Thursday 25 October 2012

Re: [wanabidii] Waliogomea Shahada za UCLAS sasa kutunukiwa na UDSM - Mwanzo

Mambo ya warasimu wetu,
Tangu 2008 mpaka leo watu wanateseka kwa jmbo ambalo lingemalizwa mara moja bila kuendesha kesi muda wote huo.


Walewale.



From: Magiri paul <kiganyi@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, October 25, 2012 5:24 PM
Subject: [wanabidii] Waliogomea Shahada za UCLAS sasa kutunukiwa na UDSM - Mwanzo

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kitakuwa na mahafali ya 42 tarehe 27 Oktoba 2012 na Novemba 3, 3012.
Jumla ya wahitimu 3,643 watatunukiwa shahada na stashahada wakati wahitimu 902 wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ardhi (UCLAS) watatunukiwa shahada.
UCLAS kwa sasa ni sehemu ya UDSM.
Hayo yalisemwa na Makamu Mkuu wa wa UDSM, Profesa Rwekaza Mukandala akitoa taarifa kwa umma kupitia waandishi wa habari.
"Tunapenda kuufahamisha umma pia kuwa, katika mahafali ya sasa wanafunzi wa UCLAS na wao watatunukiwa shahada kama wanafunzi wa UDSM, uamuzi huu umefuatia kumalizika kwa kesi Lello & Others Vs Ardhi University, University of Dar es Salaam and Attornry General, Misc.Civil Cause No. 69 of 2008, iliyofunguliwa na wanafunzi wa UCLAS wakipinga kupata shahada za UCLAS kwa madai kuwa udahili wao ulibaki wa UDSM, hivyo UDSM kinakubalina kwa dhati na uamuzi wa Mahakama Kuu," alisema Prof Mukandala.

http://wotepamoja.com/archives/9683#.UIlLfiGWp0U.gmail --
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


0 comments:

Post a Comment