Friday 30 August 2013

[wanabidii] Re: [Wanazuoni] TABIA ZA VIONGOZI WETU KUTOROKA

Yona,
Wanatoroka kwani wapo kifungoni?, Na hizo taarifa za wanapotakiwa kulala huwa zinawekwa kwenye gazeti gani ili na wengine tukusaidie kuwaripoti iwapo tutawaona huku Bagamoyo.


From: Yona Maro <oldmoshi@gmail.com>
To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>; Wanazuoni <wanazuoni@yahoogroups.com>
Sent: Friday, 30 August 2013, 13:29
Subject: [Wanazuoni] TABIA ZA VIONGOZI WETU KUTOROKA

 
Ndugu zangu ,

Kuna tabia na sasa umekuwa utamaduni wa baadhi ya viongozi wa nchi kutoroka usiku kule walipopangiwa kufikia wakati wa safari zao za sehemu mbalimbali wengine ni pale wanapokuwa kwenye nyumba walizopangiwa na serikali lakini usiku wao hutoroka kwenda wanapojua wao .

Kuna tukio limetokea katikati ya wiki hii ambapo kiongozi mmoja wa nchi alifumwa saa 6 usiku tena akiwa na msafara wake , Mwingine aliwahi kukutwa na zahama karibu na nyumbani lounge na rais wa zamani ndugu Mwinyi nae aliwahi kukutwa na balaa maeneo ya ubungo baada ya kuchelewa .

Ni vizuri kujua hawa viongozi wa nchi waliapa na kuridhia taratibu za nchi kuhusu usalama wao lakini wanapoamua kukaidi amri hizi na kutembea wanavyojua wao wanakuwa wanaharibu taratibu za usalama wa taifa kuhusu usalama wao na kusababisha matatizo mengine kwa wale wanaowalinda muda wote .

Nashauri wanausalama kutumia nguvu kurudisha viongozi majumbani kwao au pale wanapopitiliza muda wa kukaa nje bila sababu za msingi walazimishwe kurudi kwenye sehemu walizopangiwa kwa muda unaotakiwa .


--
Find Jobs in Africa Jobs in Africa
International Job Opportunities International Job Opportunities
Jobs in Kenya Jobs in Kenya

__._,_.___
Reply via web post Reply to sender Reply to group Start a New Topic Messages in this topic (1)
Recent Activity:
.

__,_._,___


0 comments:

Post a Comment