Thursday, 1 August 2013

[wanabidii] SERIKALI INAVYOCHOCHEA MIGOGORO YA ARDHI

SERIKALI INAVYOCHOCHEA MIGOGORO YA ARDHI 

Ndugu zangu 

Nilinunua ardhi sehemu moja katika mkoa wa dare s salaam yenye hekari 20 hivi na nilianza kuweka vitega uchumi hapo kwa miaka 2 uliyopita mpaka siku za karibuni tu niliposhikwa na mshangao  , mshangao wenyewe ni huu .

Baadhi ya viongozi wa serikali za mtaa wa maeneo yale kwa kushirikiana na halmashauri wameleta masuala ya mipango miji wakati kipindi chote hicho hili suala halikuwepo na kila mpango ulikuwa sawa tu mpaka tulipoamua kuwekeza hapo .

Sisi wenye ardhi hapo tumeambiwa tutalipwa asilimia 40 ya mauzo ya ardhi hiyo kwa bei ya sasa na tuiache , serikali itakuja kuchukuwa hiyo ardhi kwa matumizi mengine hiyo mipango miji wanayoisemea .

Kitu ambacho mimi nimeona ni kwamba kuna mwekezaji ameshaongea na baadhi ya madiwani na viongozi wengine kuhusu nia yake ya kutaka kuchukuwa maeneo hayo kwa ajili ya maslahi yake lakini huku upande wa pili tunadanganywa .

Sisi tumeamua kupeleka suala hili mahakamani na mahakama imeshapiga marufuku mpango huo kuendelea kwa upande wa serikali mpaka kesi itakapoisha .

Sijawahi kushuhudia migogoro ya ardhi kwa njia rahisi kama hii iliyonikuta mimi na kwa kweli nasema serikali yetu sikivu ya chama cha mapinduzi na viongozi wake iwe nakini na migogoro ya ardhi wanayojaribu kuichochea kwa visingizio vyovyote vile hali itakuwa mbaya siku zijazo .

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment