Thursday, 29 August 2013

[wanabidii] Kuwafukuza wahamihaji haramu ni matokeo, Serikali ishughulikie kiini

Hivi karibuni kumekuwepo na hekaheka za kuhakikisha waamihaji kutoka nchi jirani wanarudishwa makwao.

Hii ni baada ya kukaa na miaka mingi zaidi na baadhi ya waliorudisha wamezaliwa hapa Tanzania.

Sababu kubwa ya kuwarudisha ni kutokana na vitendo wa wizi wa kutumia silaha na kuteka magari, kushamiri hapa nchini hasa mkoani Kagera. Hivyo wenye mamlaka wameona kuwarudisha waamihaji kwao ndio njia ya kutatua tatizo ila wamesahau kuwa wao pia ni wahusika wa tatizo mfano mipakani wamewaweka watu wasio waaminifu na kuishia kulalamika hasa jamaa yangu aliyepo mpakani mwa
Tanzania na Uganda (Mtukula), viongozi hao hao wamekuwa wakiwakamata wahaohusika wa vittendo vya wizi (wakiwemo waamihaji na Watanzania wazawa) na kuwaachia mara baada ya kutoa chochote.

Napenda kuwaambia viongozi wangu bado tatizo liko palepale na huenda likakua zaidi kwani baadhi ya waamiaji wamerudi kwao na silaha wamewaachia Wabongo wenzetu na wahamihaji walioondoka kwa kuwa tayari wana mahusiano na majambazi wa Kitanzania mmewapa mwanya wa kuwatafutia silaha zenye viwango zaidi.

Wezi wa hapa Tanzania kwa sasa watakaa kimya ili mdhani kuwa wahalifu walikuwa wahamiaji kumbe ndivyo sivyo na wakati wa sikukuu hasa Noel na Mwaka Mpya wataanza shughuli!

Nimeandika hili kwani si mara ya kwanza maamuzi kama haya kuchukuliwa, hivyo wenye dola ni bora kuwa jasiri na kushugulikia kiini cha tatizo na si matokeo ya tatizo na maneno kuwa mengi na kutupotezea muda wa kuyasikiliza!

Nawasilisha,
KALYANKOZILE


Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/08/kuwafukuza-wahamihaji-haramu-ni-matokeo-serikali-ishughulikie-kiini.html#ixzz2dLLozdt7

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment