Thursday 25 October 2012

Re: [wanabidii] KITENDAWILI CHA NYERERE;

Chamani, amin hakupindua bali alifuatwa na wanajeshi walioasi wakampeleka ikulu wakamwambia tanguleo wewe ndo rais wetu, na alipoteua baraza la mawaziri mwanajeshi alikuwa mmoja tu, waziri wa ulinzi. Na vita vya kagera vilianzishwa na makoplo wa tanzania na uganda waliofyatulina riasasi, amin akaagiza wanajeshi wa uganda wawasogeze nyuma askari wa tanzania ili waweze kuregroup na kuongeza nguvu wasijelipiziwa kisasi, hili ndo kosa kubwa la amin kwani hakuwa amejiandaa kijeshi.
 
 

2012/10/25 Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
Shehe Chamani,
Haya bwana, niwie radhi kwa kukudhania kwamba unamtetea Idi Amin kwa sababu za kidini.
Matinyi.
 

Date: Thu, 25 Oct 2012 09:02:59 -0700

From: abachamani@yahoo.com
Subject: Re: [wanabidii] KITENDAWILI CHA NYERERE;
To: wanabidii@googlegroups.com

Matinyi,
Niombe radhi basi.




Walewale.


From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, October 25, 2012 6:59 PM
Subject: RE: [wanabidii] KITENDAWILI CHA NYERERE;

Chamani,
 
He! Unamruka Amin tena? Vipi, imekuwaje?
 
Nimekujibu kila kitu isipokuwa kuna mstari hujaosoma. Nimesema kuhusu ile makala nitaandika makala ya kuijibu na kukutumia. Mwenzako hapa nipo kazini, wewe huko labda usharejea nyumbani baada ya kazi - wataka nifukuzwe Yakhe? 
 
Amin si mgeni kwa Tanzania na Afrika Mashariki. Ukweli unabakia hivi, hata kama Obote asingekuja Tanzania bado Amin angevamia tu. Soma vitabu vilivyoandika kuhusu mtu huyu umwelewe haswa!
 
Matinyi.
 

Date: Thu, 25 Oct 2012 08:41:32 -0700
From: abachamani@yahoo.com
Subject: Re: [wanabidii] KITENDAWILI CHA NYERERE;
To: wanabidii@googlegroups.com

Matinyi.
Samahani kwa kosa hilo.
Mbona umejikita zaidi kwa Amini kuliko hata kwenye mada husika au ndiyo unaonesha utaalamu wako katika kuondoana kwenye mada.
Naomba nami uniombe radhi kwani hakuna pahala nimesema Amini alipigwa kwa sababu ya Imani yake hata kama naamini hivyo.
Nakuomba ujibu niliyokuuliza au hayajibiki.
Uko wapi ushahidi wa haya maneno yako au wewe ni "authority" tosha maana wenzio umewataka ushahidi huo.
Nimenukuu gazeti la Mwananchi kama lilivyofanya mahojiano na Mzee Mtei unasema je kuhusu huo msimamo wa mzee Mtei ambaye alikuwa mtu muhimu katika nchi yetu?
Nakunukuu;

"Alikuwa na matatizo na Tanzania kabla ya Tanzania kufanya lolote zaidi ya kumpokea Obote tu."
Wakati huo yeye Amini akiwa nani?
Una paradox nyingi sana Matinyi kwamba wewe kila ninachokiandika nakiangalia kwa udini lakini wewe huniangalie kwa udini?
Matinyi wacha ndalile zako jibu nilichokuuliza kuhusu makala hii hapo chini wacha kuzunguka zunguka na kupoteza maana.Silaha yako ni kunitisha na hilo neno Udini tu.
Jibu tafadhali wacha mineno mengi MURA.



Walewale. 


From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
To: Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Thursday, October 25, 2012 6:05 PM
Subject: RE: [wanabidii] KITENDAWILI CHA NYERERE;

Chamani,
 
Kwanza, ni kweli wewe si mwandishi wa makala hii; sijui kwa nini ulijihisi. Hii makala imetoka pia kwa Kiingereza kwenye gazeti jingine na imemtaja mwandishi wake kwa jina kamili. Itafute na huko pia.
 
Pili, mimi sina imani na dhana ya Mwenyeheri au Mtakatifu ila kwa hoja yangu mimi ni kwamba yeye Nyerere mwenyewe asingekubali kuitwa hivyo. Mwanaye aliwahi kuliambia Daily News na pia yeye Nyerere akiwa New Delhi mwaka 1996 alisema kwamba hata kupewa tuzo ya amani ya Gandhi haikuwa haki kwa kuwa alipendelea mapambano ya bunduki ili kuwakomboa watu wa Afrika na kwingine kama Palestina. Hilo ni suala lako wewe na Wakatoliki wachache.
 
Tatu, ni kweli nimeiponda ile makala na nina sababu moja tu: Kuna uongo na upotoshaji. Kuchambua kitu haina maana uweke na uongo ili kujiridhisha. Unaweza ukamchambua kiongozi na kumshambulia bila kuweka uongo. Natarajia kuijibu kwenye toleo la Kiingereza na la Kiswahili wiki ijayo katika magazeti mawili au matatu hivi. Nitakutumia nakala zake uone kwa nini ninaiponda.
 
Nne, kuna mchangiaji mmoja aliandika maneno haya na umeamua kunibandika mimi; sijui lengo ni nini au ulipitiwa tu? Mtafute aliyeandika yumo humu humu; huyo siye mimi na wala huhitaji kusumbua akili kujua kwamba siyo mimi. Yabebe ukamuulize mwenyewe, ni haya hapa:
2."Mchambuzi hakuonyesha source ya baadhi ya information ili wengine wajiridhishe na ukweli wa alichoandika. Vile vile hajazungumzia wimbi la upendeleo wa watu fulani kwenda kusoma India, Ukraine, Uturuki, Italia huku wakiwa watokea kwenye utamaduni wa aina moja na kuwaacha watu wa tamaduni zingine steanded. Hajaongelea kinachoendelea sasa kuhusu mambo ya upendeleo kwa watu wa utamaduni mmoja. Uchambuzi wake haujakamilika aandike na mapungufu ya wengine wote waliopo na waliopita wakirithi kiti hicho. Mwisho nasema naonya tu kuwa tukihukumu watu cheaply hivi bila kufanya fare and thorough analysis tutaishia pabaya."

Tano, kuhusu suala la Idi Amin, nadhani kinachokusumbua ni dini ya Idi Amin na si jingine. Bahati nzuri hujifichi. Ngoja nikupe dondoo kidogo kwa sababu nahisi hujawahi kutumia muda wako kulitafiti hili suala ila unabeba hisia tu kwamba Amin alikuwa mwislamu na kwa hiyo kupigwa na Nyerere ilikuwa dhambi na hujali kwamba aliwaua waganda 300,000 wakiwemo Waislamu. Museveni anasema hata Gadhafi alimtetea Amin eti kwa kuwa ni mwislamu.
 
Amin alimpindua Obote 1971 wakati Mkutano wa Jumuiya ya Madola ukiendelea Singapore. Nyerere alirudi Dar es Salaam. Obote alikwenda Nairobi na si kwamba walirejea wote kama ulivyosoma sijui wapi. Kenyatta akamtuma Moi kwenda uwanjani kumwambia Obote kwamba Kenya haitaki kumpokea kama mkimbizi. Kwa kuwa Obote alikuwa rafiki wa Nyerere (wakiwa na klabu yao na Kaunda iliyoitwa Mulungushi), alikuja Tanzania na kupokewa kama rais wa Uganda lakini baadaye aliishi kama mkimbizi kwenye nyumba iliyokuwa ile njia ya kwenda Makao Makuu ya JKT kupitia kwa Mwalimu Msasani. Obote aliwahi kuhojiwa na mwandishi wa vita wa Tanzania na alieleza maisha yake na hakuna hadhi ya urais wala kitu kama hicho. Hakuishi kama rais wa Uganda hapa Tanzania zaidi ya kupokewa tu. Wanajeshi wa Obote walikimbilia Sudan na wanasiasa wake wengi walikimbilia Kenya. Amin aliweka uadui na nchi zote hizi lakini kwa Tanzania aliongeza mambo mawili; aliiomba Israel na Uingereza zimsaidie silaha ili achukue bandari ya Tanga lakini wajaja hawa wakasema hana akili timamu; pili akasema kwamba mpaka halali wa Tanzania na Uganda ni Mto Kagera. Alikuwa na matatizo na Tanzania kabla ya Tanzania kufanya lolote zaidi ya kumpokea Obote tu. Usizisahau Kenya na Sudan.
 
Rais wa Sudan, Jaffery Nimeiri alikuwa rafiki mkubwa wa Nyerere kiasi kwamba Mwingireza mmoja alipomwandika vibaya kwenye Daily News alipewa masaa 24 kuondoka Tanzania. Uliza utapewa jina lake. (Nadhani hapo utaridhika kwamba Nyerere alikuwa na rafiki mwislamu). Nimeiri akasaini mkataba na Amin ili kumaliza uasi wa kusini ya Sudan ambao ulikuwa ukimtegemea Amin na yeye Amin akasema Nimeiri awafukuze wanajeshi wa Obote kutoka Sudan. Ndipo walipokuja Tanzania kwa meli kwa kupitia Tanga na baadaye kufungua kambi Tabora. Mwaka 1972 rafiki mwingine wa Nyerere (na yeye mwislamu ili uridhike), Mohamed Siad Barre, alizikutanisha Tanzania na Uganda na kusaini mkataba wa amani kwamba zisiweke majeshi yao mipakani umbali wa km 20. Tukasaini na Amin akauvunja mkataba mapema kabisa. Brigedia Himid (naye mwislamu ili ufurahi) aliwahi kueleza kwamba wakati Amin anavamia Tanzania ilikuwa na kombania tu tena mbali na mpaka.
 
Ndiyo, wapiganaji wa Uganda walifanya mazoezi Tanzania na kujaribu kurejea Uganda - cha ajabu ni nini? Mbona wapiganaji wa Zaire, Msumbiji, Angola, Namibia, Zimbabwe, na Afrika Kusini walikaa Tanzania? Mbona Tanzania ilivunja uhusiano na Israel kwa maslahi ya Wapalestina (waislamu ili ufurahi), lakini Israel haikuichokoza Tanzania? Makaburu, Wareno, Waingereza, n.k. mbona wao hawakuichokoza Tanzania licha ya kuwa nguvu zaidi? Viongozi wa Afrika waliokuwa wanamuunga mkono Nyerere kwa kumpinga Amin ni pamoja na marais wa Algeria na Misri (waislamu), na Ahmed Sekou Toure wa Guinea (mwislamu). Ninataja dini zao kwa sababu ndipo upeo wako ulipo hapo - huna dunia nyingine nje ya hii.
 
Amin haikuchokoza Tanzania peke yake. Aliichokoza Kenya mwaka 1976 baada ya ile opersheni ya dakika 90 Entebbe akiilaumu Kenya kwa kuwaruhusu Wayahudi kuitumia Nairobi katika operesheni ile. Bahati mbaya kwake, Wamarekani waliombwa kuisaidia Kenya na wakaja na meli lao kubwa hadi Mombasa na kumwambia Amin: "Tuko tayari, ivamie Kenya." Alikuja Tanzania kutokana na hali ya kisiasa ya enzi zile, kwamba Tanzania haikuwa na uhusiano mzuri na wazungu wa magharibi na pia Warusi walikuwa wakiiuzia Uganda silaha na kutoa mafunzo, kwa hiyo akaamini kwamba Tanzania haitapata msaada wowote hasa akizingatia kuwa China ilikuwa na matatizo na Vietnam mpaka wakapigana. Lakini kubwa zaidi alikuwa ni mwehu na hakuna ushahidi wowote kwamba sisi tulimchochea. Wanaodai hivyo wana yao lakini hawana ushahidi zaidi ya kulialia kwamba watu wa Obote walikuwa Tanzania.
 
Nimalizie kwa leo, wewe huzijui gharama zilizotumika kwenye vita ile zaidi ya kulalamika tu kwamba ilitupa umaskini. Madai haya hayana ushahidi wa kitaalamu. Aidha, misaada tuliyopata katika enzi zile inazidi gharama za vita ile ambazo zimefanyiwa utafiti na zipo. Pia, sehemu ya gharama zile imeshalipwa na Uganda katika awamu zilizofuatia baada ya Nyerere. Aidha, madeni mengine tulishasamehewa. Pia tulisaidiwa na marafiki zetu kwenye gharama za vita ile ikiwemo China, Algeria na Msumbiji iliyoleta bataliani nzima. Hata Uingereza baadaye ilitusaidia ilipoona mwehu anang'oka ingawa awali ilisita. Toa ushahidi wa madai kwamba ile vita ilitutia umaskini hadi leo. Hivi kila nchi maskini duniani ilipigana na Amin? Umaskini wetu ni matokeo ya mambo mengi ukiwemo ubwege wetu.
 
Sita, unaonekana kuwa na homa ya udini. Punguza hizo hisia kwa kuwa zimejengwa juu ya ubaya na uongo. Aidha, usifikiri kwamba ulivyo wewe ndivyo walivyo wengine. Kwangu mimi Waislamu na Wakristo na wengineo ni Watanzania wenzangu na ndugu, marafiki na washikaji zangu. Simo kwenye chama chako. Tujadiliane tu, basi! Hizo kofia zako vaa mwenyewe.
 
Naomba uniombe radhi kwa kunibandikai mambo ambayo sikuyaandika. Kuwa tu muungwana na utaheshimika.
 
Matinyi.

 

Date: Thu, 25 Oct 2012 00:13:24 -0700
From: abachamani@yahoo.com
Subject: Re: [wanabidii] KITENDAWILI CHA NYERERE;
To: wanabidii@googlegroups.com

Matinyi,
Nimejitahidi kidogo kukaa kimya juu ya jambo hili na sababu yangu ni kwamba mimi si mwandishi wa waraka huu na sikupenda watu wawahi kunishambulia mimi badala ya kujadili kilichoandikwa.
Ila nilicho kibaini ni kwamba kwako Mwenyeheri Ni zaidi ya rais wetu mstaafu.Kuna kitu hutaki kukisema maana hata busara ya kawaida inakutoka nitaonesha kidogo.Unasema

1."Nilikuwa mapumziko ya chai/kahawa nikawa nasoma huu upupu. Nitaujibu kwa vielelezo vyenye vyanzo rasmi. Huyu mtu ni mzushi mwenye ajenda ambayo hata mtoto wa darasa la kwanza hawezi kushindwa kuibani. Ni hili genge linalokua siku hizi ambalo siku si nyingi litatumbukiza kwenye matatizo makubwa."

-Ni upupu vipi? Ajenda gani isiyosemwa? Uzushi upi na kwani mwandishi unamjua?
-Unataka kujibu kwa vielelezo kwa jambo ambalo hata mtoto wa darasa la kwanza anaweza
 kubaini? Kwa hiyo unamwandikia wa darasa la ngapi ambaye unataka asidhuliwe na upupu huu?

-Genge hilo ni lipi na kuna uhusiano gani kati ya kilichoandikwa na kutumbukizana kwenye
 matatizo makubwa.Vitisho ni vyanini katika mazingira kama haya?

Kabla ulisema;

2."Mchambuzi hakuonyesha source ya baadhi ya information ili wengine wajiridhishe na ukweli wa alichoandika. Vile vile hajazungumzia wimbi la upendeleo wa watu fulani kwenda kusoma India, Ukraine, Uturuki, Italia huku wakiwa watokea kwenye utamaduni wa aina moja na kuwaacha watu wa tamaduni zingine steanded. Hajaongelea kinachoendelea sasa kuhusu mambo ya upendeleo kwa watu wa utamaduni mmoja. Uchambuzi wake haujakamilika aandike na mapungufu ya wengine wote waliopo na waliopita wakirithi kiti hicho. Mwisho nasema naonya tu kuwa tukihukumu watu cheaply hivi bila kufanya fare and thorough analysis tutaishia pabaya"

-Matinyi,unasema kuna upendeleo wa watu fulani kwenda kusoma nje kwa hiyo unakubaliana nami kwamba upo bila kujali niwakundi gani katika jamii?
-Unataka na mapungufu ya wengine yatajwe kwa hiyo unakubali kwamba kwa Mwenyeheri Nyerere hayo ni mapungufu?

Vile vili ulisema;

3."Kama huyu mwandishi amesema kwamba suala la Amin lingewezwa kumalizwa kwa mazungumzo, na nimeona kuna vijineno vya aina fulani hivi amevichomeka, nadhani ni kupoteza muda kuisoma, labda kama lengo litakuwa kuokoa upotoshaji. Na kwa lugha yake ya sentensi chache niliziona, huyu muungwana anajulikana na yumo humu humu jamvini. Ni matatizo yale yale tu. Nyerere alikuwa binadamu na kiongozi makini aliyeipenda nchi yake; na katika utendaji wake kuna mambo alikosea lakini hatupaswi kuchambua uongozi wake kwa uongo, udini, n.k."

-Matinyi unajua kwanini tulienda vitani na kwa bahati nzuri Mzee Mtei alishalizungumza hili.Kwa hicho kidogo naomba nilinukuu gazeti la Mwananchi 9 Desemba 2011;

Anasema mwaka 1971 Hayati Mwalimu Nyerere alisafiri na Rais wa Uganda wakati huo, Milton Obote kwenda kwenye mkutano wa nchi za Jumuiya ya madola ambao ulifanyika nchini Singapore.
Anasema Hayati Mwalimu Nyerere na Obote walikuwa marafiki sana na wakati wakirejea nchini ndipo walikuta Idd Aman amefanya mapinduzi na kujitangaza Rais wa Uganda.
Anasema wakiwa njiani kutoka katika mkutano huo, walipofika Nairobi nchini Kenya, Obote aliandamana na hayati Baba wa Taifa mwalimu Nyerere hadi jijini Dar es salaam.
Mtei anasema Obote alipewa makazi Dar es Salaam katika eneo la Msasani na serikali ya Tanzania ilikuwa inamgharamia kwa kila kitu kama rais wa nchi.
Anasema kutokana na mauaji na hali ya usalama kuwa mbaya nchini Uganda, Waganda wengi walikimbilia nchini Tanzania na kuanza kujipanga kurejea nchini kwao kuikomboa nchi yao.

-Ulitegemea Dikteta Nduli Idd Amin Dada afanye nini wakati kuna azma tayari ya kumwwondoa madarakani?
Ndicho hicho unachokiona Mashariki ya Kongo ya Kabila na uhusiano wa Rwanda na Uganda ulivyokuwa wakati RPF walipoanza harakati zao Uganda mwanzoni mwa miaka ya 1990.Ifatilie vizuri historia ya Yoweri Kaguta Museveni na hata ujue hiyo zawadi ya shule tuliyojengewa huko Kamachumu Muleba.
-Matinyi unakubali kwamba kuna baadhi ya maeneo Mwenyeheri Nyerere alikosea ni maeneo yapi?
-OAU walishindwa kulaani kwa kuwa sababu na maelezo yaliyokuwa yanatolewa na upande wetu yalikuwa hayawaridhishi.

Matinyi nadhani umeandika sana ndugu yangu na huwa najitahidi kukusoma ila naomba uandike historia hiyo kama ulivyohaidi na nakushauri usome tena huo waraka ukiwa na roho isiyo na chuki utaelewa maana kitu kinachozungumzwa ni chakawaida mno kwa ambao tulikuwa hadhiri katika uongozi wa mtukuka huyo.




Walewale.

From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
To: Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Tuesday, October 23, 2012 9:25 PM
Subject: RE: [wanabidii] KITENDAWILI CHA NYERERE;

Chengula,
Mimi nakiona huruma kizazi cha vijana wadogo wa leo wakiwemo watoto wangu; kwamba watalishwa uongo mwingi sana na watu wenye mioyo mibaya dhidi ya taifa letu. Dawa yake ni kuyajibu mambo haya na ikibidi kuandika vitabu ili kuiweka rekodi sawa kama wafanyavyo wenzetu. Huwezi kukuta Wamarekani wanapotosha historia na kazi za viongozi wao waliolijenga taifa lao; huwezi hata siku moja. Sikubaliani na mambo fulani ya Nyerere na niliwahi kuyaandikia lakini kumsingizia uongo na kupinda historia yake ni uhuni mkubwa.
matinyi.
 
> Date: Tue, 23 Oct 2012 17:11:37 +0000
> From: achengula@gmail.com
> Subject: RE: [wanabidii] KITENDAWILI CHA NYERERE;
> To: wanabidii@googlegroups.com; wanabidii@googlegroups.com
>
>
> Well said kaka Matinyi,
>
> ni kweli nimeupitia kwa makini nimekundua ni wale wake wa vuguvugu hili. Mwandishi mwenyewe anajichanganya huwezi kupata hitimisho la makala yake. Mambo aliyoyaandika yanatokana pengine na kile anachokifikiria ili kutimiza lengo lake. Maandishi yake yalivyo kaa hayaonyeshi kayapata wapi. Labda alete vyanzo vyake hapo nitaamini. Yanaonekana kuwa ni utafiti wa kubuniwa.
>
> Vita yake ni Muungano na Ukristo, hapa ndipo utajua ni wale wale. Angalia alivyoelezea muungano hali kadhalika Ukatoliki, huna haja ya kujua aliye andika ana itikadi gani ya kidini. Aliye uleta ni wale wale sawa na mwandishi wenye malengo yale yele.
> -----Original message-----
> From: Godfrey Ngupula
> Sent: 23/10/2012, 18:12
> To: wanabidii@googlegroups.com
> Subject: RE: [wanabidii] KITENDAWILI CHA NYERERE;
>
>
>
> thanks Matinyi..i love people with sterio thinking like u do.People with digital mind (and not analogue).Simple to grasp and analyse beyond the reach of human eyes.Ngupula
>
>
>
> ------------------------------
> On Tue, Oct 23, 2012 5:52 PM EEST Mobhare Matinyi wrote:
>
> >
> >Kabalika,
> >Nilikuwa mapumziko ya chai/kahawa nikawa nasoma huu upupu. Nitaujibu kwa vielelezo vyenye vyanzo rasmi. Huyu mtu ni mzushi mwenye ajenda ambayo hata mtoto wa darasa la kwanza hawezi kushindwa kuibani. Ni hili genge linalokua siku hizi ambalo siku si nyingi litatumbukiza kwenye matatizo makubwa.
> >Matinyi.
> >
> >
> >
> >
> >Date: Tue, 23 Oct 2012 15:47:50 +0100
> >From: rotts76@yahoo.co.uk
> >Subject: Re: [wanabidii] KITENDAWILI CHA NYERERE;
> >To: wanabidii@googlegroups.com
> >
> >
> >
> >
> >
> >
> >Mchambuzi hakuonyesha source ya baadhi ya information ili wengine wajiridhishe na ukweli wa alichoandika. Vile vile hajazungumzia wimbi la upendeleo wa watu fulani kwenda kusoma India, Ukraine, Uturuki, Italia huku wakiwa watokea kwenye utamaduni wa aina moja na kuwaacha watu wa tamaduni zingine steanded. Hajaongelea kinachoendelea sasa kuhusu mambo ya upendeleo kwa watu wa utamaduni mmoja. Uchambuzi wake haujakamilika aandike na mapungufu ya wengine wote waliopo na waliopita wakirithi kiti hicho. Mwisho nasema naonya tu kuwa tukihukumu watu cheaply hivi bila kufanya fare and thorough analysis tutaishia pabaya.
> >
> >
> >
> >
> >
> >From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>;
> >To: Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>;
> >Subject: RE: [wanabidii] KITENDAWILI CHA NYERERE;
> >Sent: Tue, Oct 23, 2012 12:01:25 PM
> >
> >
> >
> >
> >
> >
> >Kama huyu mwandishi amesema kwamba suala la Amin lingewezwa kumalizwa kwa mazungumzo, na nimeona kuna vijineno vya aina fulani hivi amevichomeka, nadhani ni kupoteza muda kuisoma, labda kama lengo litakuwa kuokoa upotoshaji. Na kwa lugha yake ya sentensi chache niliziona, huyu muungwana anajulikana na yumo humu humu jamvini. Ni matatizo yale yale tu. Nyerere alikuwa binadamu na kiongozi makini aliyeipenda nchi yake; na katika utendaji wake kuna mambo alikosea lakini hatupaswi kuchambua uongozi wake kwa uongo, udini, n.k.
> >Matinyi.
> >
> >
> >
> >
> >
> >Date: Tue, 23 Oct 2012 12:51:16 +0100
> >From: ngupula@yahoo.co.uk
> >Subject: Re: [wanabidii] KITENDAWILI CHA NYERERE;
> >To: wanabidii@googlegroups.com
> >
> >
> >Binafsi ingawa namfagilia sana Mwalimu kama mwanasiasa safi,lakini huwa nakubali kuwa alikuwa na mapugufu mengi pia kama binadamu.Ni hotuba nzuri ingawa msimuliaji hakuwa na balance katika kuelezea haswa balance ya mambo fulanifulani. Mfano,anaposema vita ya Uganda ingeweza kuisha kwa mazungumzo...sio kweli. Kwa tuliokuwepo kwa wakati huo Nyerere alitoa nafasi kubwa kwa OAU na UN yamkini hata ya kumlaani AMIN na hakuna taifa lililofanya hivyo. Sasa,unawezaje kusubiri mazungumzona mtu kicha kama Amin asiye na utu na huku anaua watu wako.Diplomasia ni nzuri but ina wakati wake.Ukiiikosea unaonekana tu ni mtu usiye na maamuzi.Kwa hilo hakukosea,sio kweli.
> >
> >Na kuhusu utaifishaji,anaweza akalaumika kwa upande fulani,lakini kwa upande mwingine halaumiki. Kwa mfano,alivyotaifisha mashule ili kufanya watu wote wasome kwa usawa...
> >
> >Hayo ni baadhi tu...
> >
> >Godfrey
> >
> >
> >
> >
> >
> >
> >
> >
> >
> >
> >
> >
> >
> >
> >From: Ben Nyitambe <matikubn@gmail.com>
> >To: wanabidii@googlegroups.com
> >Sent: Tuesday, 23 October 2012, 9:05
> >Subject: Re: [wanabidii] KITENDAWILI CHA NYERERE;
> >
> >Asante sana kaka!
> >
> >On 10/23/12, mngonge <mngonge@gmail.com> wrote:
> >> Mwandishi wa makala kaibua maswali muhimu ambayo majibu yake ni juu
> >> yetu kutafakari. Siamini kama kuna mtu anayefikiri kwamba Nyerere
> >> hakufanya kosa ata moja. Yeye mwenyewe (Nyerere) alikiri kwa kinywa
> >> chake kwamba yapo makosa mengi yaliyofanywa na serikali yake lakini
> >> pia yapo mazuri aliyoyafanya. Wakati akipigania haki za watanzania,
> >> yapo mambo ambayo siamini kama yalikuwa na baraka za umma bali matakwa
> >> yake mwenyewe hasa hasa mambo yaliyohusu mahusiano yetu na nchi za
> >> nje.
> >>
> >> Sera zake za ndani zilididimiza maendeleo ya maeneo fulani huku
> >> akiyainua mengine bila shaka kwa nia nzuri, bila kuwa dikteita kwa
> >> wakati huo tusingekuwa na Tanzania tunayoiona leo. Sitegemei kama
> >> wamissionari na mabepari wenye mashamba makubwa walifurahishwa na
> >> kitendo cha Nyerere kutaifisha mali zao. Kulikuwa na machifu ambao
> >> uhusiano wao na watu wengine ni wa bwana na mtumwa hawa kwa vyovyote
> >> vile lazima wamlaani Nyerere kwa vile walikuwa ni wanyonyaji na
> >> wangependa kuendelea kufanya hivyo. Yapo mambo mengi tu ambayo
> >> tunaweza kuyaangalia kwa mitizamo tofauti kutegemea na nafasi
> >> tulizokuwa nazo au tulizo nazo kwa sasa.
> >>
> >> Kwa mtizamo wangu namuona Nyerere kama mtu aliyekuwa na mapungufu ya
> >> kawaida kama binadamu lakini kwa ujumla namuona kama kiongozi safi wa
> >> wakati huo katika mazingira ya wakati ule.
> >> 2012/10/23 <hkigwangalla@gmail.com>:
> >> Duh! Makala nzuri, imeandikwa kwa umahiri japokuwa wengi wetu
> >> hatutoikubali
> >> kwa sababu tunampenda Baba wa Taifa na tunaamini ni mtu aliyekuwa na nia
> >> nzuri na Taifa hili na nia hiyo haikujificha hata siku moja! Kuanguka kwa
> >> itikadi zake ama kutotekelezeka kwa mikakati yake haimaanishi he was a
> >> bad
> >> leader, wengine tunaona better him he tried...
> >> Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania
> >> ________________________________
> >> From: amour chamani <abachamani@yahoo.com>
> >> Sender: wanabidii@googlegroups.com
> >> Date: Mon, 22 Oct 2012 20:40:41 -0700 (PDT)
> >> To: wanabidii@googlegroups.com<wanabidii@googlegroups.com>
> >> ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
> >> Subject: [wanabidii] KITENDAWILI CHA NYERERE;
> >>
> >>
> >> Mwandishi Wetu|RAIA MWEMA,Toleo la 263 |17 Oct 2012
> >>
> >> WATAFITI wengi wamejaribu kuelezea kwa kina Julius Nyerere alikuwa
> >> binadamu
> >> wa aina gani, lakini baadhi yao wanaamini alikuwa ni mtu ambaye ni vigumu
> >> kumuelezea kinagaubaga taswira yake na mwenendo wake mzima kwa ujumla.
> >> Katika makala hii tutajaribu kumchambua angalau tupate ufunuo kuhusu
> >> hilo.
> >> Katika zama zake kileleni Mwalimu, kama wafuasi wake walivyopenda
> >> kumwita,
> >> msomi huyu mahiri wa Afrika, alinyenyekewa mno kwa heshima na Watanzania
> >> wengi huku wengi pia wakimnanga kwa staili ya utawala wake ambao ulikuwa
> >> wa
> >> kibabe na wenye harufu za kidikteta. Wengine walimpa jina 'dikteta
> >> mrahimu'.
> >>
> >> Ukweli ni kuwa Watanzania mara kwa mara wamekuwa wakishindwa kutafsiri
> >> yale
> >> ambayo Mwalimu aliyasimamia, misimamo yake ya sera zenye misingi ya utu
> >> wa
> >> binadamu na azma zake za kifilosofia. Kuyajadili mafanikio yake na
> >> vilevile
> >> makosa yake. Tumeshindwa kumsoma bila ya ushabiki, sijui ni kwa sababu za
> >> uvivu au ni woga. Kwa hakika, kwa yeyote atakaye kupanda ngazi ama ya
> >> kijamii au ya kisiasa, basi busara ya kawaida tu itamlazimu akwepe kutaja
> >> makosa ya Nyerere hata kama yanafahamika kwa wote. Hii imekuwa kama hulka
> >> ya
> >> Kitanzania.
> >>
> >> Nyerere hayuko nasi leo na hii ni sababu nzuri ya kutaka kukumbuka kuwa
> >> hapo
> >> zamani alipata kuwapo mwanasiasa aliyeongoza harakati za kutafuta uhuru
> >> wa
> >> nchi hii; akabahatika kuaminiwa na watu wake; akajaribu kufanya yale
> >> aliyoamini kuwa ni ya manufaa kwa nchi yake; akalazimisha majaribio tata
> >> ya
> >> fikra na sera zake kwa wananchi wake aliowapumbaza, kwa muda wa miongo
> >> miwili na nusu na tofauti na watawala wengine wa Kiafrika, hakustaafu kwa
> >> kupinduliwa. Lakini mwishowe, kwa msaada wa masharti magumu ya kiuchumi
> >> ya
> >> Benki ya Dunia (Bretton Wood Institutions) aliachia ngazi, mwaka 1985.
> >>
> >> Hivi Nyerere alikuwa ni nani? Je, alikuwa ni mwana wa chifu mmoja
> >> asiyejulikana kutoka madongokuinama aliyeamua kuishi maisha ya mtu wa
> >> kawaida? Je, alikuwa mkristo mzuri aliyevaa baraghashia ya kiislamu kama
> >> vazi lake la kawaida tu? Au, ni mwalimu msomi aliyeacha kufundisha ili
> >> ajiunge na siasa? Au, 'Mkomunisti' aendaye kanisani kila leo na kupata
> >> sakramenti? Ama kiongozi aliyejizatiti kuwafikiria wananchi wake na
> >> ukombozi
> >> wa Afrika tu? Yawezekana alikuwa muunganishaji aliyetuachia Muungano
> >> wenye
> >> nyufa tele? Au alikuwa mmajumui wa Afrika aliyekataa katakata kuanzishwa
> >> kwa
> >> Serikali moja ya Bara la Afrika. Haswa, huyu Nyerere alikuwa mtu wa aina
> >> gani?
> >>
> >> Mwalimu alikuwa mtu mwenye familia njema na alijaaliwa watoto kadhaa.
> >> Ukweli
> >> sote tunaujua kuwa, familia yake iliishi maisha ya kawaida bila ya
> >> kuonyesha
> >> kiburi, fahari
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 



--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 



--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 



--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment