Friday, 30 August 2013

[wanabidii] Rais Kikwete ateuliwa miongoni mwa watu mashuhuri duniani kujadili Utandawazi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Rais Kikwete ateuliwa miongoni mwa watu mashuhuri duniani kujadili Utandawazi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameteuliwa kuwa miongoni mwa watu wachache mashuhuri duniani ambao watajadili Mawazo na Njia Mpya za Utandawazi wa Usawa na Haki (New Ideas for a Fair Globalisation) na jinsi Utandawazi unavyoweza kuendeshwa kwa usawa zaidi na kunufaisha nchi zote duniani.

Watu hao mashuhuri wameteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mheshimiwa Ban Ki-Moon na Rais wa Kamisheni ya Ulaya, Mheshimiwa Jose Barosso kujadili njia mpya ya Utandawazi wa haki na usawa zaidi katika mkutano(retreat) wa watu wachache utakaofanyika katika Kijiji cha Alpbach, Austria, kuanzia kesho.

Mkutano huo wa siku mbili ambao utakuwa chini ya Wenyeviti Wenza Waheshimiwa Ban Ki-Moon na Barosso utafanyika chini ya kivuli cha Taasisi yaEuropean Forum Alpbach na Rais Kikwete ni kiongozi pekee wa Afrika aliyealikwa kushiriki katika mkutano huo.

Mbali na kushiriki katika majadiliano ya mada mbali mbali, Rais Kikwete amepangiwa kuzungumza katika kikao cha ufunguzi pamoja na waheshimiwa Ban Ki Moon na Barasso na pia kuzungumza katika kikao cha kufunga mkutano huo na wenyeviti wenzao hao wawili pamoja na Rais wa Muungano wa Austria, Mheshimiwa Dkt. Heinz Fischer.

Rais Kikwete aliondoka nchini usiku wa jana, Jumatano, Agosti 28, 2013, kwenda Alpbach tayari kwa mkutano huo ambao mada zake kuu zitakuwa ni Nishati Endelevu na Mabadiliko ya Tabianchi, Usalama wa Chakula na Lishe na Elimu na Vijana.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
29 Agosti, 2013

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment