Friday, 30 August 2013

[wanabidii] NAOMBA USHAURI: PUA ZA MTOTO ZINAOTA VINYAMA.

Rafiki wanabidii,

Mtoto wangu mwenye umri wa miaka saba sasa, anapatwa na tatizo la kuota vinyama ndani ya pua na vinamsumbua sana. Hali hii nimesikia inawatokea watoto wengi siku hizi ila SIJUI NI KWA SABABU GANI!!?? Ningependa kujua sababu inayoleta hilo tatizo.

Pili, watu wengi wenye tatizo hili nimesikia wanafanyiwa upasuaji kuondoa vinyama hivyo, lakini pia nimejifunza kuwa huwa vinaota tena na hivyo upasuaji hurudiwa tena. Wapo wanaosema pia, kuna tiba mbadala ambayo aihitaji upasuaji. Ningependa kujua tiba hii mbadala na uhakika wake kama kuna mtu anaifahamu kabla sijaenda kwenye njia hii ya upasuaji.

Asante.
 
Martin Pius
P. O. Box 561, BABATI
Manyara
Tanzania
Mob: +255 78 447 4940 / +255 71 3474940
Email:malagila01@yahoo.co.uk

0 comments:

Post a Comment