Kwa wale wanafuatilia maandiko matakatifu,yanasema,ukimtwanga mpumbavu kwenye kinu pamoja na ngano,ngano itaiva na maandazi utakula lakini mpumbavu atabaki na upumbavu wake.pia,yanasema mpe hekima mwenye hekima atakupenda,lakin mpumbavu atakudharau. Hoja ya mpumbavu ni vijembe na wingi wa maneno yake...
Mimi nafahamu,kuna watu wengine,hata wa humu kwenye mtandao ni diplomasia tu ya kimazingira ndo inawalazimisha hata kuaccept kuwa Nyerere tried alot and did something to this country.Lakini,kiukweli kabisa wangelipenda wamlaumu kwa kila kitu na asipewe heshima yeyote..Ngupula
------------------------------
On Thu, Oct 25, 2012 6:01 PM EEST Emmanuel Muganda wrote:
>Hapana,
>Nimechagua la Amin kama kianzio tu. Pia kuongezea: ni uwongo kuwa JKN
>alipiga marufuku maandamano.
>Unakumbuka maandamano ya wanafunzi kupinga national service? Waliruhusiwa
>kuandamana.
>Unakumbuka maandamano ya wanafunzi kupinga UDI Rhodesia?
>em
>
>2012/10/25 amour chamani <abachamani@yahoo.com>
>
>> Emmanuel,
>> Mengine yote huna tabu nayo ila la Amini siyo?
>>
>>
>>
>> Walewale.
>>
>> ------------------------------
>> *From:* Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com>
>> *To:* wanabidii@googlegroups.com
>> *Sent:* Thursday, October 25, 2012 12:55 PM
>>
>> *Subject:* Re: [wanabidii] KITENDAWILI CHA NYERERE;
>>
>> Amour,
>> Hivi unaelewa ni nani aliyemhimiza Amin ampindue Obote? Na ni kwa nini?
>> em
>>
>> 2012/10/25 amour chamani <abachamani@yahoo.com>
>>
>> Matinyi,
>> Nimejitahidi kidogo kukaa kimya juu ya jambo hili na sababu yangu ni
>> kwamba mimi si mwandishi wa waraka huu na sikupenda watu wawahi
>> kunishambulia mimi badala ya kujadili kilichoandikwa.
>> Ila nilicho kibaini ni kwamba kwako Mwenyeheri Ni zaidi ya rais wetu
>> mstaafu.Kuna kitu hutaki kukisema maana hata busara ya kawaida inakutoka
>> nitaonesha kidogo.Unasema
>>
>> 1."Nilikuwa mapumziko ya chai/kahawa nikawa nasoma huu upupu. Nitaujibu
>> kwa vielelezo vyenye vyanzo rasmi. Huyu mtu ni mzushi mwenye ajenda
>> ambayo hata mtoto wa darasa la kwanza hawezi kushindwa kuibani. Ni hili
>> genge linalokua siku hizi ambalo siku si nyingi litatumbukiza kwenye
>> matatizo makubwa."
>>
>> -Ni upupu vipi? Ajenda gani isiyosemwa? Uzushi upi na kwani mwandishi
>> unamjua?
>> -Unataka kujibu kwa vielelezo kwa jambo ambalo hata mtoto wa darasa la
>> kwanza anaweza
>> kubaini? Kwa hiyo unamwandikia wa darasa la ngapi ambaye unataka
>> asidhuliwe na upupu huu?
>>
>> -Genge hilo ni lipi na kuna uhusiano gani kati ya kilichoandikwa na
>> kutumbukizana kwenye
>> matatizo makubwa.Vitisho ni vyanini katika mazingira kama haya?
>>
>> Kabla ulisema;
>>
>> 2."Mchambuzi hakuonyesha source ya baadhi ya information ili wengine
>> wajiridhishe na ukweli wa alichoandika. Vile vile hajazungumzia wimbi la
>> upendeleo wa watu fulani kwenda kusoma India, Ukraine, Uturuki, Italia huku
>> wakiwa watokea kwenye utamaduni wa aina moja na kuwaacha watu wa tamaduni
>> zingine steanded. Hajaongelea kinachoendelea sasa kuhusu mambo ya upendeleo
>> kwa watu wa utamaduni mmoja. Uchambuzi wake haujakamilika aandike na
>> mapungufu ya wengine wote waliopo na waliopita wakirithi kiti hicho. Mwisho
>> nasema naonya tu kuwa tukihukumu watu cheaply hivi bila kufanya fare and
>> thorough analysis tutaishia pabaya"
>>
>> -Matinyi,unasema kuna upendeleo wa watu fulani kwenda kusoma nje kwa hiyo
>> unakubaliana nami kwamba upo bila kujali niwakundi gani katika jamii?
>> -Unataka na mapungufu ya wengine yatajwe kwa hiyo unakubali kwamba kwa
>> Mwenyeheri Nyerere hayo ni mapungufu?
>>
>> Vile vili ulisema;
>>
>> 3."Kama huyu mwandishi amesema kwamba suala la Amin lingewezwa kumalizwa
>> kwa mazungumzo, na nimeona kuna vijineno vya aina fulani hivi amevichomeka,
>> nadhani ni kupoteza muda kuisoma, labda kama lengo litakuwa kuokoa
>> upotoshaji. Na kwa lugha yake ya sentensi chache niliziona, huyu muungwana
>> anajulikana na yumo humu humu jamvini. Ni matatizo yale yale tu. Nyerere
>> alikuwa binadamu na kiongozi makini aliyeipenda nchi yake; na katika
>> utendaji wake kuna mambo alikosea lakini hatupaswi kuchambua uongozi wake
>> kwa uongo, udini, n.k."
>>
>> -Matinyi unajua kwanini tulienda vitani na kwa bahati nzuri Mzee Mtei
>> alishalizungumza hili.Kwa hicho kidogo naomba nilinukuu gazeti la Mwananchi
>> 9 Desemba 2011;
>>
>> Anasema mwaka 1971 Hayati Mwalimu Nyerere alisafiri na Rais wa Uganda
>> wakati huo, Milton Obote kwenda kwenye mkutano wa nchi za Jumuiya ya madola
>> ambao ulifanyika nchini Singapore.
>> Anasema Hayati Mwalimu Nyerere na Obote walikuwa marafiki sana na wakati
>> wakirejea nchini ndipo walikuta Idd Aman amefanya mapinduzi na kujitangaza
>> Rais wa Uganda.
>> Anasema wakiwa njiani kutoka katika mkutano huo, walipofika Nairobi nchini
>> Kenya, Obote aliandamana na hayati Baba wa Taifa mwalimu Nyerere hadi
>> jijini Dar es salaam.
>> Mtei anasema Obote alipewa makazi Dar es Salaam katika eneo la Msasani na
>> serikali ya Tanzania ilikuwa inamgharamia kwa kila kitu kama rais wa nchi.
>> Anasema kutokana na mauaji na hali ya usalama kuwa mbaya nchini Uganda,
>> Waganda wengi walikimbilia nchini Tanzania na kuanza kujipanga kurejea
>> nchini kwao kuikomboa nchi yao.
>>
>> -Ulitegemea Dikteta Nduli Idd Amin Dada afanye nini wakati kuna azma
>> tayari ya kumwwondoa madarakani?
>> Ndicho hicho unachokiona Mashariki ya Kongo ya Kabila na uhusiano wa
>> Rwanda na Uganda ulivyokuwa wakati RPF walipoanza harakati zao Uganda
>> mwanzoni mwa miaka ya 1990.Ifatilie vizuri historia ya Yoweri Kaguta
>> Museveni na hata ujue hiyo zawadi ya shule tuliyojengewa huko Kamachumu
>> Muleba.
>> -Matinyi unakubali kwamba kuna baadhi ya maeneo Mwenyeheri Nyerere
>> alikosea ni maeneo yapi?
>> -OAU walishindwa kulaani kwa kuwa sababu na maelezo yaliyokuwa yanatolewa
>> na upande wetu yalikuwa hayawaridhishi.
>>
>> Matinyi nadhani umeandika sana ndugu yangu na huwa najitahidi kukusoma ila
>> naomba uandike historia hiyo kama ulivyohaidi na nakushauri usome tena huo
>> waraka ukiwa na roho isiyo na chuki utaelewa maana kitu kinachozungumzwa ni
>> chakawaida mno kwa ambao tulikuwa hadhiri katika uongozi wa mtukuka huyo.
>>
>>
>>
>>
>> Walewale.
>> ------------------------------
>> *From:* Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
>> *To:* Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>
>> *Sent:* Tuesday, October 23, 2012 9:25 PM
>>
>> *Subject:* RE: [wanabidii] KITENDAWILI CHA NYERERE;
>>
>> Chengula,
>> Mimi nakiona huruma kizazi cha vijana wadogo wa leo wakiwemo watoto wangu;
>> kwamba watalishwa uongo mwingi sana na watu wenye mioyo mibaya dhidi ya
>> taifa letu. Dawa yake ni kuyajibu mambo haya na ikibidi kuandika vitabu ili
>> kuiweka rekodi sawa kama wafanyavyo wenzetu. Huwezi kukuta Wamarekani
>> wanapotosha historia na kazi za viongozi wao waliolijenga taifa lao; huwezi
>> hata siku moja. Sikubaliani na mambo fulani ya Nyerere na niliwahi
>> kuyaandikia lakini kumsingizia uongo na kupinda historia yake ni uhuni
>> mkubwa.
>> matinyi.
>>
>> > Date: Tue, 23 Oct 2012 17:11:37 +0000
>> > From: achengula@gmail.com
>> > Subject: RE: [wanabidii] KITENDAWILI CHA NYERERE;
>> > To: wanabidii@googlegroups.com; wanabidii@googlegroups.com
>> >
>> >
>> > Well said kaka Matinyi,
>> >
>> > ni kweli nimeupitia kwa makini nimekundua ni wale wake wa vuguvugu hili.
>> Mwandishi mwenyewe anajichanganya huwezi kupata hitimisho la makala yake.
>> Mambo aliyoyaandika yanatokana pengine na kile anachokifikiria ili kutimiza
>> lengo lake. Maandishi yake yalivyo kaa hayaonyeshi kayapata wapi. Labda
>> alete vyanzo vyake hapo nitaamini. Yanaonekana kuwa ni utafiti wa kubuniwa.
>> >
>> > Vita yake ni Muungano na Ukristo, hapa ndipo utajua ni wale wale.
>> Angalia alivyoelezea muungano hali kadhalika Ukatoliki, huna haja ya kujua
>> aliye andika ana itikadi gani ya kidini. Aliye uleta ni wale wale sawa na
>> mwandishi wenye malengo yale yele.
>> > -----Original message-----
>> > From: Godfrey Ngupula
>> > Sent: 23/10/2012, 18:12
>> > To: wanabidii@googlegroups.com
>> > Subject: RE: [wanabidii] KITENDAWILI CHA NYERERE;
>> >
>> >
>> >
>> > thanks Matinyi..i love people with sterio thinking like u do.People with
>> digital mind (and not analogue).Simple to grasp and analyse beyond the
>> reach of human eyes.Ngupula
>> >
>> >
>> >
>> > ------------------------------
>> > On Tue, Oct 23, 2012 5:52 PM EEST Mobhare Matinyi wrote:
>> >
>> > >
>> > >Kabalika,
>> > >Nilikuwa mapumziko ya chai/kahawa nikawa nasoma huu upupu. Nitaujibu
>> kwa vielelezo vyenye vyanzo rasmi. Huyu mtu ni mzushi mwenye ajenda ambayo
>> hata mtoto wa darasa la kwanza hawezi kushindwa kuibani. Ni hili genge
>> linalokua siku hizi ambalo siku si nyingi litatumbukiza kwenye matatizo
>> makubwa.
>> > >Matinyi.
>> > >
>> > >
>> > >
>> > >
>> > >Date: Tue, 23 Oct 2012 15:
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment