Saturday, 31 August 2013

[wanabidii] WAPATA UFADHILI WA MASOMO KUTOKA SERIKALI YA WATU WA CHINA KUPITIA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo uliopo jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wanafunzi nane waliopata ufadhili wa masomo ya shahada ya uzamili katika fani ya mafuta na gesi kutoka Serikali ya watu wa  China. Wanafunzi hao wanatarajia kuondoka nchini hivi karibuni pia wanafunzi wengine 10 wamepata ufadhili wa masomo kama hayo kutoka Serikali ya Brazil.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, akimpongeza mmoja wa wanafunzi hao, Grace Mkongwa, kutoka mkoa wa Njombe, ambaye amepata ufadhili wa masomo ya shahada ya uzamili katika fani ya mafuta na gesi kutoka Serikali ya watu wa China wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wanafunzi hao nane waliopata ufadhili huo iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo  jijini Dar es Salaam. Grace ni mmoja kati wa wasichana saba waliopata ufadhili wa kusomea masomo hayo katika nchi za China na Brazil jumla ya wanafunzi 18 wamepata ufadhili wa masomo.
Katibu Mkuu wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi (watatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya vijana waliopata  ufadhili wa masomo ya shahada ya uzamili katika fani ya mafuta na gesi kutoka Serikali ya watu wa China mara baada ya kumalizika kwa  hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo uliopo jijini Dar es Salaam. Jumla ya wanafunzi 18 wamepata ufadhili wa masomo katika nchi za China na Brazil. Picha na Anna Nkinda - Maelezo

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment