka kuwa na
Wizara na Waziri wake wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na
haitokubali chochote chini ya hapo. Amesema kuwa "udhibiti wa mambo ya
nje ndiyo kigezo cha nchi kukubalika na kutambulika kimataifa na
Zanzibar inataka kurejesha mamlaka hayo na kurejesha kiti chake kwenye
Umoja wa Mataifa".

http://zanzibardaima.com/2013/03/04/wazanzibar-hawatokubali-kukosekana-zbar-yenye-mamlaka-kamili-maalim-seif/

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment