majambazi nane yamlifanikiwa kupora zaidi ya Shilingi bilioni moja kutoka kwenye benki ya Habib African Ltd, iliyopo mtaa wa Livingstone na Uhuru, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema uporaji huo ulitokea leo saa 3:00 asubuhi.
Alisema majambazi hayo ambayo wawili kati yao yalikuwa na asili ya Kiasia yakisindikizwa na askari polisi aliyevaa sare, yalifika katika benki hiyo yakijifanya ni wateja lakini baada ya muda mfupi tu yalimwamuru Meneja wa benki hiyo, Daniel Matemba (55) na wasaidizi wake wayape ufunguo wa chumba maalumu cha kuhifadhia fedha (Strong Room), na hapo ndipo yalipofanikiwa kuchukua Sh milioni 792 za Kitanzania na dola za Marekani 181, 885 ambapo jumla ya fedha zote ni zaidi ya Sh. bilioni moja.
Imeelezwa kuwa majambazi hayo yalikuwa yakizungumza lugha ya Kiingereza na mara chache Kiswahili kwa shida.
Meneja anadaiwa kukataa kubonyesha kitufe cha kuomba msaada.
Meneja huyo pamoja na mlinzi wanashikliwa na polisi kwa mahojiano na uchunguzi zaidi baada ya uchunguzi wa awali kuonesha kuwa yalikuwepo mawasiliano baina ya baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo na majambazi hayo.
Kamanda Kova ametangaza zawadi ya Sh milioni 100 kwa mwananchi yeyote atakayetoa taarifa na kufanikisha kukamatwa kwa majambazi hayo.
-- Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema uporaji huo ulitokea leo saa 3:00 asubuhi.
Alisema majambazi hayo ambayo wawili kati yao yalikuwa na asili ya Kiasia yakisindikizwa na askari polisi aliyevaa sare, yalifika katika benki hiyo yakijifanya ni wateja lakini baada ya muda mfupi tu yalimwamuru Meneja wa benki hiyo, Daniel Matemba (55) na wasaidizi wake wayape ufunguo wa chumba maalumu cha kuhifadhia fedha (Strong Room), na hapo ndipo yalipofanikiwa kuchukua Sh milioni 792 za Kitanzania na dola za Marekani 181, 885 ambapo jumla ya fedha zote ni zaidi ya Sh. bilioni moja.
Imeelezwa kuwa majambazi hayo yalikuwa yakizungumza lugha ya Kiingereza na mara chache Kiswahili kwa shida.
Meneja anadaiwa kukataa kubonyesha kitufe cha kuomba msaada.
Meneja huyo pamoja na mlinzi wanashikliwa na polisi kwa mahojiano na uchunguzi zaidi baada ya uchunguzi wa awali kuonesha kuwa yalikuwepo mawasiliano baina ya baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo na majambazi hayo.
Kamanda Kova ametangaza zawadi ya Sh milioni 100 kwa mwananchi yeyote atakayetoa taarifa na kufanikisha kukamatwa kwa majambazi hayo.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment